Rais Magufuli mulika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, kuna ufisadi na wewe ni kiboko ya mafisadi

ndege joni

JF-Expert Member
May 23, 2017
540
1,000
Kama inavyojieleza.

Mimi nasomesha wadogo zangu, mmoja yupo SUA na mwingine yupo UDOM. Niachane na maelezo mengine ila huyu wa SUA michango ni mingi kuliko wa UDOM, mpaka nashindwa kuelewa.

Maana baada Waziri wa Afya kutangaza kuwa bima ya afya inatakiwa ilipwe serikalini moja kwa moja, na sio 100,000/= kama walivyokuwa wanalipa chuoni inatakiwa iwe 54,000/=.

Basi kuna mchango wa tahadhari umejitokeza usiokuwa na control number wa 50,000/= ambao wanafunzi wote wanatakiwa walipe.

Ukiwauliza wanasema kuwa mwanafunzi akiugua anatakiwa agharamikiwe na Chuo, ndio hiyo 50,000/=.

Sasa sielewi hilo tukio la kuwapeleka hospitali wanafunzi waliolipia bima hizo gharama kubwa kiasi hicho lishawagharimu kiasi gani siku zilizopita na inasadikika kuna wanafunzi zaidi ya 15,000/=.

Hapa Mhe Rais tunaomba utume timu yako iangalie.
 

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
7,181
2,000
Iyo hela ya Bima NHIF kwa wanafunzi sio 54,000/= ni 50,400/=.

Kuhusu michango ya Afya sio Chuo iko tu vingi sana vinafanya ivo ila vinaijumlisha katika Direct cost.

Unakuta Chuo kina Zahanati ndogo so dogo anaweza pata jelaa dogo mfano anavocheza soka so atahitaji First Aid, basi iyo hela ndio itafanya mambo hapo.

Ila kama haina Control Number ilo swala jingine sasa. Ninavojua kila mchango lazima uwe na control number.
 

ndege joni

JF-Expert Member
May 23, 2017
540
1,000
Mad Max,

Asante kwa marekebisho kiongozi ila gharama ya 50,000/= ni kubwa kuliko hali inavyotakiwa. 50,000/= x 15,000/= ni pesa mingi sana
 

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,726
2,000
Mkuuu Gawio kwanza hayo malalamiko yako baadae. SUA lazima wampite IFM kwenye gawio na hizo zako lazima pia zikumbwe na fagio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom