Rais Magufuli, nakuomba umteue Pascal Mayalla kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,900
141,836
Siyo kwamba huyu aliyepo Dr Abbas hafanyi vizuri la hasha, ni kwa sababu mambo mengi mazuri unayoyafanya yanahitaji mkongwe wa habari aliyetumikia awamu zote kuweza kuyaelezea kwa ufanisi na ulinganifu.

Nikisema zaidi utaona kama nampamba huyu Mayalla, basi nikuombe tu mh Rais ipitie CV ya nguli huyu wa habari za maendeleo na ikikupendeza atusaidie katika kuhabarisha juu ya maendeleo yanayopatikana siku hadi siku katika taifa letu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Upo sahihi MwanaCCM. Hizi Njaa Zikihamia Kichwani inakuwa shida saana. Pascal anaganga saaana Safari hii!
 
Mkuu acha roho mbaya kwani aliyopo anakukera nini?Kwani aliopo aliyemteua alikosea? Mh.Rais wangu hao ndio wachochezi usiwasikilize.
 
Tatizo la Mayala alijitanabaisha Kama afisa habari wa Lowasa 2015 na alikuwa Katika list iliyodakwa ya vyeo vya watu ambao wangepewa nafasi ipi Kama Lowasa angekuwa Raisi.Anyway Mayalla haku project vizuri future .Wengi waliingizwa pori na Lowassa viongozi wa serikali na mashirika ya umma na private sector akiwemo Mayalla
 
Swali ateuliwe sawa.
Tatizo wengi watasema kwa vile ni kabila na dini yake.
Labda ungelisema ampagiwe kazi ili amsaidie Mh.Rais au msemaji aliyepo apangiwe kazi nyingine/apande cheo.
 
Tatizo la Mayala alijitanabaisha Kama afisa habari wa Lowasa 2015 na alikuwa Katika list iliyodakwa ya vyeo vya watu ambao wangepewa nafasi ipi Kama Lowasa angekuwa Raisi.Anyway Mayalla haku project vizuri future .Wengi waliingizwa pori na Lowassa viongozi wa serikali na mashirika ya umma na private sector akiwemo Mayalla
Lowasa si mwanachama wenu? Iweje mnawachukia wafuasi wake!!!
 
Walichokifanya 2015 kibaya mno.Nilikwenda Kilimanjaro kuangalia Magufuli anakubalika au la nikaenda kanisa moja la KKKT nikakuta kibao karibu na kanisa kimeandikwa Pombe hapa haitakiwi Ni marufuku kwenye kanisa .Nikauliza Nini maana yake? Nikaambiwa John Pombe Magufuli marufuku kupewa kura.Jina pombe lilitumika kampeni kumnyima kura makanisani Kama secret code.Lowasa alichoifanyia CCM siyo no no no no
 
At nini? kwani inaruhusiwa?
Walichokifanya 2015 kibaya mno.Nilikwenda Kilimanjaro kuangalia Magufuli anakubalika au la nikaenda kanisa moja la KKKT nikakuta kibao karibu na kanisa kimeandikwa Pombe hapa haitakiwi Ni marufuku kwenye kanisa .Nikauliza Nini maana yake? Nikaambiwa John Pombe Magufuli marufuku kupewa kura.Jina pombe lilitumika kampeni kumnyima kura makanisani Kama secret code.Lowasa alichoifanyia CCM siyo no no no no
 
Tatizo la Mayala alijitanabaisha Kama afisa habari wa Lowasa 2015 na alikuwa Katika list iliyodakwa ya vyeo vya watu ambao wangepewa nafasi ipi Kama Lowasa angekuwa Raisi.Anyway Mayalla haku project vizuri future .Wengi waliingizwa pori na Lowassa viongozi wa serikali na mashirika ya umma na private sector akiwemo Mayalla
Bashe hakuwa kwenye listi ya Lowasa?
 
Amteue aisee anahangaika sana mtandaoni kugeuza nyeusi iwe nyeupe na nyeupe iwe nyeusi ili kumpamba jiwe na awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom