Rais Magufuli na PM Majaliwa Wameamua kuwa Wapinzani wa CCM na Kikwete

amilyroley

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
621
1,199
Kinachofanyika sasa sio hakuna mwanaCCM wa Lumumba aliyezoea kula kiyoyozi na kula kwa ubua atakipenda. Sio Sera kabisa za CCM iliyozoeleka, ni Sera za upinzani zilizokuwa zikipingwa na wanaCCM na Kikwete. Lumumba sasa wananongona wanajuta na wengine wanasema walikosea. Anachokifanya magufuli ni kufufua kile na kukipinga kile alichokifanya JK.

Wakwepaji kodi walikuwa marafiki wa serikali iliyopita na marafiki wa CCM. Magufuli na Majaliwa wameamua kuwaadhibu na kuwadhalilisha marafiki wa CCM na serikali iliyopita. Wale matajiri wa kitanzania wenye asili ya Yemen walikokwepa kodi miaka kuki kwa urafiki wa watoto wa vigogo sidhan kama watabaki. Magufuli na Majaliwa hakika wameamua kuipinga CCM na kumpinga JK.
 
Kikwete na CCM watamkumbuka sana Lowassa safari hii.

Usiniache ni mbaya sana, najaribu kufikiri hapo kikwete alipo nini kinaendelea kichwani kwake.
 
Hata Yeye Anajua Aliboronga, Maana Hakuna Nchi Yoyote Inaendeshwa Bila Kukusanya Kodi toka Kwa Wafanya Biashara.

Only Kutegemea Paye as You Earn ya Wafanyakazi.
 
bado unamfikiria lowassa kipindi hiki? kikwete biashara yake imeisha huu ni wakati JPM huyo lowassa aende monduli kuchunga anajidhalilisha tu amekosa mvuto mujini hapa kazi tuuu
 
sikumpa kura yangu lakini kwa anayofanya naomba MUNGU amlinde na kumwongezea ujasiri.AMEN
 
Nimeamua kutubu dhambi yangu ya kutompigia kura Magufuli, nasali na kuomba mara tatu kwa siku kwa siku saba. Naamini baada ya hapo Mungu atanisamehe dhambi yangu
 
Sijutiii na sitokuja kutia maisha yangu, na bado naamini niliyempa kura Yangu ni bora zaidi ya huyu, lowassa ndo jibu LA mambo yote

Mkuu shida ya watanzania ni kupelekwa na kila upepo ndo maana tunadharaulika sana...huyu mh Magufuli hajagusa hata linyangumi limoja, bado anahangaika na vidagaa vilivyotumwa, basi mtanzania amewehuka utadhani halali njaa.
 
Nimeamua kutubu dhambi yangu ya kutompigia kura Magufuli, nasali na kuomba mara tatu kwa siku kwa siku saba. Naamini baada ya hapo Mungu atanisamehe dhambi yangu

Badala ya kutubu kwa kuchagua upinzani ni vema utubu kwa kuliombea Taifa letu lililoridhia Demokrasia ya vyama vingi kwani maamuzi hayo ndiyo haliyokusababishia hiyo dhambi.Waombee wenye mamlaka waufute mfumo wa vyama vingi na uchaguzi mkuu usifanyike tena.Muombe hiyo mungu wako amfanye magufuli rahis wa kudumu wa Wadanganyika.
 
Kikwete na CCM watamkumbuka sana Lowassa safari hii.

Usiniache ni mbaya sana, najaribu kufikiri hapo kikwete alipo nini kinaendelea kichwani kwake.

Kama ana akili; vinginevyo yupo burudani anachekacheka tu!! Takwimu zinaonyesha kwamba Waswahili wa pwani huwa hawapati pressure kwa jambo lolote kwani they are never serious about anything; read anything!!
 
Mnajaribu kumtengenezea matatizo na chama chake kana kwamba watu woote wanaotuhumiwa sahivi walikuwa nyuma ya CCM wakati wa uchaguzi ..hamtafanikiwa kwa hira zenu na uzandiki
 
Mnajaribu kumtengenezea matatizo na chama chake kana kwamba watu woote wanaotuhumiwa sahivi walikuwa nyuma ya CCM wakati wa uchaguzi ..hamtafanikiwa kwa hira zenu na uzandiki, Magufuli levo nyingine.
 
Back
Top Bottom