Rais Magufuli nakujuza, usishushe upanga uliopewa na watanzania

Ndendende

Member
Oct 8, 2016
40
125
Usiushushe upanga uliopewa na watanzania dhidi ya wabadhirifu. Wewe ni kamanda mkubwa mwenye uthubutu na weledi ambaye hajawahi tokea katika kiza chetu kilichojaa utandawazi na utandawizi. Mungu jaalia daima anakuongoze.

Watanzania wanaimani katika mikono, kichwani kwako na roho yako, hata hivyo, watanzania tunasema wapingaji wapo tu, hata mitume ya munge wetu mmoja ilipingwa. Mimi nasema usishushe upanga uliopewa na watanzania waliokupenda.

Rais wangu nakupongeza kwa mengi saana, sitaweza kuyataja kwani mungu ameyataja moyoni mwako na umeyatekeleza, ila.... Nakuomba nikwa, bie machache tuu...

Rais wangu nakwambia, watumishi wanasubiri kauli yako kuhusu mishahara kwani budget yako ambayo pia ni ya kuvutia haijaongelea watumishi wako, najua wajua kuwa kwa watumishi wako wanaishi maisha ya hovyo na ukizingatia hali ya uchumi kwa sasa maisha yamekuwa juu na makato ni makubwa.

Mfano kwa walimu na wauguzi wasaidie nyumba, hata kwa kutangaza harambee kama ulivyotangaza kwenye ya shule madawati tulifaulu vema, hawa huruma kwani pesa za kulipia pango ambazo hulipa kwa mishahara yao, walipwe stahiki wanazodai, ili ufanisi uonekane kutoka kwao.

Ningekuwa sio muumini wa democracy ningesema tangaza kuitawala ardhi hii mpaka mungu wetu akutake umuangaze mwenye nia njema na ardhi hii. Ila mimi ni muumini wa democracy, hivyo mwaka 2020 naamini utashindwa kwa 94% ya kura za watanzania na utatutumikia mpaka 2025.

Pia rais nakwambia, tumia pia muda na kipindi hiki kimkakati kumpata mwema kwa watanzania ili ifikapo 2025 wepesi upewe na mungu jaalia kwa mamlaka ya kiti hapo ndani ya ccm kwa maana ya kuendeleza mazuri yenye tija kwa watanzania.

Rais Magufuli nakwambia, hapa tanzania hakuna chama mbadala, ila vilivyopo ni vyama ngekewa na vya kupiga deal tu. Hii namaanisha kwamba hakuna chama sahihi zaidi ya ccm mpya chini ya uongozi wako, vingine ni miyayusho na vya matukio na kustaajabu tu.

Rais nakwambia, watanzania tunakupenda kama vile wimbo wetu wa taifa na wa tanzania.
Tunakupenda,
Tunakuhitaji,
Mungu akulinde kwa afya njema na ulinzi wake daima.
2020 tutakuchagua kwa huu uzalendo wako.

Ndendende
18, June, 2017
 

Genghis Khans

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
502
500
Nathani CCM wameanza mchakato wa kuanzisha chuo cha leadership. Nathani kitatoa viongozi watakao weka maslahi ya nchi kwanza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom