Rais Magufuli na CCM mpya kwa Tanzania imara: Falsafa inayojenga mtazamo chanya kwa watanzania juu ya CCM

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,590
4,600
Tukiwa tumeuanza mwaka 2020, mwaka wenye tukio muhimu la uchaguzi mkuu , uchaguzi unaotazamiwa na wengi kuwa ndio uchaguzi utakaoanzisha mwanzo wa mwisho wa siasa za upinzani hasa wa vyama vya uchaguzi kama Katibu Mkuu wa CCM ndg.Dkt. Bashiru anavyopenda kuviita na muendelezo wa falsafa wa CCM mpya kwa Tanzania imara

CCM mpya kwa mtazamo wa walio wengi haina sababu ya kushindwa uchaguzi wowote kwa sababu nia na uwezo wa kushinda inayo. Kipindi cha utawala wa Rais Magufuli umedhihirisha kuwa kiongozi huyu ana nia ya dhati ya kuijenga CCM mpya kwa Tanzania imara. Ni Imani yangu, CCM mpya itakuwa nuru kwa Tanzania imara kwa vizazi vingi sana vijavyo.

Uchaguzi mkuu unaenda kufanyika watanzania wakiwa na kumbukumbu sahihi ya kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2019, uchaguzi ulioipa CCM ushindi wa kishindo, uchaguzi ule ulitoa mwanga wa kukubalika kwa falsafa ya CCM mpya. Kipimo cha kukubalika kwa chama cha siasa ni kampeni na uchaguzi hivyo falsafa ya CCM mpya imekubalika kwa watanzania.

Tofauti na miaka ya nyuma hasa juu ya mtazamo wa vijana kwenye siasa za vyama , kipindi hiki vijana wameonekana kuikubali na kuheshimu falsafa ya CCM mpya na kufanya kuungwa mkono na vijana wengi hata wa vyama vya upinzani. Vijana ni jeshi kubwa na vijana wote wanakubaliana na CCM mpya kwa Tanzania imara.

Katika kipindi hiki cha awamu ya tano, watanzania wameona umuhimu wa CCM ambao pengine ulianza kubezwa na vyama vya upinzani, katika awamu hii imeonekana Tanzania inahiitaji CCM kwa maendeleo yake kuliko chama kingine chochote. CCM ni hitaji la Tanzania la wakati wote huku Rais Magufuli akiwa ni hitaji la Tanzania la wakati huu.

Upinzani ina wakati mgumu sana, wakati huu ambapo Tanzania inahiitaji CCM na inamuhitaji Rais Magufuli kuliko yeyote yule, huu ni wakati ambao kila mtanzania anaona matumizi sahihi ya kodi, huu ni wakati ambao uwajibikaji umeongezeka, huu ni wakati ambao nidhamu imerejea , huu ni wakati ambao pato la taifa linaongezeka na uchumi unakua kwa kasi. Huu ni wakati wa CCM mpya na Rais Magufuli kuijenga Tanzania imara.
 
Kwaheri mama Kabendera...upumzike Salama...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom