Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja - Jicho letu, Star TV

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Wanabodi,

Salaam.
Moja ya vipindi vipindi bora kabisa vya TV vya mazungumzo (TV Talk Show) hapa nchini kwetu Tanzania ni kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorushwa live na Star TV, kila siku za Jumamosi asubuhi, kikiendeshwa na mtangazaji nguli na mahiri Dotto Emmanuel Bulendu (ambaye pia ni mhadhiri mwandamizi wa SAUT), kwa upande wa Mwanza, na mkongwe nguli Angalieni Mpendu kwa upande wa Dar es Salaam kikijikita kwa yanayojiri kwenye tasnia ya Habari kwa wiki nzima ambapo waandishi mbalimbali wa habari hukaribishwa kuchangia.

Kwenye kipindi cha leo, hoja kuu ilitojadiliwa ni jukumu la vyombo vya habari, kama jicho la jamii, kumkosoa rais Magufuli na kuikosoa serikali pale ambapo inafanya makosa kwa lengo la kuisaidia kujirekebisha.

Jee ukosoaji huu ufanyike namna gani?.

Wachangia mada wameshauri media kama media inatakiwa kuwa impartial kwa kutoegemea upande wowote hivyo rais Magufuli na serikali yake, wakifanya mazuri wapongezwe na wakifanya makosa tumkosoe Magufuli na serikali yake kwa hoja na sio kwa viroja au vijembe. Ukosoaji ufanyike with objectivity na kwa lugha ya heshima na staha na sio kwa lugha ya machukizo, maudhi au kutukana, na ukosoaji huo pia ufanyike constructively kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, yaani "contructive criticism".

Mwendeshaji Dotto Bulendu amenigusa sana aliposema huku kwenye mitandao ya kijamii wengi wameegemea upande fulani, wale wa kusifu kazi yao ni kusifu tuu hata madhaifu ya wazi wao watasifu tuu, na wale wa kukosoa kazi yao ni kukosoa na kubeza tuu kila kitu, hata Magufuli afanye mazuri vipi au serikali ifanye mazuri gani wao watabeza tuu.

Sasa wanapojitokeza watu objective na impartial ambao kwenye mazuri watasifu na kwenye mabaya watakosoa, siku wakisifu, wale wakosoaji watawanyooshea vidole kuwa ni upande wa CCM na serikali na siku wakikosoa wale wasifuji tuu watawanyooshea kidole kuwa wao ni wapinzani.

Kiukweli hili alilolisema Dotto Bulendu lipo sana humu jf, kuna watu kazi yao ni kumkosoa tuu na kupinga kila kitu kinachofanywa na Awamu ya Tano, hata kiwe kizuri vipi. Na kuna wengine kazi yao kusifu tuu hata serikali iboronge vipi wao watasifu tuu.

Hali hii impelekea sisi tunaochangia kwa kusifia mazuri na kwenye mabaya tunakosoa huwa tunashutumiwa kwa kunyooshewa vidole kuwa hatueleweki, siku tukisifu tunaitwa CCM, siku tukikosoa tunaitwa wapinzani.

Jee hatuwezi sisi wana jf wote tukawa more objective kwenye kumsifu au kumkosoa Magufuli na serikali yake kwa hoja na sio kwa viroja bila kunyoosheana vidole?.

Paskali
Rejea
Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli
 
Nafikiri wengi hukosoa kwa vijembe baada ya kupigwa vijembe na serikali hiyo hiyo.

Kwa wale wataalamu wa physics wanasema "for every action there is an equal and opposite reaction" wengine huita Tit for Tat :rolleyes:
 
Pascal hakuna cha kukosoa kwa hoja bali haitakiwi mtu yoyote mwenye mtazamo tofauti kutoa maoni yake. Mfano jana David Kafulila alikuwa kipindi cha mada moto channel 10, kwa mshangao wa wengi kipindi kilipoanza tu matangazo yakakatwa!! Katika mazingira hayo ni kwamba hayatakiwi maoni yoyote tofauti. Naangalia kipindi hicho star tv kina huyo jamaa amevaa suti nyeusi anapata tabu kupanga utetezi kwani inabidi ajikite kwenye propaganda zaidi.
 
Hivi mpaka sasa hajaona hoja za wakosoaji wake? basi hakutatokea akajua hoja za wakosoaji vinginevyo aseme anahitaji msaada namna ya kushilikiana na upinzani maana ashauweka pembeni tangu mwanzo aliposema hairuhusiwi mikutano ya kisiasa isipokuwa yeye afanye siasa atakavyo, sasa anakosolewa kila upande anasema zitoke hoja sasa hoja zipi? Au utasikia toeni mawazo mbadala katika kukosoa,

Mimi niseme tuu njia ya kupata mawazo mbadala, ni kuweka mazingira huru ya siasa na kisiasa ikiwa in pamoja na kuweka Uhuru wa mawazo kuanzia bungeni mpaka kwa wananchi wa kawaida kwa hali ilivyo sasa ategemee ukosoaji na zaidi kejeli za hasira ya wananchi na wanasiasa kujiona yeye tuu ndio mwenye mamlaka na mawazo mazuri ya uongozi wakati watu wanaona kuna mengi hayaendi sawia kama nchi yetu tunataka tusonge mbele.
 
Pascal hakuna cha kukosoa kwa hoja bali haitakiwi mtu yoyote mwenye mtazamo tofauti kutoa maoni yake. Mfano jana David Kafulila alikuwa kipindi cha mada moto channel 10, kwa mshangao wa wengi kipindi kilipoanza tu matangazo yakakatwa!! Katika mazingira hayo ni kwamba hayatakiwi maoni yoyote tofauti. Naangalia kipindi hicho star tv kina huyo jamaa amevaa suti nyeusi anapata tabu kupanga utetezi kwani inabidi ajikite kwenye propaganda zaidi.
wenyewe wanakwambia maagizo kutoka juu au kwasababu.zilizo nje ya uwezo wetu.. ukiona hvyo mada sio ya kusifia
 
Angalia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari kinachorishwa live na Star TV, kinashauri tumkosoe Magufuli na serikali yake kwa hoja na sio kwa viroja au vijembe.

Fuatilia

Paskali


Hata mimi naungana na wewe. Watu wengine wanakosoa kwa hoja kama vile wengine wanavyotetea kwa hoja. Ninashukuru wakosoaji wengi wanakosoa kwa hoja, isipokuwa watetezi wengi hawajibu hoja ila wanatetea kwa vioja na hivo kufanya kambi ya utetezi kuwa haina great thinkers ila ina majuha fuata upepo. Mijuha ambayo haiwjuezi kukubali hata kama inaona kabisa imekwama kwenye matope na sasa inaenda kufa (die hards), na hakuna sababu za kufanya hivyo..

Kwa ujumula, ninapingana kwa nguvu zote na watetezi mijuha ambao ni wengi, na wakosoaji vioja ambao ni wachache, huku nikisimama na wakosoaji wa hoja ambao ni wengi na watetezi wa kweli ambao ni wachache.

Magu ameshika nafasi kubwa ya uongozi bial kujali nani alimweka hapo na kama ni kiongozi ama la.. Ninakubaliana na wewe kwamba wakosoaji wakosoe kwa hoja badala ya hidden agenda ambazo hazina maslahi kwa taifa letu. Lakini pia, wateteaji, watetee kwahoja badala ya ujinga ujinga na ushabiki usiojibu changamoto zinazotolewa na wakosoaji wa hoja. Utetevzi wa makelele ya kishabiki kama wanayoyafanya vijana wa ccm hapa mitandaoni, unadhalilisha serikali na kueneza chuki kati ya waathirika na wapiga kelele hao ambao ni ccm wala si serikali.

Ninachokitamani mimi ni serikali kukubali criticisms badala ya kuzizuia kwa nguvu. Kuna constructive criticisms nying i ambazo kama kusingekuwa na vinyongo, ubabe, visasi, kukomoana, kuonyeshana na kuchukiana, bila shaka zingejenga msingi mzuri wa klinasua taifa katika kaburi ambako taifa lilikuwa imelazwa tayari kwa kufukiwa na awamu iliyopita.

Raisi amekuta hazina hakuna fedha, mfumo fisadi umetamalaki kila kona, uozo uliokithiri katika sekta zote, sasa anahitaji mchango wa Watanzanai wote juu ya naman gani tufanye ili kurudisha taifa katika hali salama. Watanzania ni Watanzania na hawategemei vyama vya siasa, dini, kabila wala jinsia. Kuwashirikisha watanzania katika ujenzi wa taifa, chini ya mwongozo na sera sahihi, bila shaka kungejenga ushirikino na uwajibikaji mzuri ambao ungetusogez mbele.

Kama mimi ningelikuwa ni mheshimiwa mkuu, bila shaka nisingefukuzana na wakosoaji kiasi kilipofikia. Badala yake ningejikita kufanya kazi sahihi, ku address hayo ninayokosolewa kwayo, kuboresha ustawi wa taifa na watu wake bila visa, vinyongo wala chuki. Ningewaacha wapige kelele, wafanye mikutano na kampeni vile wanataka. Lakini kwa vile kazi ninayoifanya inaonekana, ninashirikisha Watanzaniana tunafanya wote kukalbili changamoto za wananchi, bila shaka watu wangeona mabadiliko na mwisho wa siku automatically wangepiga kelele lakini miyo yao inawasuta. Wangepiga kelele lakini umma ungeona kelele zile hazina nguvu kwa kuwaa serikali imejikita kwa wananchi na inaboreshamaisha yao.

Wakosoaji, wakosoloewaji, watalwala wote waache kuondesha mambo kwa chuki, visasi, ubaguzi, kukomoana na kuonyehsna ubabe. Dhamira safi zitatushikamanisha na kutupa taifa jama kuliko hila zinazo facilitate hidden agendas. Hazitatusaidia.
 
Leo ukimwangalia kila mtanzania anaonekana kama mkimbizi vile. Leo mtanzania hajisikii fahari kuwa ndani ya nchi yake. Yaani ametokea mtu mmoja tu kujiona kuwa yeye ndiye mwenye hati miliki ya kila kitu Tanzania. Siasa ni zake peke yake, mawazo ni yake peka yake, akili nio zake tu ndio za maana na kila kitu ni yeye tu! Hakuna cha mhimili unaokohoa kwake, mihimili yote imefyata mkia kwa mtu mmoja tu. Viongozi wa kiroho ndio usiseme. Wanatamani kujifisha uvunguni mbele ya bwana huyu. Hii siyo Tanzania tuijuayo. Tanzania tuijuayo ni hii:

1. Watu tuliitana "ndugu', leo tunaitana majipu na mashetani
2. Nchi ilisisitiza siasa safi kama njia ya kuleta maendeleo, leo siasa imekuwa ni uadui. Hakuna anayeruhusiwa kufanya shughuli za kisiasa zaidi ya mtu mmoja tu.
3.Serikali ilibebe jukumu la kuwasomesha watoto wa maskini Chuo Kikuu bure. Leo ni mabomu tu kwa watoto wetu wakipigania haki ya kusomeshwa.
4. Serikali ilijali uhai wa watu wake na ilipotokea vifo visivyoeleweka ilifanya uchunguzi wa kina kama wale wachimba madini wa morogoro. Leo wanaoonekena wamekufa kitatanishi wanaambiwa hao ni wakimbizi
5. Janga la njaa lilipotokea serikali ilifanya kila iwezalo kulisha watu wake. Sote tunakumbuka njaa ya miaka ya sabini na unga wa Yanga. Leo tunaambiwa serikali haina shamba na kila mtu abebe msalaba wake
6. Lilipotokea janga kama lile la tetemeko la Kagera, wananchi walichangishana kila walichonacho kwa usimamizi wa serikali na wahanga kufikishiwa msaada wa kibinadamu. Leo misaada ikichangwa inageuzwa ni fedha ya serikali na inapangia matumizi itakavyo
7. Tuliwasha mwenge ili ulete matumaini pasipo na tumaini na upendo palipo na chuki. Leo tunawasha mwenge na kuukimbiza nchi nzima tukieneza chuki na masimango ya kisiasa. Watu wanatumia majukwaa ya mbio za mwenge kuwazodoa wengine.
8. Shule za serikali zilikuwa ni fahari kwa umma. Mtoto akichaguliwa kwenda shule za serikali ilikuwa ni shangwe kwa familia na ukoo mzima. Leo mzazi hataki kuona mtoto wake akisoma shule za serikali. wanabaki watoto wa wale wasio na namna ya kufanya.
9. Mfanyakazi wa serikali alijisikia fahari kuwa kwenye utumishi wa umma. Leo ni kaa la moto. Hakuna kupanda cheo wala daraja wala kulipwa stahiki za kiutumishi mpaka mtu mmoja tu apende.
10.Mtumishi wa umma akikosea alichukuliwa hatua kulingana na vikao, kanunu, sheria na taratibu za utumishi wa umma. Leo anafukuzwa kazi jukwaani au barabarani. Na kila kiongozi amepewa mamlaka ya kumfukuza kazi mtumishi wa umma.
11. Mtumishi wa umma hata pale ilipoonekana hawezi tena kuendelea na utumishi huo tuliambiwa ki-utu kuwa amestaafishwa kwa manufaa ya umma. Leo tunaambiwa, nimemtumbua au ametumbuliwa, tena ni hadharani bila staha.
12. Kiongozi mkubwa nchini alikuwa ni wa wote na nafasi za uongozi zilikaa kitaifa zaidi. Leo zimekuwa ni za ukanda wa anakotoka huyu kiongozi. Nchi inaelekea kugawanywa kikanda
13. Kiongozi akishinda uchaguzi aliwashukuru watanzania wote kwa kumchagua. Leo tunaambiwa ushindi wake umetokana na kupewa mojawapo ya alama au vyombo vya kiimani vya dini yake .

SOTE KWA PAMOJA TUTAFAKARI TUNAKOELEKEA NA TUNAACHA URITHI GANI KWA KIZAZI KIJACHO. TUKUMBUKE NCHI IMEKUWA KAMA TULIVYOIKUTA KWA SABABU WALIOTANGULIA KUTUONGOZA WALIACHA URITHI FULANI WA KITAIFA. TUSIBOMOE KILA KITU KANA KWAMBA SISI TUNA AKILI ZAIDI YAO. YAKUREKEBISHA YAREKEBISHWE NA YAONEKANE YANAREKEBISHWA KWA NIA NZURI NA SI KUKOMOA AU KUMUUMIZA MTU AU WATU FULANI. TUACHE TABIA YA KUFURAHIA KUUMIZA WENGINE.
 
Back
Top Bottom