Uchaguzi 2020 Rais Magufuli na Tundu Lissu wote ni Wakatoliki wazuri. Je, Kanisa halioni umuhimu wa kuwapatanisha?

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Ni jambo lililo wazi kwamba hawa watu wawili wana mengi yanayofanana na kukinzana.

Wote ni public figures na wanasiasa tofauti ni kwamba mmoja ni rais wa nchi na mwingine ni mwanasiasa anayependwa sana kwa sasa.

Wote hawa ni Wakatoliki wazuri sana na wanaoijua imani yao vema.

Kwasababu ambazo sioni haja ya kuzieleza hapa, hawa wote wana tofauti kubwa hasa kwa mambo yalivyokuwa kwa kipindi cha miaka mitatu nyuma mpaka sasa.

Swali langu kwa kanisa Katoliki:
Je, halioni umuhimu wa kuwapatanisha Hawa waumini wake wawili? Je kanisa linafurahishwa na Hali iliyopo kwa sasa baina ya wawili hawa?

Nini mchango wa kanisa katika kubeba hisia za Lissu na kumtuliza? Na ni nini mchango wa kanisa katika kumpa Mh Rais Magufuli tulizo la moyo linalotokana na cheche za Lissu?

Mwisho wa siku sisi ni Watanzania.

Usiku mwema.
 
Natamani siku moja niwaone wawili hawa wakikumbatiana kwa tabasamu pana lenye bashasha hakika itakuwa ni ushindi kwa taifa letu.

Amani iwe kwako Mh Rais Magufuli
Amani iwenkwako Mh Tundu Lissu
Amani iwe kwa wana CCM wote
Amani iwe kwa wana Chadema wote
Amani iwe kwa Watanzania wote
 
Superbug,

Hii ni nchi ya wote na ndicho Tundu Lissu anasema tena na tena na siyo suala la watu wawili yaani Magufuli vs. Lissu.

CCM Mpya mmevurugwa mawazo kiasi cha kutaka kuitoa nchi mmliyoikabidhi kwa mtu mmoja na sasa mawazo yenu mnataka kujenga nadharia anayoikataa Tundu Lissu kuwa nchi hii haiwezi kukabidhiwa kwa mtu mmoja au genge la watu wachache mfano maaskofu au masheikh n.k. kutupa muelekeo.

Muelekeo wenye afya njema kwa nvhi tutaupata kwa kupitia demokrasia pana ya kijamii kupitia vyama vingi, watawala kuwa wasikivu, bunge huru n.k

Tundu Lissu na waTanzania wengi wanapenda ushirikishwaji mpana wa wananchi katika kuamua mustakabali wa nchi yao.

Ushirikishwaji huo unaanzia mfano Halmashauri ya Chama NEC CCM, Kamati Kuu, iwe na uwezo wa kumdhibiti mgombea rais wao akiwa amepewa mamlaka ya kiuongozi.

Nchi kuwa na Bunge la kuiwajibisha serikali na Mahakama kuwa huru kutafsiri sheria bila kuingiliwa na dola/ serikali kuu, huo ndio msimamo wa Tundu Lissu, CHADEMA na watu-huru waTanzania na siyo mustakabali wa nchi "umilikishwe" kwa mtu au watu wawili au kikundi cha watu au chama kimoja.

WaTanzania wa 2020 wanaenda kukataa kurudisha ile dhana iliyopo ambayo ni ukweli kuwa sasa wamekuwa 'mateka tangu 2015' kwa vile wamepiga kura kumkabidhi mtu ofisi ya Urais.

WaTanzania wanataka uhuru Na kazi, Uhuru Na Maendeleo, Uhuru Na umoja na pia haki ya mlipa-kodi kutoa mapendekezo kodi yao itumike vipi na siyo kumkabidhi mtu mmoja aamue kutumia pesa za walipa kodi itakavyompendeza kama ilivyo sasa.
 
superbug,

Lissu, kwa utu wake, matendo yake na maneno yake, bila hata kujua dini yake, mtu yeyote anaweza kutambua kuwa ni muumini wa dini fulani inayoeleweka lakini huyo mwingine ni Mfarisayo anayekwenda kila nyumba ya Ibada ili aonekane na watu.

Mfarisayo anaonekana kwenye misikiti ya madhehebu yote na makanisa ya madhehebu mbalimbali ikiwa ni pamoja na yale ya Manabii wa Uwongo kama lile la mzee wa Upako.
 
Unalisema Kanisa Katoliki hilihili lililo simamia utekeleza mauaji ya Kimbari ya huko Rwanda 1994? Au unasema Katoliki ipi? Hilihili la akina Pengo na Methodius Kilaini? Linaloshindwa kukemea viongozi wa kisiasa kwa mambo wanayoyafanya yasiyokuwa mema machoni pa binadamu?

Unalisemea Katoliki hili ambalo wazazi wkitenda kosa linamgharimu na mtoto au mtoto akitenda kosa linagharimu na wazazi?

Hivi ni hii Katoliki yetu ambayo usipolipa michango ya jumuia hupewi huduma ya Kanisa? Unalisema hili ambalo ibada ya marehemu tajiri anaenda Padri/Askofu na kwa maskini wanaenda Makatekista?

Au sijakusikia vizuri uongeze sauti mkuu.
 
