Rais Magufuli nakuomba uhutubie Taifa 'live' mkesha wa Mwaka Mpya, huenda ukawa mwaka wako wa mwisho ukiwa Rais wa Tanzania

Yacoubu

Member
Nov 23, 2019
29
123
Tangu uingie madarakani, haujawahi kuhutubia taifa live kupitia vyombo vya habari, badala yake umekuwa ukitoa salaam kupitia msemaji wako. Hali hii haijengi umoja na mshikamano.

Tofauti na watangulizi wako, haujawahi kutoa hotuba ya kila mwisho wa mwezi badala yake hotuba zako ni za majikwaani tu.

Naomba mwaka huu wa TANO wa uongozi wako uoneshe tofauti na Mungu atakubariki.

Ushindani uliopo ndani na nje ya chama ni mkubwa sana. Huenda 2020 usirudi Magogoni, maana ikulu kuhamia Dodoma siyo miaka hii, watahamia wengine ila siyo Rais. Kwahiyo ni vyema mwaka uliobaki ukautumia vizuri kurekebisha penye kasoro na kuboresha zaidi pale panapoenda vizuri.

HERI YA KRISMAS NA MWAKA MPYA.

......UPDATES.....
January 01, 2020 saa 12:00pm

Rais amegoma kabisa kulihutubia Taifa. Si kwa maandishi wala kwa mdomo 'live'.

Hii ni mpya kabisa, haijawahi kutokea ashindwe kutuma salamu za mwaka mpya kwa maandishi.

Je, hana jipya?
Je, hapendi wananchi?
JE KUNA HAJA YA KUMUONGEZEA MUHULA MWINGINE?
 
Sisi hatutaki hotuba, tunataka SGR, Umeme Bwawa la Nyerere > 2100 MW, highway system, economic growth > 7%, BRT system Dar nzima, Usalama Barabarani ajali na vifo barabarani vimepungua kwa zaidi ta 70%, Huduma za Afya kuanzia juu mpaka chini vijijini, Elimu, Maji ya kunywa safi na salama kila mahali,n.k.
Hivyo ukitaka hotuba nzuri kamsiklize Obama YouTube na hope yake, lkn hapa kwetu ni kazi tu!
 
Nchi haiendeshwi kama wewe unavyopenda, au marekani sijui wapi mnapotelea mifano nchi zao kila raia anatoa maelezo jinsi ya uendeshaji wa nchi?
 
Tunataka watu waache kutekwa, na kupotea kama wana makosa washitakiwe tu, Sote tuna haki ya kuishi kama wengine walivyo na haki
Sisi hatutaki hotuba, tunataka SGR, Umeme Bwawa la Nyerere > 2100 MW, highway system, economic growth > 7%, BRT system Dar nzima, Usalama Barabarani ajali na vifo barabarani vimepungua kwa zaidi ta 70%, Huduma za Afya kuanzia juu mpaka chini vijijini, Elimu, Maji ya kunywa safi na salama kila mahali,n.k.
Hivyo ukitaka hotuba nzuri kamsiklize Obama YouTube na hope yake, lkn hapa kwetu ni kazi tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi..
Umeona like yangu huko?
 
Back
Top Bottom