Rais Magufuli muendelezaji wa utumbuaji majipu ulioanza kwenye mchujo wa wagombea.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Ulihitajika ujasiri wa hali ya juu kuweza kuliondoa jina la EL ili lisiwe kuingia ndani ya tano bora ya wagombea wa CCM mwaka jana. EL alikuwa na nguvu ya kuweza kupata wadhamini maelfu kwa maelfu, tena kila mkoa.
Inasemekana watendaji wakuu wa halmashauri karibu zote walikuwa ni watu wa mzee kutoka Monduli, hivyo alikuwa na mizizi mizito sana ambayo katika hali ya kawaida sio rahisi kung'olewa.
Wazee ambao walikuwa ni marais wa awamu zilizopita walifanya kazi ya ziada kuweza kulitumbua jipu zito, lakini walikuwa hawajui kwamba JPM atakuja na falsafa ya utumbuaji wa majipu. Wao walifanya kwa sababu ya kutaka kutokuona CCM ikiwafia mikononi.
Anachokifanya rais kwa sasa ni muendelezo tu wa utumbuaji wa majipu, kwani mwanzo au baraka za akifanyacho, ni tendo la ujasiri wa hali ya juu wa kulitumbua jipu zito.
Uwezo wa kufanya maamuzi magumu ni sifa ya kiongozi bora. Mfano halisi ni utumbuaji wa jipu zito wakati wa kutafuta mgombea wa CCM mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom