Rais Magufuli, mtumbue CAG Assad au TR Mafuru au wote

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali-CAG Prof. Musa Assad na Msajili wa Hazina-TR Laurence Mafuru wameshatofautiana. Kikauli na kitaarifa. Tayari ni mara mbili. Hawachangamani. Mara ya kwanza wametofautiana kwenye suala la PRIDE Tanzania. Wakati CAG akisema hilo ni shirika la kiserikali,TR akasema ni shirika lisilo la kiserikali.

Mara ya pili ni kuhusu UDA. Wakati CAG akisema UDA haijauzwa,TR anasema UDA imeuzwa. Kupishana kwa kauli kwa waandamizi hawa wa kiserikali ni jambo sensitive. Extremely serious matter. Hawa wanapaswa kushughulikiwa. Kushughulikiwa kwa namna ya kumtoa mmojawapo au wote.

Ima CAG Assad au TR Mafuru,mmoja anapaswa kutumbuliwa. Kupishanapishana kwa kauli kutapunguza au kuondoa imani ya wananchi kwa kauli za serikali. Yatarudi yale mambo ya za umma...si za umma za Escrow! Wasibaki wote tena!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Mafuru anajitumbua mwenyewe..Kumbuka swala la NBC.Huyu sijui ni ngosh kutoka wapi au kwa kuwa amekulia hapo uswahilini
 
Leo nilimsikia Mafuru TBC FM akihojiwa na kukiri kuwa kumekuwa na makosa makubwa katika mchakato wote wa kuuziana shirika hilo. Serikali inarekebisha makosa hayo na wahusika wanajulikana watachukuliwa hatua.

Ripoti za ukaguzi siyo kama za uchunguzi. Ukimnyima ushirikiano na kutompa nyaraka za kuonyesha mauziano, mkaguzi atasema halijauzwa.
 
Huyo Laurence Mafuru ni wale wale, hana maana hata,

Anatafauti gani na yule au wale waliosema Escrow si fedha za umma/serikali !?

Kaka Rais huyu muangalie kwa jicho pevu huyu,

Yaani sisi CAG anajitahidi kutuonyesha mali zetu zipo wapi yeye anakumbatia maslahi ya tumbo lake,

Hizi teuzi nyingine mnatuchanganya inatubidi turudi kule kwenye # Katiba mpya.
 
Kila mtu atakuwa ana sehemu ambayo anategemea katika kufanya maamuzi! Watupe facts zao
 
Wa kutumbuliwa ni huyo mafuru.ila prof. Assad hapana.

I swear nitapiga kolabo na akina faiza fox,Ritz na Mohamed said kumtetea japo Mimi siyo wa upande ule kiimani.

si mnaona jina la dkt dau linapotajwa hali inavobadilika.
Ni hatari sana kutanguliza imani za kidini katika kufanya maamuzi. Kama aliyekosea ni mkristo tuache taratibu na miongozo ya kiutendaji ichukue mkondo wake.
Ni vema watu tukaangalia rekodi za kiutendaji za hawa watu. Kwa utendaji huwezi ukalimlinganisha Assad na Mafuru, Assad kwa wale tunaomfahamu ni daraja lingine kabisa. Assad hana makandokando ya kiutendaji kama Mafuru.
Na kwa hali hii inavyoendelea, itafika hatua utaweza kuamini Mafuru yuko pale kwa suala moja tu, kuficha na kulinda nyaraka za madubwana yanayotiliwa mashaka ili ukweli halisi usipatikane.
 
mkuu usichukulie serious sana hapo kwenye imani.

nilichombeza tu kuchangamsha mnakasha.
tupo pamoja.
 
Prof. Asad ni jembe, Mchango wake unaonekana ila anakwamishwa na wachache. Naona mzimu wa Dr. Dau bado hauja wakaa vizuri.
 
mkuu usichukulie serious sana hapo kwenye imani.

nilichombeza tu kuchangamsha mnakasha.
tupo pamoja.
Aksante sana kwa chombezo, ila wengine tunauangalifu sana kwenye hilo ili kuondosha misigano isiyo natija kwa taifa letu.
 
Kwa mtazamo wangu nahisi wote wako sahihi. Mafuru yuko sahihi na prof Assad nae yupo sahihi ingawa kikauri wanatofautiana. Mafuru kama mtu wa hazina ameambiwa UDA imeuzwa na kaletewa documents halafu kule kwenye shirika lenyewe ambalo CAG anaenda kukagua hakuna document yoyote ya mauziano au ya kubadirisha wamiliki, Assad hapo atasemaje na Mafuru nae atasemaje?
 
Mwenye uhakika ni CAG,TR siyo Mkaguzi,alipaswa kuwasiliana na CAG kabla hajatoka kwenye Media.Unapommnyima Mkaguzi documents maana yake hazipo siyo kwamba umenyima bali hazipo wala hayo mauziano hayapo.CAG yupo sahihi.
 
Mafuru ni kiherehere tu wala hata hahitajiki, mtu pekee mwenye mandate ya kikatiba kuuelezea umma masuala yote ya fedha ni CAG basi, huyo kilaza cjui hata kaibukia wapi, yeye ni msimamizi wa mashirika ya umma, lakin hawajibiki kutupa taarifa za mashirika ya umma, sababu sio independent, jaman mbona tunapenda kupindisha mambo namna hii ili kutafuta majibu tunayopenda kuyasikia.
 
Back
Top Bottom