Tunkamanin
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 951
- 865
Kupenda uadilifu na kuchukia ufisadi, kupenda haki na kuchukia unyanyasaji, ni mambo ambayo kiongozi wetu wa nchi anayo na nani basi asiyelifahamu jambo hilo kwa Mh. wetu? Lakini je kupenda peke yake, au kuchukia peke yake ndio lengo lake? jibu hapana......
Najua Rais wangu anaumiza kichwa, halali usingizi ukanoga, hali chakula kikaingia vizuri tumboni, anatafuta namna ya kufikia uadilifu wa kiwango cha juu, anatafuta namna ya kuweka hisia zake katika vitendo ili kuwasaidia wananchi wa Tanzania.
Naam hapo ndipo ulipo ugumu, unachukia ufisadi, je unauondoaje? unataka watoto wa tanzania wasome bila Bughudha, je unafanyaje ili wafikie hapo? Unataka kueneza uadilifu katika jamii, wanyonge wawe daraja sawa na watawala, hayo yote ni mambo tunayoyataka.
Amini hakuna jipya katika dunia ambalo waliopita kabla yetu hawajafanya, wapo viongozi waadilifu mno walipita katika ulimwengu huu, wakaeneza haki, usawa , uadilifu, neema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu zikaenea katika ardhi zao.
Hazina kubwa ipo kwenye vitabu, mimi naweka historia hapa ya Sayidnaa Umar, huyu alifanikiwa kueneza uadilifu na kupambana na ufisadi angalia namna alivyoongoza, utajifunza kitu.
Siku moja alishawahi kusema baada ya tumbo lake kutoa sauti kwa ajili ya njaa " Alisema wewe tumbo, nakuapia kuwa hutakaa uonje nyama mpaka watoto wa nchi hii watakapo shiba" speech yake wakati anapokea madaraka ilikua hivi.
Tukumbuke kuwa huyu alikua kiongozi wa nchi ya kiislamu kipindi hicho lakini yako mengi ya kujifunza hata kama ni wa dini nyingine.