Rais Magufuli na Serikali yetu punguzeni spidi kidogo tutafakari, kwa maana dah!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Angalau tupeni muda wa kupumua na kutafakari kidogo, kwa maana haya maendeleo mnayotuletea yanatuzidi sasa, hili hatulijalizoea tayari mmeshafunika lile, kabla ATCL hata hatujaizoea tayari TTCL ina take off kwa fujo, karibia tunayachoka maendeleo sasa, duh!

Mnashindwa kuongeza mishahara na kuajiri mmebaki kutafua sifa kwa vitu vya kuonekane machoni.

Wenzenu walijaribu kubalance hawakuta sifa kwa gharama ya masikini wa nchi hii.

Mnanunua ndege kwa cashi, huku mnaongeza makato ya Loan Body karibu mara mbili huku hata mishahara hamuongezi (vipaumbele hovyo kabisa)
 
Kamanda huna namna. Kufa tu. Nchi inazidi kusonga mbele
 
Hakuna uwiano anachokifanya na maendeleo halisi ya Watanzania. Maisha yamekuwa magumu kutokana na kulimbikiza fedha nyingi kwenye ununuzi wa ndege tena kwa Cash kitu ambacho kinatufanya tulipie kwa gharama kubwa kuliko kawaida kutokana na sifa ya kutaka kuacha legacy ndani ya muda mrefu, huku akisahau kuwa walipa kodi hawajaandaliwa mazingira mazuri ya kuendelea kulipa kodi, ajira binafsi na serikalini zimesimama, maendeleo na ustawi binafsi wa mtu mmoja mmoja umekwama. Sekta ya ujenzi na mawasiliano iliyofanya vizuri na kusaidia kukuza uchumi imesimama. Mabadiliko ya makazi vijijin toka nyumba za tope na nyasi mpaka zile za bati zimekwama. Fedha nyingi zinalipwa kwa makampuni ya nje kuliko ndani na hivyo kuondoa mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Ukweli ni hali ni mbaya mijini na vijijini kinachofanyika hivi sasa kwenye kodi na tozo ni kama ambacho wakoloni wa kijerumani walichofanya.
 
Huko Ulaya wanakoandamana hivi vitu hawana?

Endeleeni kupuuza maisha ya watu na mkadhani hitaji la binadamu ni maendeleo ya vitu mtakuja kuona madhara yake!
Watanzania tunaikubali serikSer yetu kwa kazi nzuri inayofanya Na ndiyo sababu hatuandamani
 
Kwa haya DAH,naunga mkono..!yaani yanakuja Dabali dabali....!tunahitaji nafasi ya kutafakari......Mh Magu....embu tupe breki...yaani ndege 7 zinadondoka bongo hii hii...ndege 7 !!. bado hatujapumua...SGR inakimbiza bado tukiwa tunatafakari......daraja la kilombero...bado hatujapumua....interchange ubungo...maendeleo ni ni kujari watu... na watu ndio Sisi tutavuka haya madaraja kifua mbele fursa za biashara,elimu ,afya n.k....kwa kweli tunaomba upinzani wenye tija.. .sio huu wa manung'uniko na ulalamishi muda wote....upinzani dhaifu kuwahi kutokea TZ.
 
Wameambiwa safari za nje ni maalum kwa Dada Samia na Kaka Kassim, yeye na wengine waliobaki ni kazi kwa kwenda mbele.

Waliozoea majungu wanaendelea nayo, wanaoendelea na kazi wanapiga kazi.
 
Hakuna uwiano anachokifanya na maendeleo halisi ya Watanzania. Maisha yamekuwa magumu kutokana na kulimbikiza fedha nyingi kwenye ununuzi wa ndege tena kwa Cash kitu ambacho kinatufanya tulipie kwa gharama kubwa kuliko kawaida kutokana na sifa ya kutaka kuacha legacy ndani ya muda mrefu, huku akisahau kuwa walipa kodi hawajaandaliwa mazingira mazuri ya kuendelea kulipa kodi, ajira binafsi na serikalini zimesimama, maendeleo na ustawi binafsi wa mtu mmoja mmoja umekwama. Sekta ya ujenzi na mawasiliano iliyofanya vizuri na kusaidia kukuza uchumi imesimama. Mabadiliko ya makazi vijijin toka nyumba za tope na nyasi mpaka zile za bati zimekwama. Fedha nyingi zinalipwa kwa makampuni ya nje kuliko ndani na hivyo kuondoa mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Ukweli ni hali ni mbaya mijini na vijijini kinachofanyika hivi sasa kwenye kodi na tozo ni kama ambacho wakoloni wa kijerumani walichofanya.

Hata Ulaya maisha ni magumu!
 
Hivi wewe ulieweka huu uzi upo Sawa sana me naona umelewa na rangi ya kijani kichwani kwako eti tumekinai maendeleo loh! Wakati Kenya ELECTRIC TRAIN imejengwa kitambo tu munafurahia Mali zitakapo enda huko Rwanda
 
Watu waliozoea kutambaa wakiona wamesimama dede wanashangilia! Fikiria kama Mwalimu alisema miaka ya 60 kwamba wakati wenzetu wanatembea sisi tulitakiwa tukimbie sijui sasa tunatakiwa kufanya nini?
 
Back
Top Bottom