Rais Magufuli na timu yako yote chapeni kazi, miluzi mingi isiwapotezee muelekeo

Mimi na amini hata ukatoka hapo nje now na kuanza kugawa IST bure, bado watu watalalamika.
Mara kwanini IST kama unajiona una hela ungetupa RAV4, Hela ya mafuta je? Si bora ungenipa mtaji kuliko gari, unanipaga gari hujailipia bima bwana, n.k.
Ubinadamu shida...
Issue sio watu kalalamika,hoja hapo ni watu wanalalamika nini??wanacholalamikia kina ukweli??...so kwa iyo kwa kuwa ni kawaida watu kulalamika unataka watu wasilalamike wanapoona maswala ya kubambikiziana kesi....utekaji na kubambikiana kesi ni uhuni wa kishamba
 
Unao uhakika kuwa huko kutekana chanzo ni yeye?, unaweza ukatuwekea ushahidi halisi unaomhusisha yeye kama mkuu wa nchi?. Jifunze kuielewa (system) ya nchi inavyofanya kazi.

Hata kama anatimiza wajibu wake, kumwambia kwamba anachokifanya ni kizuri sio jambo lenye kuhitaji nguvu nyingi za kimwili na kiakili.

Unaweza ukawa unatimiza wajibu wako, lakini unautimiza vipi ndio suala muhimu.
Kama mambo mazuri yanayofanyika nchini chanzo huwa ni yeye kwanini kwenye mabaya huwa mnamtoa yeye na kuonekana hausiki na lolote
 
Mkuu unadhani wanao tukana na kubeza hawayaoni hayo?? Wanaona sana ila lilijina la UPINZANI limewaharibu sana, wao wanapinga na kukusoa kila kitu.
Baba Mkwe Magu piga kazi nabii hasifiwi kwao na akisifiwa ujue hayupo kwao.
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa marais wenye haiba yenye nguvu sana (charisma).
Ucheshi wake, uwezo wake kiakili na uwezo wa kuweka mizani ya kimahusiano ni sifa yenye kufanana na watu waliozaliwa mwezi wa kumi (libra).

Watanzania walimpachika mzee huyu jina la utani wakimuita Vasco Da Gama, kwa jinsi alivyokuwa akifunga mikanda ya ndege mara kwa mara. JK ni mstaarabu sana, alizodolewa na kukejeliwa, yeye akiishia kutabasamu na kupuuzia.

Leo hii kinaibuka kichekesho eti kwamba haya anayoyafanya JPM ni muendelezo wa yale yaliyoanzishwa na JK. Lakini ni huyo huyo JK ambaye baadhi ya wanajamii walidai kuwa zaidi ya kutembea hakuna kipya ndani ya awamu yake ya uongozi!.

JPM na team yako nzima ya utendaji, chapeni kazi, msisikilize miluzi mingi. Haya mnayoyafanya yatakuja kuongelewa awamu ya sita wakati wanaharakati wakijenga hoja za kuuponda uongozi wa wakati huo.

Pigeni kazi, legacy itakuja kuonekana miaka ijayo. Hivyo viwanja vya ndege vitakuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wa miongo ijayo. Hizo bandari zinazoongezwa ukubwa, zitakuwa ni muhimu kwa wafanyabiashara wa miaka mingi ijayo.

Hizo rada nne zinazoweka kimkakati, faida zake ni kubwa sana kiuchumi katika miaka ijayo.

Pigeni kazi msipoteze muelekeo eti kwa sababu watu wanalalamika.

Nawatakia Watanzania wote nane nane njema.
 
Kama mambo mazuri yanayofanyika nchini chanzo huwa ni yeye kwanini kwenye mabaya huwa mnamtoa yeye na kuonekana hausiki na lolote
Mada ya huu uzi ina lengo la kuwatia moyo wote wenye mamlaka kwa umoja wao. Collective responsibility imejumuishwa kwenye mada hii.
 
Mimi na amini hata ukatoka hapo nje now na kuanza kugawa IST bure, bado watu watalalamika.
Mara kwanini IST kama unajiona una hela ungetupa RAV4, Hela ya mafuta je? Si bora ungenipa mtaji kuliko gari, unanipaga gari hujailipia bima bwana, n.k.
Ubinadamu shida...
Kweli kabisa mkuu.
 
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa marais wenye haiba yenye nguvu sana (charisma).
Ucheshi wake, uwezo wake kiakili na uwezo wa kuweka mizani ya kimahusiano ni sifa yenye kufanana na watu waliozaliwa mwezi wa kumi (libra).

Watanzania walimpachika mzee huyu jina la utani wakimuita Vasco Da Gama, kwa jinsi alivyokuwa akifunga mikanda ya ndege mara kwa mara. JK ni mstaarabu sana, alizodolewa na kukejeliwa, yeye akiishia kutabasamu na kupuuzia.

Leo hii kinaibuka kichekesho eti kwamba haya anayoyafanya JPM ni muendelezo wa yale yaliyoanzishwa na JK. Lakini ni huyo huyo JK ambaye baadhi ya wanajamii walidai kuwa zaidi ya kutembea hakuna kipya ndani ya awamu yake ya uongozi!.

JPM na team yako nzima ya utendaji, chapeni kazi, msisikilize miluzi mingi. Haya mnayoyafanya yatakuja kuongelewa awamu ya sita wakati wanaharakati wakijenga hoja za kuuponda uongozi wa wakati huo.

