Rais Magufuli mtumbue Bosi wa TTCL anaihujumu kampuni

Jan 9, 2020
54
125
Shalom,

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mh Rais tunaomba umtumbue boss wa TTCL haiwezekani tangu apewe uongozi mwaka 2016 mpaka leo kampuni ipo ovyo.
Kampuni haijiongezi na pia huyo boss sio mbunifu kabisa.
Yaani 52% wa watumiaji wa TTCL hawajui menyu ya kuangalia salio ipoje.
Kampuni haina ofa kwa wateja wake utadhani inauza nyanya.
Watoa huduma wa Costumer Care ndiyo ovyo baba, ukimpigia simu anakujibu oke, sawa, yes mpaka sometimea nafikiria kuwatongoz baba.

Huduma mbovu haziridhishi kabisa. Mtu yupo tu ofisini anapunga upepo hana hata hadhi ya kuongoza kampuni kama hiyo.

Tafadhali tunaomba umpe uongozi mtu mwingine mwenye huruma na Watanzania.

Mbaya zaidi mtu mwenyewe anamiliki hisa zake huko kwenye kamouni ya SMILE. TTCL ipo tangu 1993 hadi leo huduma ovyo.

Halotel wamekuja juzi tu hapa lakini wamekiwasha balaa mpaka wanyonge tunakimbilia kule.

Waziri Kindamba OUT
Unaiharibu TTCL yetu.
Yaani watoa huduma baada ya kutufuata sisi wao ndio wanataka sisi tuwafuate.

Asanteni
 

KITAULO

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
1,740
2,000
Waziri huyu huyu ninayemjua mimi ni moja ya kampuni za mwanzo kabisa kutoa gawio kwa serikali...hebu ngoja nijiridhishe kwanza.
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,662
2,000
Namba hazidanganyi,

Kindamba kaikuta TTCL mahututi mbapaka sasa inatoa gawio serikalini. Tatizo kuu lilikua ni mtaji na hakupewa,anafanya maboresho kutokana na mtaji mdogo uliopo,hata awekwe mwingine hataweza kufanya zaidi ya huyu Kindamba.
 

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,641
2,000
Namba hazidanganyi
Kindamba kaikuta TTCL mahututi mbapaka sasa inatoa gawio serikalini
Tatizo kuu lilikua ni mtaji na hakupewa,anafanya maboresho kutokana na mtaji mdogo uliopo,hata awekwe mwingine hataweza kufanya zaidi ya huyu kindamba
Anakuwaje na mtaji mdogo wakati anaipa serikali gawio?
 

Percy

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
6,079
2,000
Uko sahihi ila bado haujasema TTCL wanafeli wapi? Offers, Miundombinu, teknolojia, Bundles, Customer care service? Hebu orodhesha vitu wanavyofeli jamaa toa facts hata uongozi wakisoma wajue kweli wamefeli ukicompare with others kwenye ushindani.

List them all.

Binafsi naona upande wa bundles wako fair mnoo.. bei chee speed ya 4G tena ukiwa na laini ya chuo unaweza hisi unamiliki kampuni nzima😂🙌🏽 hongera sana Boss wa TTCL kwa hili, ila network yao haiko strong baadhi ya maeneo Dar Es Salaam hii hii 🥺. Yaani hilo gawio walilotoa ni bora wangetumia kutengeneza minara strong ya 4G kuliko kututesa wateja wao.
 

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
492
1,000
Nadhani kama una malalamiko na TTCL ni vizuri kushare hata hapa hapa, lakini personal attacks hazitamfanya Kindamba na TTCL wafanye kazi vizuri. Waoneshe udhaifu sana.
 

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
1,150
2,000
Kindamba kwa namna fulani kajitaidi, Tukumbuke kwenye telecom industry kunahitajika uwekezaji mkubwa sana mpaka kampuni/shirika lisimamame lipambane na washindani wengine, kitu ambacho nahisi kwa TTCL hamna uwekezaji mkubwa wowote uliofanyika, wanaenda kwa kusuasua, hata leo umchukue CEO wa vodacom umtupe ttcl hamna cha maana atafanya.

Serikali na biashara ni kushoto na kulia, serikali kwa kawaida ina uasilia wa kutoa huduma kwa hiyo swala la hasara au ufinyu wa mapato ni jambo la kawaida na wana uhakika wa ku cover up kwa kodi za wananchi, ila ukija kwenye makampuni binafsi kitu kikubwa kinaangaliwa ni faida na ukuaji mzuri wa kampuni ndani ya kipindi kifupi ama kirefu kulingana na malengo ya kampuni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom