Say no to actors
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 637
- 640
Wadau ni matunaini yangu kuwa wazima wa buheri.
Leo napenda nidadavue juu ya majibu ya mkuu wetu wa nchi siku amekutana Na wahariri wa vyombo vya habari. Rais aliulizwa suala la katiba mpya lakini yeye majibu aliyotoa hayakuwa yenye uhalisia na wataalam wanasema yalikuwa ya uongo.
Kwanza nikili kuwa suala la katiba mpya liko kwenye ilani ya chama cha Mapinduzi, angalia ilani ya chama cha mapinduzi page 164 kipengele cha 145(g) inasema "Kukamilisha mchakato wa kutunga Katiba Mpya na kuanza kuitekeleza kwa mjibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba".
Pia hili suala la kukamilisha mchakato cha katiba na kuanza kuitumia ndani ya 2015/2020 ni mojawapo ya maazimio ya mkutano mkuu wa CCM na ambayo yamewekwa pia kwenye ilani yao ya uchaguzi page 185 kipengele cha 183a kudumisha muungano ambapo CCM inaamini ndani ya katiba hii inayopendekezwa kero nyingi za muungano zimepatiwa majawabu ya kuridhisha.
Na ninakumbuka kipindi huyu ndugu amepitishwa na mkutano mkuu wa chama kama mgombea urais aliulizwa na waandishi wa habari juu ya kipaumbele chake na alisema ni ILANI YA CCM ya uchaguzi lakini leo hii anaisimanga na kusema si kipaumbele.
Na jambo la kushangaza chama nacho kimeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa serikali. Kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi pg 188 Jukumu la CCM kipengele 187 "chama kina jukumu la kufuatilia utekelezaji wa ilani hii".
Chama leo kinacheza ngoma ya Rais Magufuli akisema leo hakuna kuvaa nguo za chama wote wananywea na hakuna wa kukohoa. Hakuna hata press conference ya CCM ya kujitokeza na kurekebisha kauli ya mtu wako. Au kumuita na kumwambia hapa unaenda kinyume na ilani.
Watanzania walidanganywa kupindi cha campaign kuwa mtuchague tutakamirisha katiba mpya nao wakawapatia kura na leo wanaambiwa ngoja kwanza tuwanyooshe ilani baadaye, na wao wasijiulize
- Je, tulikuwa tumepinda?
- Je kama tulikuwa tumepinda?
- Je, ukitunyoosha hatutovunjika?
NI GARI BOVU NA DREVA MLEVI HUKU KONDAKTA NI TEJA, Safari si salama.
Nawasilisha.