Mwaka 2018 mwezi Machi tarehe 3
Dr. LWAITAMA, AMVAA MAGUFULI ATAKA ADHIBITIWE
Wananchi wanataka Maendeleo ndani ya uhuru, hawataki kupokonywa uhuru wao kwa kisingizio cha Maendeleo ya Vitu

Watu hawataki kuwa mateka wa kikundi cha watu kwa kuwatisha kupitia chama dola. Chama dola siyo chama cha kweli cha kisiasa maana hakina ushawishi bali kinatumia dola kutisha watu.
 
Well said 👏 👏

Lakini Mkuu usichokijua ni kuwa Jiwe ndiye ambaye hataki upatanishi huo kwa kujianini kuwa analo Jeshi la Polisi, ambalo yeye anaamini linaweza kumfanyia shughuli zote za kuwaonea wapinzani pale anapoliamuru kufanya hivyo..........

Lakini naamini kwa Tundu Lissu yuko tayari kwa upatanishi huo hata ukitokea Leo hii
 
Superbug,

Hii ni nchi ya wote na ndicho Tundu Lissu anasema tena na tena na siyo suala la watu wawili yaani Magufuli vs. Lissu.

CCM Mpya mmevurugwa mawazo kiasi cha kutaka kuitoa nchi mmliyoikabidhi kwa mtu mmoja na sasa mawazo yenu mnataka kujenga nadharia anayoikataa Tundu Lissu kuwa nchi hii haiwezi kukabidhiwa kwa mtu mmoja au genge la watu wachache mfano maaskofu au masheikh n.k. kutupa muelekeo.

Muelekeo wenye afya njema kwa nvhi tutaupata kwa kupitia demokrasia pana ya kijamii kupitia vyama vingi, watawala kuwa wasikivu, bunge huru n.k

Tundu Lissu na waTanzania wengi wanapenda ushirikishwaji mpana wa wananchi katika kuamua mustakabali wa nchi yao.

Ushirikishwaji huo unaanzia mfano Halmashauri ya Chama NEC CCM, Kamati Kuu, iwe na uwezo wa kumdhibiti mgombea rais wao akiwa amepewa mamlaka ya kiuongozi.

Nchi kuwa na Bunge la kuiwajibisha serikali na Mahakama kuwa huru kutafsiri sheria bila kuingiliwa na dola/ serikali kuu, huo ndio msimamo wa Tundu Lissu, CHADEMA na watu-huru waTanzania na siyo mustakabali wa nchi "umilikishwe" kwa mtu au watu wawili au kikundi cha watu au chama kimoja.

WaTanzania wa 2020 wanaenda kukataa kurudisha ile dhana iliyopo ambayo ni ukweli kuwa sasa wamekuwa 'mateka tangu 2015' kwa vile wamepiga kura kumkabidhi mtu ofisi ya Urais.

WaTanzania wanataka uhuru Na kazi, Uhuru Na Maendeleo, Uhuru Na umoja na pia haki ya mlipa-kodi kutoa mapendekezo kodi yao itumike vipi na siyo kumkabidhi mtu mmoja aamue kutumia pesa za walipa kodi itakavyompendeza kama ilivyo sasa.
Kama ambavyo amefanya ubinafsi wa hali ya juu, kwa kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa katika kijiji chake cha Chatoooo!
 
Mkuu ushauri wako ni mzuri sana, kwa kuwa hata maandiko matakatifu hutuambia wana heri wapatanishi kwani watapewa tuzo zao wakati ukifika kule mbinguni. Suala la upatanishi na tuzo yake, hii ni ahadi kutoka kwa Mungu mwenyewe kwa watu wake.

Lakini wote tu mashahidi kuhusu kongamano la amani lililofanyika hivi juzi kati lenye kuwahusisha viongozi wetu wa kidini. Sifa za mpatanishi ni lazima awe mkweli, kuaminika na pande zote zilizopo kwenye mgogoro na pia awe na uwezo usiotia shaka katika kusimamia haki.

Kwa sifa hizi za upatanishi hawa viongozi wetu itakuwa ni vigumu sana kufanikiwa. Ebu jaribu kufikiria tu, katika kuzungumzia suala la amani ya nchi yetu, ktk kongamano lao viongozi wa kidini hawakuona umuhimu wa kuwaalika viongozi wa upinzani isipokuwa ni kujipendekeza kwa serikali na kuwapiga vijembe vya wazi kuwa wao ndiyo tishio la amani ya nchi yetu.

Viongozi wa kidi ambao kila uchao huuibili haki ya Mungu na uvumilivu wake dhidi ya dhambi za wanadamu, wanatoa mapendekezo juu ya uwepo wa amani na kwa makusudi wanakwepa kuzungumzia haki za kiraia ambazo serikali wanayoisifu ilikwepa kuzitoa.

Mimi naona viongozi wetu wa kidini wameamua kuunga mkono juhudi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na wala si ya waumini wao wanaowaongoza. Hawasukumwi na suala la upatanishi kwa kuwa wanaogopa kuonekana wanakinzana na viongozi wa serikali wenye kupenda kusifiwa.
 
LWAITAMA :WASOMI WENGI WANATUMIWA NA WANAWATUMIKIA WATAWALA

Tulichokipigania ili nchi ipate uhuru, je sasa hapa katikati kamebadilika inabidi tuanze mapambano kudau uhuru wetu ?
Superbug au unatumika tusione kwamba kuna kitu kikubwa tunakipigania lakini unataka kuwaaminisha hakipo bali kuna uhasama wa kibinafsi baina ya wanasiasa hawa wawili tu na kuwa maaskofu wakiwapatanisha nchi itakuwa haina malalamiko mengine toka kwa wananchi ?
 
Back
Top Bottom