MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Haifahamiki kwa nje (officially) kilichokuwa kinaongewa na viongozi wetu wakuu wa nchi lakini duru za kisiasa za ndani zinasema, Suala la Baraza la Mawaziri lilikuwa kwenye ajenda!
Ikumbukwe kuwa, siku moja kabla ya Waziri Mkuu, Majaliwa hajafanya ziara ya kushtukiza bandarini Dar es Salaam na kuwaita maofisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kikaoni kujadili changamoto kuhusu ufanisi na mapato alikutana na Rais Magufuli kwenye ofisi yake.
Tusishangae kesho kama tutasikia serikali ya Rais Magufuli ikiwashangaza tena watanzania kwa tukio lingine la kihistoria.
The man is on mission!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, (kushoto) akizungumza na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, wakati Rais na Waziri Mkuu walipomtembelea Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015 kwa mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (kushoto) akiagana na Makamu wake, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Nov 30, 2015. Wa pili (kulia) ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais, Mohamed Khamis.