Rais Magufuli na mbinu ya Charm offensive: Ujuha wa Chadema

Altenative ya chadema ni ipi? Waliingia vitani wameshindwa, hivyo ni lazima kusalimu amri, hiyo ni kawaida Dunia nzima.
 
Kama kuna kitu inabidi nimsifu au niwasifu washauri wa kisiasa wa rais Magufuli ni uwezo wake wa kuwatumia mahasimu wake kujipandisha chati kisiasa.

Tekniki mojawapo ambayo rais Magufuli ameonekana kuimaster ni kukuminya kisha akakutumia wewe mwenyewe kumsafisha na athari za kibinyo chake mbele ya umma na Mataifa.

Hebu angalia mbinu hizi
1. Makanisa yanatoa waraka mzito, Serikali inahaha kuuzima inashindikana, waraka unasambaa kama moto wa kiangazi, Serikali inaamua kutumia rungu lake kama dola kudeal. na baadhi ya viongozi wa dini, lakini hili nalo linashindwa kuuzima moto wa waraka.

Kisha Magufuli anakuja na wazo la Kuwaita viongozi wa dini Ikulu. Viongozi wanashindana kuzungumza kwa kumsifu bwana mkubwa, sifa kede kede zinamwagwa LIVE kwenye TV almost Nusu Siku ya kazi.

MATOKEO YAKE NINI?
Rais Magufuli anaibuka kidedea, Walewale waliomwandikia waraka mzito ndo wakawa wa kwanza kumsafisha, kawapa charm offensive ya kukaribishwa Ikulu wakaanza kuona kuwa huyu bwana mkubwa kumbe ni mtu safi!.

Tujiulize, Kuna kilichobadirika baada ya waraka?, Mbona basi miaka miwili baadae Utawala wa Magufuli umeenda kufanya yale yale kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

kilichotokea katika waraka ni kuwabana viongozi wa juu wa dini. lakini usifikirie kwamba viongozi wote wa dini wanaunga mkono ufidhuli huo. ni kwamba tu sasa hivi tumetambua kwamba tuna viongozi wa dini ambao ni MANABII WA UWONGO. wanakula kondoo na kujishibisha matumbo yao. hao huwezi kuwaita kuwa ni VIONGOZI WA DINI. haki lazima ishinde, hiyo ni historia.

2. Mfano wa pili, Wafanyabiashara!
Serikali ya Magufuli, iliharibu sekta binafsi, Kodi zikawa hazieleweki, biashara zikaanza kuyumba, kila kona ya nchi kilio kuwa sekta binafsi inakufa. Alichokifanya bwana mkubwa ni nini?.

Kuwaita Wafanyabiashara Ikulu, kuwapa airtime, wafanyabiashara wakaanza kumsifu mheshimiwa, na kuanza kuitupia lawama TRA. Yaani wafanyabiashara walewale wakamsafisha Magufuli mbele ya umma huku lawama zikienda kwa TRA. Umeuona ugenius wa Magufuli kwenye kucheza na makundi ya kijamii?
Hiyo ingemsaidia Magufuli kama kweli angebadili mambo na kuleta nafuu. Tatizo la Magufuli ni kwamba anatumia FAILED POLICIES. Kwa hiyo matatizo yataendelea tu. Pia Magufuli hashughulikii matatizo ya msingi. anapaka mafuta juuu juu tu. na kimsingi hii habari ya kuita watu ikulu siyo ufumbuzi hata kisiasa. ni kupaka mafuta juu ya kidonda lakini hakuna antibiotics wala antigerms lotion. matokeo yake hivi karibuni katika mkutano wa wafanyabiashara, imeonekana matatzo ni yale yale. na ndio maana pamoja na "MAFANIKIO YOOOTE" ya Magufuli, bado anahitaji kutumia FIGISU hata kwenye uchaguzi wa vijiji.

3. Issue ya Mo
Serikali ilipata lawama sana jinsi ilivyohandle issue ya Mo, mpaka sasa haijulikani nani almteka Mo. Umma una concensus yake kuhusu hili suala, Sasa namna gani serikali itajisafisha kuhusu Mo?. Ni mheshimiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kiwanda (ambacho sidhani kama kweli kipo) na TV kuonyesha live kuwa kumbe hakuna bifu

Hili halijaisha, ndio maana Magu ataendelea kuishi kwa figisu

4. Issue ya Assad na Trlion 1.5
Assad anaitwa Ikulu mbele ya Camera, anaulizwa makusudi eti serikali imepiga Trilion 1.5, Assad akiwa amewekwa kwenye kona ya kimamlaka anatamka "hakuna kitu kama hicho", Hapo tayari message imeshatumwa kwa skepticals kuwa mheshimiwa yuko Safi ila anazushiwa.

Wewe ndio ulipigwa chenga. alichojibu Assad ni je, hiyo fedha imeibwa? of course ishu ilikuwa kutojulikana kwa matumizi ya 1.5T, na kilichotakiwa ni kuunda tume ya kuestablish nini hasa kilitokea. Assad hakuiweka hiyo 1.5T katika QUERIES RASMI, inawezekana kuna Queries nyingi alizoweka alilazimishwa kuziondoa au zilipewa majibu ya papo kwa papo. lakini hii hakuweka queries, ndio maana ilihitaji mtu anayejua kusoma hiyo ripoti kugundua kwamba ukijumlisha hapa ukatoa pale, kuna upungufu. Hilo alilithibitisha Prof Assad katika mahojiano na Azam TV. sasa alichoulizwa ni kama kuna wizi wa 1.5 T, of course hiyo aliikana. na kuthibitisha kwamba ngoma ilikuwa bado mbichi sana, rejea ile varangati ya Ndugai vs Assad hasa baada ya Ndugai kurejea kutoka ulaya katika ile news conference. na pia rejea jitihada za serikali kumtoa Assad kwenye u-CAG.

5. Sasa Chadema
Hawa Jamaa wameminywa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, huko mitaani wananchi wanawawekea question mark viongozi waliowekewa kimabavu na serikali ya CCM, migogoro ya kuwakataa hawa viongozi inaanza kuibuka mmoja baada ya mwingine.

Kwa calculations za Serikali ni kwamba inahitajika Meseji au semblance ya Meseji kutoka kwa wapinzani kwenda kwa umma ili kuonyesha kuwa mambo ni shwari, peace tu.

Pia inahitajika kuwatumia wapinzani hawahawa kwenda kwa Wahisani kuwasimanga wahisani waliohoji issue za uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa pamoja na Kuminywa kwa upinzani lakini sisi ni Taifa moja n. k.

CHADEMA wakapewa charm offensive ili watumiwe kwenye propaganda za serikali ya CCM, nao bila kung'amua wakajaa wazimawazima. Na kweli serikali ya CCM imefanikiwa kutuma meseji kwa umma unaolilia kunyang'anywa haki ya kuchagua viongozi wao kuwa kumbe "Wakubwa wanaelewana, hivyo basi mambo yako shwari".
wahisani mnawachukulia hawajui kinachoendelea nchini? wanajua kuliko unavyojua wewe. na mpaka hivi sasa serikali yetu imebanwa sana, lakini bado inajifanya hamnazo. hali ni ngumu na ndio maana imefikia hatua sasa watu wanamwambia Magufuli moja kwa moja tena MUBASHARA kabisa kwamba HALI NI NGUMU.
Kuhusu CHADEMA, hao wamecheza mchezo wa siasa. ni moja ya karata zao. Mbowe was very presidential siku hiyo pale Mwanza. pamoja na mabaya mengi wanayofanyiwa, Mbowe was not an angry person, kama alivyokuwa Mkapa siku anaongea Hard Talk na Tim Sebastian baada ya mauaji kule Pemba. alichofanya Magufuli kwenye uchaguzi wa mitaa na yote anayofanya dhidi ya wapinzani, yanajulikana sana tu. CHADEMA pia wanajua kinachopangwa na Magufuli na genge lake. bila shaka Magufuli naye anaweza kutibua calculations za CHADEMA kama anao uwezo huo. walichofanya CHADEMA ni kumrushia kamba Magufuli ajinyonge mwenyewe. Je, alichowahubiria wakenya kupitia Prof. Kabudi kwenye ile BBI, yeye kwake salama?

HITIMISHO:

CHADEMA wameuza mechi kwenye suala la kwenda kwenye haya maadhimisho ya mwaka huu. Wameipa serikali ya CCM ushindi mkubwa mno wa kipropaganda wa kuonyesha kuwa mambo yako shwari nchini

CHADEMA wanajidanganya wanapoenda kuomba demokrasia kwa raisi Magufuli. Rais Magufuli anajua anachofanya, na amedhamiria kukifanya na huenda akaendelea kukifanya.

Raisi mwenye uwezo wa kukariri sheria za barabara hashindwi kufahamu ibara za katiba juu ya Demokrasia nchini. Lakini ameamua aliyoyaamua.

