Rais Magufuli na mbinu ya Charm offensive: Ujuha wa Chadema

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
4,807
Points
2,000

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
4,807 2,000
Kama kuna kitu inabidi nimsifu au niwasifu washauri wa kisiasa wa rais Magufuli ni uwezo wake wa kuwatumia mahasimu wake kujipandisha chati kisiasa.

Tekniki mojawapo ambayo rais Magufuli ameonekana kuimaster ni kukuminya kisha akakutumia wewe mwenyewe kumsafisha na athari za kibinyo chake mbele ya umma na Mataifa.

Hebu angalia mbinu hizi
1. Makanisa yanatoa waraka mzito, Serikali inahaha kuuzima inashindikana, waraka unasambaa kama moto wa kiangazi, Serikali inaamua kutumia rungu lake kama dola kudeal. na baadhi ya viongozi wa dini, lakini hili nalo linashindwa kuuzima moto wa waraka.

Kisha Magufuli anakuja na wazo la Kuwaita viongozi wa dini Ikulu. Viongozi wanashindana kuzungumza kwa kumsifu bwana mkubwa, sifa kede kede zinamwagwa LIVE kwenye TV almost Nusu Siku ya kazi.

MATOKEO YAKE NINI?
Rais Magufuli anaibuka kidedea, Walewale waliomwandikia waraka mzito ndo wakawa wa kwanza kumsafisha, kawapa charm offensive ya kukaribishwa Ikulu wakaanza kuona kuwa huyu bwana mkubwa kumbe ni mtu safi!.

Tujiulize, Kuna kilichobadirika baada ya waraka?, Mbona basi miaka miwili baadae Utawala wa Magufuli umeenda kufanya yale yale kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

2. Mfano wa pili, Wafanyabiashara!
Serikali ya Magufuli, iliharibu sekta binafsi, Kodi zikawa hazieleweki, biashara zikaanza kuyumba, kila kona ya nchi kilio kuwa sekta binafsi inakufa. Alichokifanya bwana mkubwa ni nini?.

Kuwaita Wafanyabiashara Ikulu, kuwapa airtime, wafanyabiashara wakaanza kumsifu mheshimiwa, na kuanza kuitupia lawama TRA. Yaani wafanyabiashara walewale wakamsafisha Magufuli mbele ya umma huku lawama zikienda kwa TRA. Umeuona ugenius wa Magufuli kwenye kucheza na makundi ya kijamii?

3. Issue ya Mo
Serikali ilipata lawama sana jinsi ilivyohandle issue ya Mo, mpaka sasa haijulikani nani almteka Mo. Umma una concensus yake kuhusu hili suala, Sasa namna gani serikali itajisafisha kuhusu Mo?. Ni mheshimiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kiwanda (ambacho sidhani kama kweli kipo) na TV kuonyesha live kuwa kumbe hakuna bifu

4. Issue ya Assad na Trlion 1.5
Assad anaitwa Ikulu mbele ya Camera, anaulizwa makusudi eti serikali imepiga Trilion 1.5, Assad akiwa amewekwa kwenye kona ya kimamlaka anatamka "hakuna kitu kama hicho", Hapo tayari message imeshatumwa kwa skepticals kuwa mheshimiwa yuko Safi ila anazushiwa.

5. Sasa Chadema
Hawa Jamaa wameminywa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, huko mitaani wananchi wanawawekea question mark viongozi waliowekewa kimabavu na serikali ya CCM, migogoro ya kuwakataa hawa viongozi inaanza kuibuka mmoja baada ya mwingine.

Kwa calculations za Serikali ni kwamba inahitajika Meseji au semblance ya Meseji kutoka kwa wapinzani kwenda kwa umma ili kuonyesha kuwa mambo ni shwari, peace tu.

Pia inahitajika kuwatumia wapinzani hawahawa kwenda kwa Wahisani kuwasimanga wahisani waliohoji issue za uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa pamoja na Kuminywa kwa upinzani lakini sisi ni Taifa moja n. k.

CHADEMA wakapewa charm offensive ili watumiwe kwenye propaganda za serikali ya CCM, nao bila kung'amua wakajaa wazimawazima. Na kweli serikali ya CCM imefanikiwa kutuma meseji kwa umma unaolilia kunyang'anywa haki ya kuchagua viongozi wao kuwa kumbe "Wakubwa wanaelewana, hivyo basi mambo yako shwari".

HITIMISHO:

CHADEMA wameuza mechi kwenye suala la kwenda kwenye haya maadhimisho ya mwaka huu. Wameipa serikali ya CCM ushindi mkubwa mno wa kipropaganda wa kuonyesha kuwa mambo yako shwari nchini

CHADEMA wanajidanganya wanapoenda kuomba demokrasia kwa raisi Magufuli. Rais Magufuli anajua anachofanya, na amedhamiria kukifanya na huenda akaendelea kukifanya.

Raisi mwenye uwezo wa kukariri sheria za barabara hashindwi kufahamu ibara za katiba juu ya Demokrasia nchini. Lakini ameamua aliyoyaamua.

Sasa CHADEMA kwa Naivety yao wanadhani wao ndo wana jukumu la kutunza amani zaidi kuliko serikali ya CCM!. Ajabu hii

CHADEMA wataendelea kupewa mkong'oto, hali ikionekana kuharibu taswira ya nchi wataitwa tena LIVE kwenye TV kuwapa Photo Op, watawala, kisha wataendelea kupewa mkong'oto na cycle itajirudia.

Nachukia sana jina Nyumbu na mfano wake, lakini ni Nyumbu ambaye huliwa na Simba, kisha baada ya muda mfupi wenzie waliobaki hujisahau, huamini maisha yatakuwa mazuri na hachukui tahadhari yoyote mpaka pale Simba anaposhambulia tena ndipo hukumbuka kuleta kashkash za hapa na pale kisha hujisahau tena!
 
shungurui

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2008
Messages
3,410
Points
2,000

shungurui

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2008
3,410 2,000
HaKuna mbinu imetumika hapo, zaidi ya maguvu na kutwa kutisha watu kwa mgongo wa tiss, police na jwtz na hicho ndicho kinachompa kiburi, maana vyombo vyote vya usalama vimeacha kufanya maslahi ya nchi badala yake yanafanyq kwa maslahi ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache tu.
 
Mohamed Abubakar

Senior Member
Joined
Jun 26, 2014
Messages
125
Points
250

Mohamed Abubakar

Senior Member
Joined Jun 26, 2014
125 250
Pamoja na maelezo yako mazuri sawa na mtazamo wako, lkn hujaonyesha ni njia tunapaswa tupite.

Hapa hivyo Watz wenye akili wote wamepita njia aliyopita Mh Mbowe. Kinyume chake njia yyt mbadala ambayo Mh Mbowe angeamua kuipita na ikaleta madhara, madhara hayo yatawaathiri zaidi wananchi kuliko Mh Mbowe, kuliko Mh Mo, kuliko Mh Rostam, kuliko Mh Manji, lkn kwakuwa wao wana akili waameamua kupita njia hii. Muhimu kuna maisha baada ya siasa. Na muhimu zaidi Ni bora, Na ni raha sana kujifanya mjinga mbele ya Mjinga
 
dolevaby

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2013
Messages
10,460
Points
2,000

dolevaby

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2013
10,460 2,000
Kwahiyo unataka magu afurahi kwa kuambiwa ukweli
SIJAONA MATUNDA YA CHADEMA KWENDA PALE KWANZA MANENO AMBAYO MBOWE ALIYAONGEA MKUU HAKUYAPENDA ANGALIA ILE CLIP THEN MSOME BOSS ALIVYOKUWA ANAMSIMILIZA INAONYESHA FIKA HAKUWA AKIYAPENDA YAKE MANENO YA MBOWE NA WALA HATOKUJA KUYAISHI
 
jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,142
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,142 2,000
Pamoja na maelezo yako mazuri sawa na mtazamo wako, lkn hujaonyesha ni njia tunapaswa tupite.

Hapa hivyo Watz wenye akili wote wamepita njia aliyopita Mh Mbowe. Kinyume chake njia yyt mbadala ambayo Mh Mbowe angeamua kuipita na ikaleta madhara, madhara hayo yatawaathiri zaidi wananchi kuliko Mh Mbowe, kuliko Mh Mo, kuliko Mh Rostam, kuliko Mh Manji, lkn kwakuwa wao wana akili waameamua kupita njia hii. Muhimu kuna maisha baada ya siasa. Na muhimu zaidi Ni bora, Na ni raha sana kuwa mjinga mbele ya Mpumbavu
Umeandika vizuri sana, kaandika hoja zake nzuri zakufikirika, nikimuuliza ana hakika gani alichokiandika ndicho kitachotokea sijui kama atanipa jibu!, halafu mwisho lazima aweke a way forward, hajaiweka!, sasa kama unaona walichokifanya CDM hakifai, na wewe huna njia mbadala wafanye nini... I think u better shut up!.
 
jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,142
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,142 2,000
Mueneza chuki. Uneongea as if una uhakika wa kiushahidi wa matukio uliyoyasimulia. Watu kama nyie kuna faida mnapata katika watu kugombana. Sherehe ya uhuru sio ya chama. Mkuu Punguza umbeya.
Great thinker wetu huyo muache, naskia ukishagusa tu jf akili inaongezeka!
 
the truecaller

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2019
Messages
457
Points
500

the truecaller

JF-Expert Member
Joined May 8, 2019
457 500
Mleta mada hii ni mmojawapo kati ya hawa hapa au mfuasi wao.

1=Zitto kabwe.
2=Bernard membe.
3=January makamba.
4=Fatuma karume.

Orodha inaweza kuwa ndefu sana ila my take ni kwamba mleta mada hii ni mtu au kundi la watu fulani aidha toka ndani ya ccm au upinzani ambao kwao ilikuwa ni furaha kuona magufuli hawapatiwi na au hapewi ushirikiano na vyama vya upinzani nchini.

Hasa wale wana CCM ambao huenda walikuwa au bado wana ndoto za kuhamia upinzani ifikapo uchaguzi mkuu 2020.

Kwao mahusiano mazuri kati ya upinzani na JPM inakuwa changamoto inayoweza kuwanyima fursa.

Wao ndoto yao ya kuingia magogoni ilipozimika, tangu hapo mpaka sasa sumu juu ya utawala wa awamu ya tano imewajaa kama cobra,

Kutwa kucha ni vikao vya siri jinsi ya kuihujumu serikali, kutoka kwenye right track, ili angalau wapate la kusema 2020.

Na hii imewaleta pamoja woote bila kujali itikadi za vyama vyao, hapa ni ITIKADI ZA MATUMBO YAO NA WANUFAIKA WAO TU,NDIO SERA WALIYOWEKA MBELE.

Na kama ni zitto itakuwa ni kwa sababu kitendo Cha yeye kutohudhuria sherehe zile juzi,hasa baada ya sherehe zile kufana, Kinyume na matarajio yake na kundi lake.

Zitto ameonekana kama mwanasiasa mhuni na mamluki, tofauti ambayo inamuweka pabaya kwenye macho ya jamii ya wapiga kura
Hivyo tumeona jinsi alivyohaha mitandaoni yeye na genge lake la ki shariff phobia.

Kuishambulia chadema wakati akijua kile ni chama chenye utawala kama ilivyo huko kwake ACT. na kinafanya maamuzi yake kulingana na utashi wao.

Watanzania tulitaka mabadiliko na tunataka maendeleo na sio mbwembwe za siasa za kimitandao.

Walioumia tunawajua na ndio maana hatukuwaona mwanza wao na wajomba zao.

Message sent
 
kirumbiu

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2016
Messages
257
Points
250

kirumbiu

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2016
257 250
Kusema kweli pale Chadema walionekana kama vikaragosi fulani, walijishusha hadhi mbele ya uma. Baada ya kitendo kile wengi sasa tumepoteza muelekeo juu yao. CHADEMA mulichokifanya ni kosa la mwaka!
Wewe ulitaka wasiende?hata wangegima kwenda wewe ungekosoa sana hadi matusi kizuri wameenda na ujumbe wameutoa vema sana ila inakuuma ulitaka wasifie utawala huu na hao usidhani wanaenda kichwa kichwa wana washauri ndugu chama chao kiko vizuri usifananishe na TLP ya lyatonga
 
KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Messages
1,874
Points
2,000

KISHADA

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2012
1,874 2,000
Mkuu umejitahidi kuonesha mbinu ovu zinazotumiwa na watawala wetu.

Mimi naliona jicho la tatu. Unaweza kuona CHADEMA kama wamejipelekesha kwenye propaganda za CCM. Upande wa Pili CHADEMA imejiweka mahali pake kisiasa. Kumbuka uongo ulioenezwa na kuaminishwa kwama Kuna VIONGOZI WA uPINZANI si wazalendo na kwamba wanatumiwa na mabeberu. Hilo Limefutwa tayari.

Lengine huu ni mtego kwa JPM. Wenziwe wamejishusha, Umma unamtazama JPM. Yaani Mbowe kamtega JPM. Yakiharibika CHADEMA ilishaonesha uungwana. Hawatolaumiwa .

Ni siasa za kutega na kutegua. Sasa ajenda ni Maridhiano. CDM imefanikiwa kupush ajenda ikijuwa fika JPM hatatekeleza? hilo umeliona kisiasa lina maana gani.

Yaani kumvua Mfalme nguo.
 
mitigator

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
4,078
Points
2,000

mitigator

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
4,078 2,000
Kama kuna kitu inabidi nimsifu au niwasifu washauri wa kisiasa wa rais Magufuli ni uwezo wake wa kuwatumia mahasimu wake kujipandisha chati kisiasa.

Tekniki mojawapo ambayo rais Magufuli ameonekana kuimaster ni kukuminya kisha akakutumia wewe mwenyewe kumsafisha na athari za kibinyo chake mbele ya umma na Mataifa.

Hebu angalia mbinu hizi
1. Makanisa yanatoa waraka mzito, Serikali inahaha kuuzima inashindikana, waraka unasambaa kama moto wa kiangazi, Serikali inaamua kutumia rungu lake kama dola kudeal. na baadhi ya viongozi wa dini, lakini hili nalo linashindwa kuuzima moto wa waraka. Kisha Magufuli anakuja na wazo la Kuwaita viongozi wa dini Ikulu. Viongozi wanashindana kuzungumza kwa kumsifu bwana mkubwa, sifa kede kede zinamwagwa LIVE kwenye TV almost Nusu Siku ya kazi. MATOKEO YAKE NINI?, Rais Magufuli anaibuka kidedea, Walewale waliomwandikia waraka mzito ndo wakawa wa kwanza kumsafisha, kawapa charm offensive ya kukaribishwa Ikulu wakaanza kuona kuwa huyu bwana mkubwa kumbe ni mtu safi!.
Tujiulize, Kuna kilichobadirika baada ya waraka?, Mbona basi miaka miwili baadae Utawala wa Magufuli umeenda kufanya yale yale kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

2. Mfano wa pili, Wafanyabiashara!
Serikali ya Magufuli, iliharibu sekta binafsi, Kodi zikawa hazieleweki, biashara zikaanza kuyumba, kila kona ya nchi kilio kuwa sekta binafsi inakufa. Alichokifanya bwana mkubwa ni nini?. Kuwaita Wafanyabiashara Ikulu, kuwapa airtime, wafanyabiashara wakaanza kumsifu mheshimiwa, na kuanza kuitupia lawama TRA. Yaani wafanyabiashara walewale wakamsafisha Magufuli mbele ya umma huku lawama zikienda kwa TRA. Umeuona ugenius wa Magufuli kwenye kucheza na makundi ya kijamii?

3. Issue ya Mo
Serikali ilipata lawama sana jinsi ilivyohandle issue ya Mo, mpaka sasa haijulikani nani almteka Mo. Umma una concensus yake kuhusu hili suala, Sasa namna gani serikali itajisafisha kuhusu Mo?. Ni mheshimiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kiwanda (ambacho sidhani kama kweli kipo) na TV kuonyesha live kuwa kumbe hakuna bifu

4. Issue ya Assad na Trlion 1.5
Assad anaitwa Ikulu mbele ya Camera, anaulizwa makusudi eti serikali imepiga Trilion 1.5, Assad akiwa amewekwa kwenye kona ya kimamlaka anatamka "hakuna kitu kama hicho", Hapo tayari message imeshatumwa kwa skepticals kuwa mheshimiwa yuko Safi ila anazushiwa.

5. Sasa Chadema
Hawa Jamaa wameminywa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, huko mitaani wananchi wanawawekea question mark viongozi waliowekewa kimabavu na serikali ya CCM, migogoro ya kuwakataa hawa viongozi inaanza kuibuka mmoja baada ya mwingine. Kwa calculations za Serikali ni kwamba inahitajika Meseji au semblance ya Meseji kutoka kwa wapinzani kwenda kwa umma ili kuonyesha kuwa mambo ni shwari, peace tu. Pia inahitajika kuwatumia wapinzani hawahawa kwenda kwa Wahisani kuwasimanga wahisani waliohoji issue za uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa pamoja na Kuminywa kwa upinzani lakini sisi ni Taifa moja n. k.
CHADEMA wakapewa charm offensive ili watumiwe kwenye propaganda za serikali ya CCM, nao bila kung'amua wakajaa wazimawazima. Na kweli serikali ya CCM imefanikiwa kutuma meseji kwa umma unaolilia kunyang'anywa haki ya kuchagua viongozi wao kuwa kumbe "Wakubwa wanaelewana, hivyo basi mambo yako shwari".

HITIMISHO:

CHADEMA wameuza mechi kwenye suala la kwenda kwenye haya maadhimisho ya mwaka huu. Wameipa serikali ya CCM ushindi mkubwa mno wa kipropaganda wa kuonyesha kuwa mambo yako shwari nchini

CHADEMA wanajidanganya wanapoenda kuomba demokrasia kwa raisi Magufuli. Rais Magufuli anajua anachofanya, na amedhamiria kukifanya na huenda akaendelea kukifanya.
Raisi mwenye uwezo wa kukariri sheria za barabara hashindwi kufahamu ibara za katiba juu ya Demokrasia nchini. Lakini ameamua aliyoyaamua.
Sasa CHADEMA kwa Naivety yao wanadhani wao ndo wana jukumu la kutunza amani zaidi kuliko serikali ya CCM!. Ajabu hii

CHADEMA wataendelea kupewa mkong'oto, hali ikionekana kuharibu taswira ya nchi wataitwa tena LIVE kwenye TV kuwapa Photo Op, watawala, kisha wataendelea kupewa mkong'oto na cycle itajirudia.

Nachukia sana jina Nyumbu na mfano wake, lakini ni Nyumbu ambaye huliwa na Simba, kisha baada ya muda mfupi wenzie waliobaki hujisahau, huamini maisha yatakuwa mazuri na hachukui tahadhari yoyote mpaka pale Simba anaposhambulia tena ndipo hukumbuka kuleta kashkash za hapa na pale kisha hujisahau tena!
Kama aina vijana mnaotaka mabádiliko ya kisiasa ni nyie mnaolaum mnaotaka viongoz wajitoe mhanga huku mmefake
jificha tuna kazi kubwa mbeleni. CCM wanajua ndo mnarubuniwa kirahisi ķama ilivyotokea kwa Elia Michael kwa kuwafitinisha na viongoz wenu. Mbowe alitoa ujumbe wenye maneno mengi lakin mmekariri maridhiano tu au mlitaka amtukane JPMkwa lugha ya moja kwa moja?Sio kitu rahisi kama unavyochovya vidole vyako kwenye keyboard.
Kupambana na mtu mwenye jeshi sio jambo jepes ,hivi mmesahau kuwa hata wazee wetu enzi za ukoloni walitumia Alliance ktk kupambana na adui?.Hvyo sion jipya ktk hili lakin pia kosa la Mbowe ni neno maridhiano au kuna njia nyingine bora ameiacha inayoweza kuleta mabádiliko?Au mna
 
Forum statistics

Threads 1,382,758
Members 526,462
Posts 33,836,803
Top