Pigeni kazi, legacy itakuja kuonekana miaka ijayo. Hivyo viwanja vya ndege vitakuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wa miongo ijayo. Hizo bandari zinazoongezwa ukubwa, zitakuwa ni muhimu kwa wafanyabiashara wa miaka mingi ijayo.

Hizo rada nne zinazoweka kimkakati, faida zake ni kubwa sana kiuchumi katika miaka ijayo.

Pigeni kazi msipoteze muelekeo eti kwa sababu watu wanalalamika.

Nawatakia Watanzania wote nane nane njema.
Kazi gani? ya kuteka na kutesa na kupiga risasi?
 
Negative mindsets inakusumbua mkuu, hakuna mema yanayokuja pasipo kujituma na kujitoa kwa dhati. Hizo teuzi na tenguzi hata USA ya Trump inazo tena ni nyingi.
Kipimo cha "dhati" kinaitwaje.

Zamani ukijituma unapata promotion, ukichapa kazi unapata increments, kikundi cha magufuli kimeondoa utaratibu huu!!

Kinaweza kuvizia na kutengua watumishi wa umma kazi zao na kuteua wauaji kama DED wa Itigi.
 
Pole sana mkuu jogi, naona mapovu yanakutoka kwelikweli.

Nadhani ulimsikia mkuu kule Mbeya ni kwanini mshahara umekuwa haupandishwi, nadhani ndugu zako watakuja kuelewa maana ya ujenzi wa mradi wa rufiji.

Miradi ina gharama kubwa lakini itakuwa ndio msingi wa uchumi wenye kuweza kujitegemea.

Ule uchumi wa kuangalia leo mtu ana mapesa mengi mfukoni wakati nchi inategemea uchuzi na mzunguko wa pesa usio na mashiko ya uzalishaji, huwa ni wa muda mfupi tu.
 
Gesi mlisema ndio muarobaini wa nishati ya umeme, leo imekuwa vinginevyo ili m SPEND!!!

Mtakuja mpandishia mshahara mtu akiwa kaburini?
 
Malalamiko ya wapinzani wetu wasio na ubunifu ni kama mzunguko flani hivi usio na mwisho.

Haijalishi nini unafanya, watalalamika tu.

Nadhani wapinzani wetu Tafsiri ya neno upinzani inawapa shida mno.
Chat group lenu kali kweli kweli. Mnashusha nondo za nguvu. Washeni moto ukolee.
 
Malalamiko ya wapinzani wetu wasio na ubunifu ni kama mzunguko flani hivi usio na mwisho.

Haijalishi nini unafanya, watalalamika tu.

Nadhani wapinzani wetu Tafsiri ya neno upinzani inawapa shida mno.
Acheni ujinga, ninyi mikutano ruksa wengine mnawazuia, halafu mna danganya eti maendeleo hayana vyama, SI upuuzi
 
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni mmoja wa marais wenye haiba yenye nguvu sana (charisma).
Ucheshi wake, uwezo wake kiakili na uwezo wa kuweka mizani ya kimahusiano ni sifa yenye kufanana na watu waliozaliwa mwezi wa kumi (libra).

Watanzania walimpachika mzee huyu jina la utani wakimuita Vasco Da Gama, kwa jinsi alivyokuwa akifunga mikanda ya ndege mara kwa mara. JK ni mstaarabu sana, alizodolewa na kukejeliwa, yeye akiishia kutabasamu na kupuuzia.

Leo hii kinaibuka kichekesho eti kwamba haya anayoyafanya JPM ni muendelezo wa yale yaliyoanzishwa na JK. Lakini ni huyo huyo JK ambaye baadhi ya wanajamii walidai kuwa zaidi ya kutembea hakuna kipya ndani ya awamu yake ya uongozi!.

JPM na team yako nzima ya utendaji, chapeni kazi, msisikilize miluzi mingi. Haya mnayoyafanya yatakuja kuongelewa awamu ya sita wakati wanaharakati wakijenga hoja za kuuponda uongozi wa wakati huo.

Pigeni kazi, legacy itakuja kuonekana miaka ijayo. Hivyo viwanja vya ndege vitakuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wa miongo ijayo. Hizo bandari zinazoongezwa ukubwa, zitakuwa ni muhimu kwa wafanyabiashara wa miaka mingi ijayo.

Hizo rada nne zinazoweka kimkakati, faida zake ni kubwa sana kiuchumi katika miaka ijayo.

Pigeni kazi msipoteze muelekeo eti kwa sababu watu wanalalamika.

Nawatakia Watanzania wote nane nane njema.

Umesahau e-mail/namba ya simu!!! hahahaa
 
Tunajitaji afya katika mshikamano na ustawi wa taifa letu.
Kuendeleza mazuri ya kiongozi aliyepita ni jambo jema kabisa...
Nadhani kama lawama zingekuwa kuyatupilia mbali hayo mema ya zamani.

Mtoa post,, TZ tunahitaji kushikamana ili tuwe na nguvu zaidi kukabili changamoto zinazojitokeza kwenye hii target yetu ya uchumi wa viwanda.

Hivyo basi. , Isikuume, usijisikie vibaya unaposikia watu wakisema JPM kaendeleza yale ya JK...
(yaliyo mazuri) . Yatupasa kumpongeza JPM kwa hili,

Lakini ya JK ni yapi na ya JPM ni yapi?
Yote ni kwaajili ya taifa hili TZ.

Mungu awabariki viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom