Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,660
- 1,801
Kwanza niseme, katika muda mchache rais Magufuli amefanya mengi mazuri ambayo kwa Tanzania ni ndoto.
Pia niseme, nina imani na nia njema ya rais Magufuli na kwamba anaitakia Tanzania kheri.
Tatu: ni faraja kubwa kupata rais anayeanza kufikiria kuwa kodi za walalahoi ni haramu kuzifuja, na kwamba haoni ana entitlement ya pesa hizo. Hii ni 'great departure' kutoka hali ilivyokuwa hapo nyuma.
Ila wasi wasi wangu ni kuwa rais huenda anapewa ushauri mbaya juu ya nini Watanzania wanangojea kukiona haraka katika siku 100 zijazo.
Suala la kubomoa sehemu zisizoidhinishwa ni suala muhimu na kubwa. Isipokuwa kama likiendeshwa kama linavyoendeshwa hivi sasa litampotezea rais popularity, ambayo ni muhimu kwa kutekeleza mambo muhimu zaidi. Sioni kwa nini suala hili likaja mwanzo, badala ya suala la kubadilisha fedha, kupiga marufuku matumizi ya dola ya kimarekani katika manunuzi ndani ya nchi n.k. Nadhani ni Clinton aliyesema:" it is the economy, stupid!"
Na kama kuna wajibu wa kubomoa haraka, kwa nini waathirika, hasa masikini, wasipewa mwezi mmoja kuhama? Najua kuna wengine watasema waliishapewa muda mwingi. Huo si ukweli. Serikali iliyopita kwa kweli ilikuwa haifuatilii mambo na ikifuatilia kuna wengi walioruhusiwa kuchomoka kwa sababu mbali mbali. Yumkini tu kuwa watu hawakuamini amri hizo. Halafu madhara gani yangepatikana kwa kuwapa watu muda huo?
Kwa nini siye Waafrika hatuwezi kufanya kitu kwa makini- hata kama ni kizuri?