Rais Magufuli na Rais Chakwera waweka jiwe la msingi Kituo Kikuu cha mabasi Mbezi, Rais Magufuli ataka Wakandarasi walipe fidia ya kuchelewesha mradi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,514
2,000
Rais Magufuli leo akiwa na mgeni wake, Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera wanaweka jiwe la msingi kituo kikuu cha mabasi ya mikoani inayoendelea kujengwa eneo la Mbezi Louis, Dar es Salaam.
2307EC1A-DD0A-480A-9810-C983A1D8C928.jpeg


7EFD95A4-201E-444D-ABE8-45AB8D530350.jpeg


===
MAGUFULI: Mkataba ulikuwa umalizike mwezi wa saba, leo ni mwezi wa kumi na waziri alikuwa anazungumza hapa wanatakiwa kukabidhi mwezi wa kwanza, this is not fair kwa sababu kuanzi mwezi wa saba mpaka mwezi wa kwanza ni miezi minne.

Palitakiwa watu wanafanya kazi hapa wanaingiza pesa, palitakiwa hiyo deployment ya watu 10 iwe hapa katika kipindi cha miezi minne, hiyo miezi minne nani atakaelipa hizo fedha na kuzifidia na ndio maana nalisema hili, mradi ni mzuri lakini utekelezaji wake ni very poor na hili nalizungumza mbele ya rafiki yangu, mheshimiwa Rais wa Malawi.

Haiwezekani watu watafute visingizio vya Korona, kwanza effect ya korona katika nchi hii ni so minimal kwa hiyo kandarasi alitakiwa awe hapa na mheshimiwa waziri huyu contractor aanze kukatwa pesa za kuchelewa kukabidhi mradi.

Tukienda kwa utaratibu huu, miradi mingi itachelewa na mimi nimeumbwa kusema ukweli kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu na ninazungumza mbele ya baba askofu mstaafu, Dr. Lazarus Chakwera. Haiwezekani, hawa makandarasi Hernan is a good contractor but you have delayed the project, we cant tolerate that stupid thing.

E20AC950-52CA-473A-9253-081F343F717D.jpeg


Ifike mahali viongozi wa Dar es Salaam mlielewe hili, hizi ni fedha za watanzania masikini, wamewekeza hapa ili kusudi wapate faida ya mradi huu kwa hiyo haiwezekani mnasema korona, baadae mtasema mvua, baadae mtasema jua, baadae mtasema matope, haiwezekani.

Kwa hiyo mkurugenzi wa jiji, wewe ndio ulisaini mkataba huu, nataka mradi huu kabla ya mwezi wa 11uwe umemalizika, hakuna extension. Mwezi wa kumi na moja, wafanye kazi usiku na mchana, umeme upo, maji yapo, watu wa kufanya kazi wapo, pesa zipo, hakuna sababu za kusingizia korona, mbona hawajavaa hata barakoa hapa.

Na niwaombe watendaji wangu, huu mradi si mmenileta mimi na mheshimiwa Rais kuja kuweka jiwe la msingi, Hiiiii...... Kwa hiyo waziri huu mradi umalizike, hamieni hapa.

Bilioni 71, naambiwa hapa patakuwa panapakiwa mabasi 1,000 teksi 280 kwa siku, patakuwa na maeneo ya bodaboda na bajaji na patakuwa na eneo la mamalishe na babalishe, hii ni safi kwa sababu mwezi wa saba walitakiwa wawe hapa.

 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
1,354
2,000
Kwa kweli ni kituo kikubwa na cha kisasa kabisa Afrika Mashariki na kati. Ni Lango kuu la kukuza Uchumi wa Tanzania, hongera sana Rais JPM.
 

Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
9,961
2,000
Huwa Majiwe ya Msingi yanawekwa mara mbili? Maana kama ni jiwe la msingi lilishawekwa toka miaka miwili iliyopita, au wanadhani watu wamesahau.

Haya Tusema ni uzinduzi, kama ni uzinduzi mbina bado kituo Hakijaisha kipo kama 80?

Kwanini hawakusema kuwa basi amekaribisha atembelee kujionea ujenzi wa Kituo cha Mabasi.
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,057
2,000
Khaaaaa kituo cha basi tu jamani ni nongwa mpaka ma Raisi wa nje?
Baasi Trump aje atufungulie kile cha morogoro
Hata mimi nilidhani kituo cha bus ni kitu kidogo sana kwa rais wa nchi ya jirani kuja kuweka jiwe la msingi.

Anyway pengine ni u-layman wangu wa kutokujua hizi mambo.
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
36,401
2,000
Huwa Majiwe ya Msingi yanawekwa mara mbili? Maana kama ni jiwe la msingi lilishawekwa toka miaka miwili iliyopita, au wanadhani watu wamesahau.

Haya Tusema ni UZINDUZI, kama ni uzinduzi mbina bado kituo Hakijaisha kipo kama 80?

Kwanini hawakusema kuwa basi amekaribisha atembelee kujionea ujenzi wa Kituo cha Mabasi.
Hata mara tatu, nne si mbaya, inaboresha zaidi mradi kuufanya uwe himilivu.
 

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
4,090
2,000
Nilipita hapo asubuhi maana sio mbali na nyumbani nikaona watu wa CCM wanaingizwa ndani, watu wa usalama. Nk. Hao watu Wa CCM walikuwa wameandaliwa kabisa na ndio walikuwa wa mwanzo kuingia ndani.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
36,517
2,000
Waziri wa Tamisemi amesema stendi ya kimataifa inayojengwa jijini Dsm ikikamilima itabadilisha kabisa muonekano wa jiji.

Jaffo amesema watu wa kutoka mkoa wa Ruvuma na wale wa kanda ya ziwa watakuwa wanakuja katika stendi hii kushangaa na watapotea kabisa hapa mjini.

Source Clouds tv

Maendeleo hayana vyama!
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
10,811
2,000
Haya ya Maendeleo ya Vitu ya CCM Mpya yang mushkeli wangewekeza katika ujenzi wa hospitali nyingine kubwa ingependeza na kuleta Maendeleo ya Watu ktk afya zao bora ili wafanye kazi zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom