Rais Magufuli mulika Hospitali ya Mkoa wa Lindi ina madudu ya kutisha

Masquarrader

Member
Aug 17, 2018
62
38
Rais Magufuli Mimi kama Mtanzania nachukua jukumu hili kukufahamisha kuwa hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine Ina watendaji/ viongoz wabovu kuwahi kutokea katika historia ya sekta ya afya mkoani Lindi.

Kwanza Kuna malalamiko kutoka karibu katika kila kada ya wahudumu wa hospitalini hapo ambapo baadhi ni Kama yafuatayo:

Wafanyakaz wengi hasa wahudumu wa afya, wauguzi ngazi mbali mbali Kama EN na RN, wataalam wa maabara n.k wahapewi haki zao mbalimbali kama za posho za ziada ya kazi, watu hawajapandishwa vyeo Zaid ya miaka 7, wengine wamejiendeleza kitaaluma kutoka wahudumu wa afya mpaka kufikia kuwa ENROLLED NUSE na REGISTERED NURSE tangu mwaka 2015 lakin hawajafanyiwa mabadiliko ya kimuundo wala vyeo wala kubadirishiwa mishahara yao.

Aidha mganga mkuu wa mkoa hataki kusikiliza mfanyakaz shida zake na hata wengine wakienda kwa mkuu wa mkoa kutoa malalamiko wanaishia kusemwa kwa mganga mkuu na mwisho mfanyakaz huyo atakomolewa kwa kila namna. Ipo mifano mingi ya walioenda kuonana na RC lakini wakaambulia kufululiza zamu za usiku Hali inayoonesha RC na RMO ni Pete na kidole.

Kutokana na Hali hiyo, kila mfanyakaz anaogopa kuongea kwa hofu ya kuadhibiwa, na wengine Wanaoanga kwenda ofisi za usalama wa taifa kutoa malalamiko yao wanaishia kuogopa isije yakarudi Kama yalivyo kwa RMO maana hawajui wapi kupo salama kupeleka malalamiko yao

Kifupi hawana ari ya kaz hasa kada nilizotaja na kwa upande wa madaktari ni wale wanaoonekana kuwa na kelele na ujasiri huwa wanaitwa na RMO na kupozwa basi mengine yanaendelea. Wabapozwa kwa kufaham kuwa Wana uelewa wa wapi wakaseme hivyo jwa vile wanaweza kuleta udhia wanapenyezewa Rupia.

Ndugu Rais kitu cha ajabu ambacho wafanyakaz Hawa wanashangaa tangu Serikali yako iingie madarakani mwaka 2015, hakuna kiongoz wa kitaifa aliyeingia pale na kusikiliza changamoto za kiutendaji wala miundombinu, wewe binafsi mwaka 2019 uliahid kwenda huku ratiba yako ikionyesha ungefika kanisan RC Mtanda ukasali yakafanyika maandaliz yote ukaondoka juu kwa juu, waziri mkuu ambae ndio kwao hajawahi hata siku moja kukanyaga maeneo ya hospitali hiyo, aliyekuwa waziri wa afya UMMY MWALIMU alijaribu kuingia kwa kupitia mlango wa nyuma akafanikiwa lakini hakufikisha dakika kumi akaondoka bila kuongea na wafanyakazi.

Ndugu Rais wapo wanaoamin uongozi wa hospitali hiyo ni washirikina Sana kiasi hawako tayari kuona viongoz mnafika pale na kuhoji MADUDU yanayoendelea Kwan RMO yuko bize kujenga maghorofa yake mtaa wa Mtanda huko juu.

Hadi inaaminika hospitali hapo miongoni nwa wafanyakaz kuwa huenda WAKUBWA wote hamtafika hapo tofauti na RC mwenye ukaribu na RMO (Waarabu wa Pemba) na kwamba hata ule moshi uliletewa ukiwa njian kutoka ruangwa unaelekea Lindi 2019 inaaminika ulitoka kwa viongoz wa hapo Sokoine kwa kushirikiana na RC Zambi anayesadiki vitendo vya dhambi Kama matamshi ya jina lake ( huyu mchunguze vizuri ana mambo mengi hata kwenye vyama vya ushirika wanamtaja Sana).

Ndugu Rais, pole kwa kukuchosha lakin najua unavyanzo vingi kuliko mm, fatlia haki za kiutumishi na kimaslah za wafanyakaz wa hospitali hii yenye miungu watu Kwan wanaogopa hata kuja kwako wakihofia pengine badala ya kupata haki wanaishia kufukuzwa kutokana na wanavyofananisha msululu wa matukio.

Baadhi ya majina ya watumishi ninayo na nyaraka zao walizolalamika kwa viongoz mbalimbali imeshindikana hadi wengine kushauriwa wakalalamike Usalama wa taifa na kukosa ujasiri wa kufanya hivyo. Ukihitaji hayo hata kwa mguu nitakuletea Chamwino unaunguza Sana watu wanavyoteseka.

Fikiria mtu amebadilishiwa muundo 2015 hakuna mabadiliko hata ya mshahara maana yake haki yake ya kupanda cheo 2018 ameikosa na mwakani Anaweza asipande tena na akifa anapata mapato ya mshahara wa sasa wa laki 6 wakati alitakiwa awe kuanzia milioni moja na laki 4 huko, mbona yule nesi mrembo wamesoma nae wote yeye alishabadirishiwa vizur na anaish safi au tuwaalike akina Mbugo wa PCCB? hata wakialikwa Nani wa kutolea maamuz ya wafanyakaz Hawa.

Ndugu Rais tunakupenda Sana hasa kwa style yako ya kujali wanyonge na kujitoa kisafisha uozo Serikalin na bado tunaiman kubwa na wewe. Allah akujaalie kheri, afya ukakamavu wa kumshinda shetani aliyetawala SOKOINE HOSPITAL Lindi ili kuepusha madhara kwa wanaofuata huduma za afya hospitalini hapo
 
Ukiona mtu anaandika uzi JF kulala mikia uongozi hasa ndani ya Utumishi wa Umma huyu sio wa kupuuza..Naamini Rais wetu msikivu kakusikia na litafanyiwa kazi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Inaonekana wewe una chuki binafsi na RMO ... hayo uliyoyasema mengi RMO hawezi kuyatatua bali ni wizara ya utumishi. Pia siyo kweli kuwa Hosp hiyo haijatembelewa na Viongozi wa kitaifa muda mrefu .. Mwaka huu 2020 baada ya July Mganga Mkuu wa Serikali prof Makuabi alifika hapo na kuongea na sisi watumishi na kutatua baadhi ya Changamoto ikiwa na pamoja na maswala ya ujenzi , huduma na watumishi wanaosomeshwa na Serikali .

Tatizo hapa kuna wauguzi wamekaa muda mrefu sana na kuwa miungu na hawataki kuguswa na wananchi haki hata huyo RMO kwa kupewa kiburi toka sehemu za juu.
 
Huyu unayemuambia hana uhalali wa kusimamia haki kabisa, labda atumie maguvu tu kama anavyofanya kutisha watu.
 
Haya madudu ya kiutumishi yapo sehemu nyingi sana hasa sekta ya afya watumishi wanamalalamiko kibao na viongozi wao hawawatetei kabisa, uenda kwa kuogopa au kujinufaisha kupitia mgogoro huo wa kiutumishi
 
SERIKALI ZA KIDIKTETA HAZIJAWAHI KUMSIKILIZA MTU WA HALI YA CHINI tafuta vitabu vya madikteta wote,rejea kidogo hapa tarehe 24:10:2020 mitandao yote ilizimwa hadi leo mara inazimwa mara inawashwa,lakini pia watumishi mlipewa laki tatu ili kubadili matokeo !!!
 
Nakubaliana na wewe juu ya uozo uliopo hospitali ya Sokoine Lindi shida ipo tena sana,watumishi baadhi hawatendewi wema katika kutekeleza majukumu yao lakini pia suala la mkuu wa Mkoa wa Lindi kuingilia kati hilo haliwezekani.Haliwezekani kwa sababu Lindi hatuna mkuu wa Mkoa active,kazi aliyopewa ya ukuu wa Mkoa haiwezi...narudia tena mkuu wetu wa Mkoa kazi aliyopewa haiwezi ameprove failer.

Kuna wakati mke wa kijana mmoja alikuwa mjamzito wa miezi tisa kwa bahati mbaya akapata shida ya upumuaji dr wa zamu alikuwa dr Mlawa lakini alimchelewesha kumpatia huduma ya dharula akafia sehemu ya kusubiria wagonjwa,baadhi ya manesi walimuomba daktari mzee Mlawa amfanyie upasuaji yule mzazi ili kumnusuru kiumbe aliyeko tumboni lakini daktar Mlawa alikataa na mtoto alifia tumboni.

Hili jambo kuna daktari anaitwa Allex alihudhunika Sana alipoingia kazini na aliwalaumu wauguzi kwa nini wasingemuita kufanya uokoaji kama aliekuwepo alikataa.Kwa ufupi Sokoine hospitali ni njia ya kifo na uzembe ni mwingi mnoo.Mamlaka ziiangalie hospitali hii na kufanya maamuzi magumu lakini pia kumhamisha mkuu wa Mkoa kwa kuwa nadhani Mkoa wa Lindi umemshinda.
 
NISHAELEWA KWANINI NURSES WANAKUWAGA HARSH SANA EEH...KUMBE WANA SHIDA NYINGI MNO...

MATATIZO HAYO YAPO HIZO ZINAZOITWA HOSPITAL ZOTE ZA MIKOA NA WILAYA...

FANYENI KAMA WITO TU...ALLAH ATAWALIPA TU...HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA...
 
Nakubaliana na wewe juu ya uozo uliopo hospitali ya Sokoine Lindi shida ipo tena sana,watumishi baadhi hawatendewi wema katika kutekeleza majukumu yao lakini pia suala la mkuu wa Mkoa wa Lindi kuingilia kati hilo haliwezekani.Haliwezekani kwa sababu Lindi hatuna mkuu wa Mkoa active,kazi aliyopewa ya ukuu wa Mkoa haiwezi...narudia tena mkuu wetu wa Mkoa kazi aliyopewa haiwezi ameprove failer.Kuna wakati mke wa kijana mmoja alikuwa mjamzito wa miezi tisa kwa bahati mbaya akapata shida ya upumuaji dr wa zamu alikuwa dr Mlawa lakini alimchelewesha kumpatia huduma ya dharula akafia sehemu ya kusubiria wagonjwa,baadhi ya manesi walimuomba daktari mzee Mlawa amfanyie upasuaji yule mzazi ili kumnusuru kiumbe aliyeko tumboni lakini daktar Mlawa alikataa na mtoto alifia tumboni.Hili jambo kuna daktari anaitwa Allex alihudhunika Sana alipoingia kazini na aliwalaumu wauguzi kwa nini wasingemuita kufanya uokoaji kama aliekuwepo alikataa.Kwa ufupi Sokoine hospitali ni njia ya kifo na uzembe ni mwingi mnoo.Mamlaka ziiangalie hospitali hii na kufanya maamuzi magumu lakini pia kumhamisha mkuu wa Mkoa kwa kuwa nadhani Mkoa wa Lindi umemshinda.
Hii shida ya hawa watu wa afya hata muhimbili ipo...
 
Inaonekana wewe una chuki binafsi na RMO ... hayo uliyoyasema mengi RMO hawezi kuyatatua bali ni wizara ya utumishi. Pia siyo kweli kuwa Hosp hiyo haijatembelewa na Viongozi wa kitaifa muda mrefu .. Mwaka huu 2020 baada ya July Mganga Mkuu wa Serikali prof Makuabi alifika hapo na kuongea na sisi watumishi na kutatua baadhi ya Changamoto ikiwa na pamoja na maswala ya ujenzi , huduma na watumishi wanaosomeshwa na Serikali .

Tatizo hapa kuna wauguzi wamekaa muda mrefu sana na kuwa miungu na hawataki kuguswa na wananchi haki hata huyo RMO kwa kupewa kiburi toka sehemu za juu.
Nakuunga mkono
 
Mh: Rais MAGUFULI Mimi Kama mtanzania nachukua jukumu hili kukufahamisha kuwa hospitali ya mkoa wa Lindi Sokoine Ina watendaji/ viongoz wabovu kuwahi kutokea katika historia ya sekta ya afya mkoani Lindi.
Kwanza Kuna malalamiko kutoka karibu katika kila kada ya wahudumu wa hospitalini hapo ambapo baadhi ni Kama yafuatayo:
Wafanyakaz wengi hasa wahudumu wa afya, wauguzi ngazi mbali mbali Kama EN na RN, wataalam wa maabara n.k wahapewi haki zao mbalimbali Kama za posho za ziada ya kazi, watu hawajapandishwa vyeo Zaid ya miaka 7, wengine wamejiendeleza kitaaluma kutoka wahudumu wa afya mpaka kufikia kuwa ENROLLED NUSE na REGISTERED NURSE tangu mwaka 2015 lakin hawajafanyiwa mabadiliko ya kimuundo wala vyeo wala kubadirishiwa mishahara yao.

Aidha mganga mkuu wa mkoa hataki kusikiliza mfanyakaz shida zake na hata wengine wakienda kwa mkuu wa mkoa kutoa malalamiko wanaishia kusemwa kwa mganga mkuu na mwisho mfanyakaz huyo atakomolewa kwa kila namna. Ipo mifano mingi ya walioenda kuonana na RC lakini wakaambulia kufululiza zamu za usiku Hali inayoonesha RC na RMO ni Pete na kidole.
Kutokana na Hali hiyo, kila mfanyakaz anaogopa kuongea kwa hofu ya kuadhibiwa, na wengine Wanaoanga kwenda ofisi za usalama wa taifa kutoa malalamiko yao wanaishia kuogopa isije yakarudi Kama yalivyo kwa RMO maana hawajui wapi kupo salama kupeleka malalamiko yao
Kifupi hawana ari ya kaz hasa kada nilizotaja na kwa upande wa madaktari ni wale wanaoonekana kuwa na kelele na ujasiri huwa wanaitwa na RMO na kupozwa basi mengine yanaendelea. Wabapozwa kwa kufaham kuwa Wana uelewa wa wapi wakaseme hivyo jwa vile wanaweza kuleta udhia wanapenyezewa Rupia.
Ndugu Rais kitu cha ajabu ambacho wafanyakaz Hawa wanashangaa tangu Serikali yako iingie madarakani mwaka 2015,hakuna kiongoz wa kitaifa aliyeingia pale na kusikiliza changamoto za kiutendaji wala miundombinu, wewe binafsi mwaka 2019 uliahid kwenda huku ratiba yako ikionyesha ungefika kanisan RC Mtanda ukasali yakafanyika maandaliz yote ukaondoka juu kwa juu, waziri mkuu ambae ndio kwao hajawahi hata siku moja kukanyaga maeneo ya hospitali hiyo, aliyekuwa waziri wa afya UMMY MWALIMU alijaribu kuingia kwa kupitia mlango wa nyuma akafanikiwa lakini hakufikisha dakika kumi akaondoka bila kuongea na wafanyakaz.
Ndugu Rais wapo wanaoamin uongozi wa hospitali hiyo ni washirikina Sana kiasi hawako tayari kuona viongoz mnafika pale na kuhoji MADUDU yanayoendelea Kwan RMO yuko bize kujenga maghorofa yake mtaa wa Mtanda huko juu. Hadi inaaminika hospitali hapo miongoni nwa wafanyakaz kuwa huenda WAKUBWA wote hamtafika hapo tofauti na RC mwenye ukaribu na RMO (Waarabu wa Pemba) na kwamba hata ule moshi uliletewa ukiwa njian kutoka ruangwa unaelekea Lindi 2019 inaaminika ulitoka kwa viongoz wa hapo Sokoine kwa kushirikiana na RC Zambi anayesadiki vitendo vya dhambi Kama matamshi ya jina lake ( huyu mchunguze vizuri Ana mambo mengi hata kwenye vyama vya ushirika wanamtaja Sana).
Ndugu Rais, pole kwa kukuchosha lakin najua unavyanzo vingi kuliko mm, fatlia haki za kiutumishi na kimaslah za wafanyakaz wa hospitali hii yenye miungu watu Kwan wanaogopa hata kuja kwako wakihofia pengine badala ya kupata haki wanaishia kufukuzwa kutokana na wanavyofananisha msululu wa matukio.

Baadhi ya majina ya watumishi ninayo na nyaraka zao walizolalamika kwa viongoz mbalimbali imeshindikana hadi wengine kushauriwa wakalalamike Usalama wa taifa na kukosa ujasiri wa kufanya hivyo. Ukihitaji hayo hata kwa mguu nitakuletea Chamwino unaunguza Sana watu wanavyoteseka. Fikiria mtu amebadilishiwa muundo 2015 hakuna mabadiliko hata ya mshahara maana yake haki yake ya kupanda cheo 2018 ameikosa na mwakani Anaweza asipande tena na akifa anapata mapato ya mshahara wa sasa wa laki 6 wakati alitakiwa awe kuanzia milioni moja na laki 4 huko, mbona yule nesi mrembo wamesoma nae wote yeye alishabadirishiwa vizur na anaish safi au tuwaalike akina Mbugo wa PCCB? hata wakialikwa Nani wa kutolea maamuz ya wafanyakaz Hawa.
Ndugu Rais tunakupenda Sana hasa kwa style yako ya kujali wanyonge na kujitoa kisafisha uozo Serikalin na bado tunaiman kubwa na wewe. Allah akujaalie kheri, afya ukakamavu wa kumshinda shetani aliyetawala SOKOINE HOSPITAL Lindi ili kuepusha madhara kwa wanaofuata huduma za afya hospitalini hapo
Andika barua kwenda kwa Katibu Mkuu Afya ndiyo mamlaka yako ya nidhamu na siyo RMO , RMO yupo TAMISEMI wewe Wizara ya Afya kwanini watumishi wa umma mnakuwa hamuelewi?
 
Hujitambui wewe siku ukijitambua utaacha huu ujinga wako. Yaani unapeleka malalamiko kwa Magufuli mtu ambaye amekusababishia matatizo yote unayolalamikia. Wewe chapa kazi tu haki zako utazipata kwa Mungu na siyo kwa huyu Magufuli.

Nikukumbushe tu April 2016 Magufuli aliagiza kuhamishwa Madaktari 16 kutoka hospitali ya mkoa wa Mtwara(Ligula) kwa sababu walikuwa na malalamiko kama haya ya kwako.

Yaani miaka yote hii ya utawala wa Magufuli bado kuna watumishi wa umma wanamuona Magufuli ni mtu wa kujali shida zao? Kweli nchi hii imejaa wajinga.
 
NISHAELEWA KWANINI NURSES WANAKUWAGA HARSH SANA EEH...KUMBE WANA SHIDA NYINGI MNO...

MATATIZO HAYO YAPO HIZO ZINAZOITWA HOSPITAL ZOTE ZA MIKOA NA WILAYA...

FANYENI KAMA WITO TU...ALLAH ATAWALIPA TU...HAPA DUNIANI NA KESHO AKHERA...
Tatizo wewe unafanya kwa wito unalala na njaa wenzako wanakula kwa raha. Nani anapenda kukaa na njaa? HAKI itolewe kwa wote utaona kazi zinaenda vizuri na malalamiko yatapungua
 
Andika barua kwenda kwa Katibu Mkuu Afya ndiyo mamlaka yako ya nidhamu na siyo RMO , RMO yupo TAMISEMI wewe Wizara ya Afya kwanini watumishi wa umma mnakuwa hamuelewi?

Kweli mkuu huyu labda mgawanyo huo haujui ndiyo maana ameyaandika hayo,anawazia tu akimwandikia Rais atapata majibu kwa haraka. Maana hapohapo hospitali pia utakuta wafanyakazi wa Tamisemi na Serikali kuu ambapo utaratibu wa kupeleka malalamiko una utaratibu wake kwa hayo maeneo mawili.
 
Anayoyasema mleta maada yafanyiwe kazi. Hata hapa Morogoro ukienda kitengo Cha ICU ni shida. Watoto wanakufa sana Ila takwimu zinafichwa. Jumamosi iliyopita mtoto amefariki kisa wamechelewa kubadilisha mtungi wa oxygen. Nurse wako busy wanauza pampasi za jero jero. The health sector is in deep shit
 
Hali ni ngumu kwenye hospitali zetu,wakati mwingine tupunguze kuwalaumu watendaji wetu. Maana hospitali haina hata dawa wala vifaa,halafu mkubwa wa hospitali pamoja na wanasiasa wanawaambia wafanyakazi mkiulizwa semeni dawa na vifaa vipo. Hivi hapo tunamdanganya nani? Kama hospitali itakuwa na dawa za kutosha na vifaa vya kutosha utendaji utaimarika na huduma zitakuwa nzuri na hata idadi ya vifo pia itapungua. Tuwe makini na wanasiasa wanaotudanganya na kututangazia kuwa kila kitu kipo pale hospitalini nendeni mkatibiwe.
 
Back
Top Bottom