Sasa CHADEMA kwa Naivety yao wanadhani wao ndo wana jukumu la kutunza amani zaidi kuliko serikali ya CCM!. Ajabu hii
Of course CHADEMA wanaweza kuwabeat CCM, maana CCM wamekuwa watu wa vurugu na figisu. lakini Hakuna hata siku moja CHADEMA wameanzisha vurugu. vurugu zote zinaanzishwa na polisi wa serikali ya CCM. Magufuli hana kawaida ya kuwaita viongozi wa upinzani wanaompinga kikweli kweli, kuhutubia. mara nyingi anawatumia wale wanaoimba mapambio. lakini juzi Magufuli kathubutu kufanya hivyo. hapo ndio kachezea anga za wapinzani. Mbowe aliweza kuongea na taifa moja kwa moja kupitia channel kibao zilizokuwa live, TV na Radio. serikali ya Magufuli imezuia Bunge live ili kuwanyima wapinzani free airtime. hapa Magufuli amemzawadia Mbowe free airtime tena Premium. umeona ujumbe wa wapinzani? a challenge to CCM. wenye akili tu ndio wanaona hayo.

CHADEMA wataendelea kupewa mkong'oto, hali ikionekana kuharibu taswira ya nchi wataitwa tena LIVE kwenye TV kuwapa Photo Op, watawala, kisha wataendelea kupewa mkong'oto na cycle itajirudia.

Kwa kuwazuia wapinzani, hali itaendelea kuwa mbaya pia kwa serikali ya CCM, hasa kwa siasa na mbinu za kiuchumi za Magufuli. mkong'oto kwa Magufuli utatoka kwa wananchi wenyewe

Nachukia sana jina Nyumbu na mfano wake, lakini ni Nyumbu ambaye huliwa na Simba, kisha baada ya muda mfupi wenzie waliobaki hujisahau, huamini maisha yatakuwa mazuri na hachukui tahadhari yoyote mpaka pale Simba anaposhambulia tena ndipo hukumbuka kuleta kashkash za hapa na pale kisha hujisahau tena!
hautapita muda mrefu Magufuli ndio atakuwa Nyumbu. sidhani kama atapata nafasi ya kuungama maovu yake kwenye kitabu kama alivyopata Mkapa
 
Na kujimwambafy kwao kote kule ati "Pombe ni mwepesi kama karatasi". Nilipoona akina Bonny, Sugu, Mnyika na wenzao wakipigana vikumbo nani awe wa kwanza kushika mkono wa Pombe akitoka uwanjani, nikajua kwisha habari yao. Sasa Pombe ni mzito kuliko Tembo😂😂
Aweke Bunduki chini tupambane kwa Hoja, bado haimuondolei sifa ya Uwepesi kama pamba.
 
Altenative ya chadema ni ipi? Waliingia vitani wameshindwa, hivyo ni lazima kusalimu amri, hiyo ni kawaida Dunia nzima.
Chadema imepigana na nani, nani kaua raia kama sio Ccm na viongozi wake, nani anajificha nyuma ya mitutu.....hahahaaaa unachekesha aise.
 
kilichotokea katika waraka ni kuwabana viongozi wa juu wa dini. lakini usifikirie kwamba viongozi wote wa dini wanaunga mkono ufidhuli huo. ni kwamba tu sasa hivi tumetambua kwamba tuna viongozi wa dini ambao ni MANABII WA UWONGO. wanakula kondoo na kujishibisha matumbo yao. hao huwezi kuwaita kuwa ni VIONGOZI WA DINI. haki lazima ishinde, hiyo ni historia.

Hiyo ingemsaidia Magufuli kama kweli angebadili mambo na kuleta nafuu. Tatizo la Magufuli ni kwamba anatumia FAILED POLICIES. Kwa hiyo matatizo yataendelea tu. Pia Magufuli hashughulikii matatizo ya msingi. anapaka mafuta juuu juu tu. na kimsingi hii habari ya kuita watu ikulu siyo ufumbuzi hata kisiasa. ni kupaka mafuta juu ya kidonda lakini hakuna antibiotics wala antigerms lotion. matokeo yake hivi karibuni katika mkutano wa wafanyabiashara, imeonekana matatzo ni yale yale. na ndio maana pamoja na "MAFANIKIO YOOOTE" ya Magufuli, bado anahitaji kutumia FIGISU hata kwenye uchaguzi wa vijiji.

Hili halijaisha, ndio maana Magu ataendelea kuishi kwa figisu

Wewe ndio ulipigwa chenga. alichojibu Assad ni je, hiyo fedha imeibwa? of course ishu ilikuwa kutojulikana kwa matumizi ya 1.5T, na kilichotakiwa ni kuunda tume ya kuestablish nini hasa kilitokea. Assad hakuiweka hiyo 1.5T katika QUERIES RASMI, inawezekana kuna Queries nyingi alizoweka alilazimishwa kuziondoa au zilipewa majibu ya papo kwa papo. lakini hii hakuweka queries, ndio maana ilihitaji mtu anayejua kusoma hiyo ripoti kugundua kwamba ukijumlisha hapa ukatoa pale, kuna upungufu. Hilo alilithibitisha Prof Assad katika mahojiano na Azam TV. sasa alichoulizwa ni kama kuna wizi wa 1.5 T, of course hiyo aliikana. na kuthibitisha kwamba ngoma ilikuwa bado mbichi sana, rejea ile varangati ya Ndugai vs Assad hasa baada ya Ndugai kurejea kutoka ulaya katika ile news conference. na pia rejea jitihada za serikali kumtoa Assad kwenye u-CAG.

wahisani mnawachukulia hawajui kinachoendelea nchini? wanajua kuliko unavyojua wewe. na mpaka hivi sasa serikali yetu imebanwa sana, lakini bado inajifanya hamnazo. hali ni ngumu na ndio maana imefikia hatua sasa watu wanamwambia Magufuli moja kwa moja tena MUBASHARA kabisa kwamba HALI NI NGUMU.
Kuhusu CHADEMA, hao wamecheza mchezo wa siasa. ni moja ya karata zao. Mbowe was very presidential siku hiyo pale Mwanza. pamoja na mabaya mengi wanayofanyiwa, Mbowe was not an angry person, kama alivyokuwa Mkapa siku anaongea Hard Talk na Tim Sebastian baada ya mauaji kule Pemba. alichofanya Magufuli kwenye uchaguzi wa mitaa na yote anayofanya dhidi ya wapinzani, yanajulikana sana tu. CHADEMA pia wanajua kinachopangwa na Magufuli na genge lake. bila shaka Magufuli naye anaweza kutibua calculations za CHADEMA kama anao uwezo huo. walichofanya CHADEMA ni kumrushia kamba Magufuli ajinyonge mwenyewe. Je, alichowahubiria wakenya kupitia Prof. Kabudi kwenye ile BBI, yeye kwake salama?

Of course CHADEMA wanaweza kuwabeat CCM, maana CCM wamekuwa watu wa vurugu na figisu. lakini Hakuna hata siku moja CHADEMA wameanzisha vurugu. vurugu zote zinaanzishwa na polisi wa serikali ya CCM. Magufuli hana kawaida ya kuwaita viongozi wa upinzani wanaompinga kikweli kweli, kuhutubia. mara nyingi anawatumia wale wanaoimba mapambio. lakini juzi Magufuli kathubutu kufanya hivyo. hapo ndio kachezea anga za wapinzani. Mbowe aliweza kuongea na taifa moja kwa moja kupitia channel kibao zilizokuwa live, TV na Radio. serikali ya Magufuli imezuia Bunge live ili kuwanyima wapinzani free airtime. hapa Magufuli amemzawadia Mbowe free airtime tena Premium. umeona ujumbe wa wapinzani? a challenge to CCM. wenye akili tu ndio wanaona hayo.

Kwa kuwazuia wapinzani, hali itaendelea kuwa mbaya pia kwa serikali ya CCM, hasa kwa siasa na mbinu za kiuchumi za Magufuli. mkong'oto kwa Magufuli utatoka kwa wananchi wenyewe

hautapita muda mrefu Magufuli ndio atakuwa Nyumbu. sidhani kama atapata nafasi ya kuungama maovu yake kwenye kitabu kama alivyopata Mkapa
Asante sana kwa ufafanuzi murua wa wiki hii ya Uhuru.
 
CHADEMA wameuza mechi kwenye suala la kwenda kwenye haya maadhimisho ya mwaka huu. Wameipa serikali ya CCM ushindi mkubwa mno wa kipropaganda wa kuonyesha kuwa mambo yako shwari nchini

CHADEMA wanajidanganya wanapoenda kuomba demokrasia kwa raisi Magufuli. Rais Magufuli anajua anachofanya, na amedhamiria kukifanya na huenda akaendelea kukifanya.
Sikujua mnajua kujidanganya kiasi hicho. Tusubiri tuone.
 
hao wenyeviti wa mitaa miwili mliyoachiwa na CCM basi nao watambueni kuwa ni wenyeviti wenu halali na muwape ushirikiano
Siyo mnataka maridhiano huku kwenye ngazi za juu wakati huku ngazi za chini wanachama wenu mnawatenga
 
Pamoja na maelezo yako mazuri sawa na mtazamo wako, lkn hujaonyesha ni njia tunapaswa tupite.

Hapa hivyo Watz wenye akili wote wamepita njia aliyopita Mh Mbowe. Kinyume chake njia yyt mbadala ambayo Mh Mbowe angeamua kuipita na ikaleta madhara, madhara hayo yatawaathiri zaidi wananchi kuliko Mh Mbowe, kuliko Mh Mo, kuliko Mh Rostam, kuliko Mh Manji, lkn kwakuwa wao wana akili waameamua kupita njia hii. Muhimu kuna maisha baada ya siasa. Na muhimu zaidi Ni bora, Na ni raha sana kuwa mjinga mbele ya Mpumbavu

Safi Mkuu,na ukicheza na Mpumbavu atakupaka kinyesi.
 
SIJAONA MATUNDA YA CHADEMA KWENDA PALE KWANZA MANENO AMBAYO MBOWE ALIYAONGEA MKUU HAKUYAPENDA ANGALIA ILE CLIP THEN MSOME BOSS ALIVYOKUWA ANAMSIMILIZA INAONYESHA FIKA HAKUWA AKIYAPENDA YAKE MANENO YA MBOWE NA WALA HATOKUJA KUYAISHI
Ukitoka Gest na mwanamke hata kama mlikua mnazungumzia mkopo umma unajua kishaliwa huyu. Nguvu utakayoitumia kusafisha hali ya hewa ni mara milioni kuliko ungekutwa naye kanisani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu CHADEMA wamecheza karata vizuri sana.
Kitendo cha kuwepo viongozi wakuu wa Chadema kwenye sherehe ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika na Mbowe akatumia nafasi hiyo kueleza matakwa yao mbele ya umati mkubwa ni ushindi kisiasa.
Nahisi kuna mazungumzo ya siri kati ya vyama vikuu vya upinzani na Raisi Magufuli yanaendelea.
Usishangae Mbowe kuteuliwa kwenye baraza la mawaziri la Magufuli kabla ya uchaguzi mkuu.

Acha kujidhalilisha boss, kwa hiyo hapo Mbowe shida yake itakuwa kupigania demokrasia au ni kupata cheo?
 
Ni mada inayo 'stimulate' ubongo. Moja ya mada nzuri kabisa kuijadili kwa kina nyakati hizi.

Mimi nichangie kwa kuuliza:

Hivi mtu akiwa na maradhi mazito, kama 'Kansa' hivi inayosababisha maumivu. Halafu mgonjwa huyo akaenda kwa daktari kupata matibabu.

Pamoja na kutambua vyema ugonjwa, yule daktari kaamua tu kupambana na maumivu yanayomsumbua mgonjwa ili kuyapunguza bila ya kutibu ugonjwa wenyewe. Nilitaka nitumie mfano wa 'panadol', dawa ya kutuliza maumivu, lakini hii ni hafifu sana kwa maumivu yanayotokana na aina ya kansa kadhaa. Kwa hiyo niseme mfano halisi hapa uwe 'morphine' yenyewe, pamoja na matatizo yake, ndiyo anayoiitumia daktari wetu hapa, ambaye ndiye mtawala.

Kwa hiyo mkuu 'Missile' kuhusu mada yako hii, hivi kweli unadhani mgonjwa wetu Tanzania anapata nafuu yoyote?

Huu ndio mchango wangu kwa mada yako hii nzuri sana.

Ngoja niwasome 'Great Thinkers' hapa
 
Kama aina vijana mnaotaka mabádiliko ya kisiasa ni nyie mnaolaum mnaotaka viongoz wajitoe mhanga huku mmefake
jificha tuna kazi kubwa mbeleni. CCM wanajua ndo mnarubuniwa kirahisi ķama ilivyotokea kwa Elia Michael kwa kuwafitinisha na viongoz wenu. Mbowe alitoa ujumbe wenye maneno mengi lakin mmekariri maridhiano tu au mlitaka amtukane JPMkwa lugha ya moja kwa moja?Sio kitu rahisi kama unavyochovya vidole vyako kwenye keyboard.
Kupambana na mtu mwenye jeshi sio jambo jepes ,hivi mmesahau kuwa hata wazee wetu enzi za ukoloni walitumia Alliance ktk kupambana na adui?.Hvyo sion jipya ktk hili lakin pia kosa la Mbowe ni neno maridhiano au kuna njia nyingine bora ameiacha inayoweza kuleta mabádiliko?Au mna
Mimi ninakubaliana na mawazo yako haya.
Matumaini yangu ni kwamba CHADEMA wanayo mikakati, na sio kujisalimisha kwa mtesi wao kama baadhi ya watu wanavyotaka kuwaaminisha wengine.
 
Tatizo la wanaharakati ni kudhani maisha siku zote yanatakiwa yawe ni harakati tu.

Maisha yakionyesha kutaka kuondokana na harakati hao wanaoishi kwa kuzitegemea harakati wanaonekana kuchanganyikiwa.
 
Nachukia sana jina Nyumbu na mfano wake, lakini ni Nyumbu ambaye huliwa na Simba, kisha baada ya muda mfupi wenzie waliobaki hujisahau, huamini maisha yatakuwa mazuri na hachukui tahadhari yoyote mpaka pale Simba anaposhambulia tena ndipo hukumbuka kuleta kashkash za hapa na pale kisha hujisahau tena!
Nilipoandika kule juu, nilikuwa sijafika huku chini ya mada yako.
Ngoja niulize tena swali juu ya hawa wanyama 'Nyumbu'

Bila shaka wale wooote uliowaorodhesha katika mada yako, kama waandika 'waraka' na wengine uliowaweka kama mfano kwenye mada yako, wana'tit' vizuri sana kwenye 'unyumbu' au sio? Na hata waTanzania wote, ni 'nyumbu!

Mimi sikubaliani na dhana hii
 
Missile of the Nation kumbuka hitimisho inatakiwa kuwa fupi na precise ili hadhira iweze kupata ukumbi tarajiwa. Hitimisho lako ni ndefu kulikoni hata main body of the topic. Haifai.
 
Mleta mada hii ni mmojawapo kati ya hawa hapa au mfuasi wao.

1=Zitto kabwe.
2=Bernard membe.
3=January makamba.
4=Fatuma karume.

Orodha inaweza kuwa ndefu sana ila my take ni kwamba mleta mada hii ni mtu au kundi la watu fulani aidha toka ndani ya ccm au upinzani ambao kwao ilikuwa ni furaha kuona magufuli hawapatiwi na au hapewi ushirikiano na vyama vya upinzani nchini.

Hasa wale wana CCM ambao huenda walikuwa au bado wana ndoto za kuhamia upinzani ifikapo uchaguzi mkuu 2020.

Kwao mahusiano mazuri kati ya upinzani na JPM inakuwa changamoto inayoweza kuwanyima fursa.

Wao ndoto yao ya kuingia magogoni ilipozimika, tangu hapo mpaka sasa sumu juu ya utawala wa awamu ya tano imewajaa kama cobra,

Kutwa kucha ni vikao vya siri jinsi ya kuihujumu serikali, kutoka kwenye right track, ili angalau wapate la kusema 2020.

Na hii imewaleta pamoja woote bila kujali itikadi za vyama vyao, hapa ni ITIKADI ZA MATUMBO YAO NA WANUFAIKA WAO TU,NDIO SERA WALIYOWEKA MBELE.

Na kama ni zitto itakuwa ni kwa sababu kitendo Cha yeye kutohudhuria sherehe zile juzi,hasa baada ya sherehe zile kufana, Kinyume na matarajio yake na kundi lake.

Zitto ameonekana kama mwanasiasa mhuni na mamluki, tofauti ambayo inamuweka pabaya kwenye macho ya jamii ya wapiga kura
Hivyo tumeona jinsi alivyohaha mitandaoni yeye na genge lake la ki shariff phobia.

Kuishambulia chadema wakati akijua kile ni chama chenye utawala kama ilivyo huko kwake ACT. na kinafanya maamuzi yake kulingana na utashi wao.

Watanzania tulitaka mabadiliko na tunataka maendeleo na sio mbwembwe za siasa za kimitandao.

Walioumia tunawajua na ndio maana hatukuwaona mwanza wao na wajomba zao.

Message sent
umegusa penyewe mkuu ila zitto id yake moja ameandika jina lake humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom