Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,495
- 51,090
Kama kuna kitu inabidi nimsifu au niwasifu washauri wa kisiasa wa rais Magufuli ni uwezo wake wa kuwatumia mahasimu wake kujipandisha chati kisiasa.
Tekniki mojawapo ambayo rais Magufuli ameonekana kuimaster ni kukuminya kisha akakutumia wewe mwenyewe kumsafisha na athari za kibinyo chake mbele ya umma na Mataifa.
Hebu angalia mbinu hizi
1. Makanisa yanatoa waraka mzito, Serikali inahaha kuuzima inashindikana, waraka unasambaa kama moto wa kiangazi, Serikali inaamua kutumia rungu lake kama dola kudeal. na baadhi ya viongozi wa dini, lakini hili nalo linashindwa kuuzima moto wa waraka.
Kisha Magufuli anakuja na wazo la Kuwaita viongozi wa dini Ikulu. Viongozi wanashindana kuzungumza kwa kumsifu bwana mkubwa, sifa kede kede zinamwagwa LIVE kwenye TV almost Nusu Siku ya kazi.
MATOKEO YAKE NINI?
Rais Magufuli anaibuka kidedea, Walewale waliomwandikia waraka mzito ndo wakawa wa kwanza kumsafisha, kawapa charm offensive ya kukaribishwa Ikulu wakaanza kuona kuwa huyu bwana mkubwa kumbe ni mtu safi!.
Tujiulize, Kuna kilichobadirika baada ya waraka?, Mbona basi miaka miwili baadae Utawala wa Magufuli umeenda kufanya yale yale kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?
2. Mfano wa pili, Wafanyabiashara!
Serikali ya Magufuli, iliharibu sekta binafsi, Kodi zikawa hazieleweki, biashara zikaanza kuyumba, kila kona ya nchi kilio kuwa sekta binafsi inakufa. Alichokifanya bwana mkubwa ni nini?.
Kuwaita Wafanyabiashara Ikulu, kuwapa airtime, wafanyabiashara wakaanza kumsifu mheshimiwa, na kuanza kuitupia lawama TRA. Yaani wafanyabiashara walewale wakamsafisha Magufuli mbele ya umma huku lawama zikienda kwa TRA. Umeuona ugenius wa Magufuli kwenye kucheza na makundi ya kijamii?
3. Issue ya Mo
Serikali ilipata lawama sana jinsi ilivyohandle issue ya Mo, mpaka sasa haijulikani nani almteka Mo. Umma una concensus yake kuhusu hili suala, Sasa namna gani serikali itajisafisha kuhusu Mo?. Ni mheshimiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kiwanda (ambacho sidhani kama kweli kipo) na TV kuonyesha live kuwa kumbe hakuna bifu
4. Issue ya Assad na Trlion 1.5
Assad anaitwa Ikulu mbele ya Camera, anaulizwa makusudi eti serikali imepiga Trilion 1.5, Assad akiwa amewekwa kwenye kona ya kimamlaka anatamka "hakuna kitu kama hicho", Hapo tayari message imeshatumwa kwa skepticals kuwa mheshimiwa yuko Safi ila anazushiwa.
5. Sasa Chadema
Hawa Jamaa wameminywa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, huko mitaani wananchi wanawawekea question mark viongozi waliowekewa kimabavu na serikali ya CCM, migogoro ya kuwakataa hawa viongozi inaanza kuibuka mmoja baada ya mwingine.
Kwa calculations za Serikali ni kwamba inahitajika Meseji au semblance ya Meseji kutoka kwa wapinzani kwenda kwa umma ili kuonyesha kuwa mambo ni shwari, peace tu.
Pia inahitajika kuwatumia wapinzani hawahawa kwenda kwa Wahisani kuwasimanga wahisani waliohoji issue za uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa pamoja na Kuminywa kwa upinzani lakini sisi ni Taifa moja n. k.
CHADEMA wakapewa charm offensive ili watumiwe kwenye propaganda za serikali ya CCM, nao bila kung'amua wakajaa wazimawazima. Na kweli serikali ya CCM imefanikiwa kutuma meseji kwa umma unaolilia kunyang'anywa haki ya kuchagua viongozi wao kuwa kumbe "Wakubwa wanaelewana, hivyo basi mambo yako shwari".
HITIMISHO:
CHADEMA wameuza mechi kwenye suala la kwenda kwenye haya maadhimisho ya mwaka huu. Wameipa serikali ya CCM ushindi mkubwa mno wa kipropaganda wa kuonyesha kuwa mambo yako shwari nchini
CHADEMA wanajidanganya wanapoenda kuomba demokrasia kwa raisi Magufuli. Rais Magufuli anajua anachofanya, na amedhamiria kukifanya na huenda akaendelea kukifanya.
Raisi mwenye uwezo wa kukariri sheria za barabara hashindwi kufahamu ibara za katiba juu ya Demokrasia nchini. Lakini ameamua aliyoyaamua.
Sasa CHADEMA kwa Naivety yao wanadhani wao ndo wana jukumu la kutunza amani zaidi kuliko serikali ya CCM!. Ajabu hii
CHADEMA wataendelea kupewa mkong'oto, hali ikionekana kuharibu taswira ya nchi wataitwa tena LIVE kwenye TV kuwapa Photo Op, watawala, kisha wataendelea kupewa mkong'oto na cycle itajirudia.
Nachukia sana jina Nyumbu na mfano wake, lakini ni Nyumbu ambaye huliwa na Simba, kisha baada ya muda mfupi wenzie waliobaki hujisahau, huamini maisha yatakuwa mazuri na hachukui tahadhari yoyote mpaka pale Simba anaposhambulia tena ndipo hukumbuka kuleta kashkash za hapa na pale kisha hujisahau tena!