Rais Magufuli: Mwaka huu tutaboresha maslahi ya Wafanyakazi nchini.

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli amesema baada ya kusafisha wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki sasa serikali yake itaanza kuajiri watumishi zaidi ya 52000, itapandisha madaraja, kuruhusu uhamisho, aidha amesisitiza Wakurugenzi na makatibu wakuu na makatibu tawala kutohamisha watumishi kabla ya kuwalipa watumishi fedha za uhamisho, vilevile Mh Rais amesema serikali itawapandishia mishahara watumishi na stahili nyingine.

TBC
 
Mwaka jana aliahidi kupunguza Kodi.
Kumbe ilikua kundi la wachache.
Mwaka jana alisema tuwape miez miwili tu then mambo yangekaa sawa ukapita mwaka.
Je kisheria watumishi hatuna haki ya kulipwa nyongeza tulostahili 2016?
 
Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli amesema baada ya kusafisha wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki sasa serikali yake itaanza kuajiri watumishi zaidi ya 52000, itapandisha madaraja, kuruhusu uhamisho, aidha amesisitiza Wakurugenzi na makatibu wakuu na makatibu tawala kutohamisha watumishi kabla ya kuwalipa watumishi fedha za uhamisho, vilevile Mh Rais amesema serikali itawapandishia mishahara watumishi na stahili nyingine.

TBC
Pia watumishi wasikubali kuhama,hadi walipwe! Hii nimeipenda!
 
Kama sijasahau kipindi cha kutafuta kura kutimia alituahidi serikali yake haitakuwa na mambo ya tuko kwenye mchakato tumefikia pazuri, sasa najiuliza hizi kauli zinazoanza na neno tutafanya hivi au vile zina utofauti na tuko kwenye mchakato? Time will tell.
 
Hajasema atspandisha mishahara! Kupandisha mishahara ni kupandisha kima cha chini cha mshahara!
Atakachofanya ni kutoa nyongeza ya kawaida ya mwaka ambayo huwa hawapati wafanyakazi wote! Walio kwenye Bar za ngazi zao hawapati kitu!
Amesema atapandisha vyeo, hii pia si kwa wote!
Kwa ujumla tunaendelea kuisoma namba!
 
Kuboresha mishahara ni pamoja na kuruhusu mabenki kukopesha wafanyakazi pesa sinazoweza angalau kujenga nyumba au kuanzisha miradi kwa riba nafuu. Kila mtu anatamani kupata maisha bora lakini kwa sasa mabenki ni kama yanawanyonya wafanyakazi kwa riba kubwa na makato mengi kwenye miamala ya kibenki.

Naona kila dalili ya mh. Kuwa na nia ya Kuwakomboa wafanyanyakazi.
Kuna wakati hua najiuliza hivi tanzania tuna bunge hili la CCM la kazi gani ! !? Mana sijaona kama kuna siku limewahi kumtetea mfanya kazi kwa kuibada serikali kwa nguvu zote bila badala yake limekua liitetea serikali kwa nguvu zote.
Natamani siku moja niwaone wabunge wate wa chama kikongwe wanapigwa chini ili nao wakae benchi wajue ugumu wa maisha. Kuna wabunge wengi kuanzia babu alikua waziri na mbunge mpaka leo na wajukuu ni wabunge . Hawa hawajui maisha ya mtanzania zaidi ya kuyasoma na kuyasikiliza kwenye vyombo vya habari.

Yani kwa miaka na miaka wafanyakazi wamekua wakionewa na mabosi wao kwa kuhamishwa hovyo hovyo na kudhulumiwa haki zao za malipo ya uhamisho huku serikali ikiingia gharama za madeni kwa mara nyingine uhamusho usiokua na tija yoyote kwa taifa zaidi ya chuki tu au rushwa ,lakini wabunge wakashindwa kuiagiza na kuitungia serikali sheria kali ya kuwabana hao mabosi marasimu yanayolitia taifa hasara kwa mambo ya kijinga.
Mpaka Mh. Rais alipoliona na kuamua kuwatetea wafanyakazi wanyonge wanaohamushwa hamishwa bila kulipwa hela zao za uhamisho huku malipo yao yakiwa ni madago. Mtu anadai milioni moja kwa miaka kumi wakati amehamishwa na kuingia hasara kubwa bila sababu ya msingi tena kwa uhamisho ambao hakuuomba.
Kuna idara zimekithiri kwa kuwahamisha hamisha wafanyakazi wake bila sababu za msingi.
Wabunge walikaa kimya bila kufikirisha akili zao huku taifa likipata hasara kwa hamisha hamisha ya kijinga kabisa iliyokua inafanywa na wakuu wa idara. Mtu anaomba uhamisho wa bila malipo tena akiwa na sababu za msingi kabisa ananyimwa lakini muda huo huo anahamishwa mtu mwingine ambaye hakuomba uhamisho. Matokeo yake serikali inapewa deni lisilo na sababu kwani ni wazi kuwa mauhamisho mengi yamegubikwa na majungu ,chuki, visasi na kutaka kufanya ufisadi kwa kutafuna pesa za watu kwa kigezo cha fungu la uhamisho.
Hakuna mtu aliyeliona na kutolea kauli yenye kuwatisha wakuu wa idara zilizokuwa zinafanya hujuma kwa watumishi walioko chini yao kwa kuhamisha hamisha hovyo mpaka mh. Rais aliposema mtu atakayehamishwa bila malipo asiende. Hii inadhihirisha wazi kuwa kwa sasa Tanzania imepata Rais anayetambua na kujua shida walizokuwa wanapewa kwa makusudi watu wa chini.
Mtu ana kamshahara kadogo na alikua anakaa na mkwe wake na watoto na alikua ameshajenga kibanda chake na kuishi na familia yake na kufuga vimbuzi vyake ghafla unamhamisha , huko anakokwenda anaenda kupanga nyumba na kuanza kuwa na maisha ya familia mbili na sio kwamba labda umempandisha cheo chochote cha kiutawala na wakati huo huo hutaki kumlipa bali unazidi kuilimbikizia madeni serikali kwa sababu ya kujiona kuwa wewe ndio mpangaji na hakuna wa kukuuliza. Kwa kweli huu ulikua ni uonevu mkubwa ambao watumishi wa umma walikua wanafanyiwa huku wakikosa watetezi.

Nadhani bado kuna haja ya mheshimiwa rais kuendelea kutumbua majipu kwani kuna watu kwa muda mrefu walikua wamelisababishia taifa hili hasara bila sababu huku wabunge na mawaziri wakikaa kimya bila kumwajibisha mtu yeyote.

Kuna wakuu wengine wa idara anaamua tu kumhamisha mtu kisa alipofanya ziara ya kiofisi hakumpa bahasha yenye fedha na kumnunuli mazawadi kibao vikiwemo vyakula wakati hana pesa za kugharamikia wageni. Ubinafsi wa mtu unaipa serikali hasara.

Nangemuomba mh. Rais ikiwezekana kiundwe kitengo maalumu cha kusimamia na kusikiliza malalamiko ya watumishi wanaoonewa huko makazini na kipewe meno ya kusikiliza na kuchunguza na hatimaye kutoa adhabu kali kwa mkuu wa idara atakayekuwa ametumia mamlaka yake kumwonea mtumishi wa umma hasa wa ngazi za chini. Watu wanagombea mabaa medi halafu hasira zao wanaenda kuzionyesha huko ofisini kwa mwenye cheo kumkomoa wa chini yake waliyegombea mambo ya mapenzi kwa kumhamisha kituo chake cha kazi. Mwishowe serikali ndiyo inapata hasara kuingia kwenye madeni.
Mambo kama haya yakigundulika basi hatua kali zinapaswa zichukuliwe kwa muhusika.

Tunataka Tanzania mpya.
 
Back
Top Bottom