Rais Magufuli: Mtu akitaka kukiona cha moto ajaribu kumshambulia Mwana-CCM aliyevaa kijani

Rais Magufuli anasema kama mtu anataka kukiona cha moto ajaribu kumshambulia Mwana-CCM yeyote aliyevaa kijani.

Mimi najiuliza, je wananchi wanaovaa kaki hawana haki ya kulindwa?

Tuna rais mbaguzi sijawai kuona yaani wakina mawazo mpaka waliuawa na watu kibao wanashambuliwa kisa wamevaa kaki hakuna hatua zinazochukuliwa.

Tuna Rais mbaguzi sana.
Acha kupandikiza chuki miongoni mwetu, husikilizi/huangalii peke yako hii hotuba.
 
Kabla ya kuuliza hilo inabidi ujiulize ulishawahi kuona mtu kavaa kaki au gwanda akizomewa au kupigwa kwa ajili ya vazi? Kama yupo mtaje tuanzie hapo, na kuhusu kupigana hilo ni swala lingine walishapiwa wa chadema na pi hivyo hivyo wa ccm walishapigwa ajili ya siasa hilo lipo., mki nadhani tatizo lipo mtu akivaa nguo ya kujani watu wanaanza kumtukana bila sababu hilo ndo nadhani anakemea.
Watu hopeless kama wewe mnatakiwa kuishi Burundi tu
 
Huyu mzee sijui hua anafikiria nini kabla ya kuongea, juzi kaombwa msaada wa maji alieomba akaambiwa akamuombe mume wake, au diwani wake (upinzani) au mbunge wake (upinzani).

Leo anasema viongozi wawatumikie wananchi wote bila kubagua chama, itikadi, wala dini kwani manendeleo hayana vyama.

Leo tena anatoa KINGA kwa wanaovaa kijani (wanachama wa CCM).

#Hizi kampeni za uchaguzi wa urais #2020 zitasababisha tafrani kuelekea uchaguzi mkuu, tusubiri upinzani waanzishe amsha amsha kwenye uchaguzi mkuu kwa KUTUMIA KAULI ZA MKULU.

Aache "kujimwambafai"
 
Uchaguzi wa mwakani kuna watu wengi sana watauawa.
Huyu mzee sijui hua anafikiria nini kabla ya kuongea, juzi kaombwa msaada wa maji alieomba akaambiwa akamuombe mume wake, au diwani wake (upinzani) au mbunge wake (upinzani).

Leo anasema viongozi wawatumikie wananchi wote bila kubagua chama, itikadi, wala dini kwani manendeleo hayana vyama.

Leo tena anatoa KINGA kwa wanaovaa kijani (wanachama wa CCM).

#Hizi kampeni za uchaguzi wa urais #2020 zitasababisha tafrani kuelekea uchaguzi mkuu, tusubiri upinzani waanzishe amsha amsha kwenye uchaguzi mkuu kwa KUTUMIA KAULI ZA MKULU.
 
Nibora ungeleta hotuba yote sio kusort maneno yako yenye lengo ovu
Mwehu wewe endelea kubinua masaburi huko lumumba
tapatalk_1565762914493.jpeg
 
Magufuli ni rais mzuri sana ila vitu vinavyomshushia hadhi ni vidogo vidogo sana

Anakosa utashi sio kama tu kiongozi bali kama gentleman

lakini namkubali kwa kuwa ana uthubutu kwa mambo makubwa mapungufu yake ni hayo ya kugawa watu
Kugawa watu unaona ni jambo dogo? akishathubutu kuyajenga hayo alafu akagawa watu na watu kuyaaribu...faida ni nini sasa? kama unayaita kugawa watu ni jambo dogo basi inabidi ujiangalie sana.
 
Mbona unaniletea mihemko mzee huwezi sems hoja hadi unichimbe mkwara
 
Rais Magufuli anasema kama mtu anataka kukiona cha moto ajaribu kumshambulia Mwana-CCM yeyote aliyevaa kijani.

Mimi najiuliza, je wananchi wanaovaa kaki hawana haki ya kulindwa?

Tuna rais mbaguzi sijawai kuona yaani wakina mawazo mpaka waliuawa na watu kibao wanashambuliwa kisa wamevaa kaki hakuna hatua zinazochukuliwa.

Tuna Rais mbaguzi sana.
Mkuu ungetafuta clip ya maneno hayo ungeupa uhai mpana huu Uzi.
Kauli zake nyingi zinakerehesha sana
 
Magufuli ni rais mzuri sana ila vitu vinavyomshushia hadhi ni vidogo vidogo sana

Anakosa utashi sio kama tu kiongozi bali kama gentleman

lakini namkubali kwa kuwa ana uthubutu kwa mambo makubwa mapungufu yake ni hayo ya kugawa watu
Huyu Jiwe anahitaji sijui nisemeje!
 
Magufuli ni rais mzuri sana ila vitu vinavyomshushia hadhi ni vidogo vidogo sana

Anakosa utashi sio kama tu kiongozi bali kama gentleman

lakini namkubali kwa kuwa ana uthubutu kwa mambo makubwa mapungufu yake ni hayo ya kugawa watu
Hayo unayoyaona madogomadogo ndio yenye simu Kali kiasi kwamba waathirika hata ukiwanywesha maziwa hiyo simu haitaisha yote.
 
Selemani alikuwa na akili sana. Mungu alipomwambia aseme alichokuwa anataka ampe yeye akaomba hekima.

Alijua ili ufaulu ktk uongozi ni hekima ndio ingekuongoza na ndio maana hakuomba ubabe wala mali.

Duniani humu kama ulizaliwa kiongozi itajulikana tu na kama umeotea kama aliyeokota embe jangwani pia itajulikana vile vile.
 
Rais Magufuli anasema kama mtu anataka kukiona cha moto ajaribu kumshambulia Mwana-CCM yeyote aliyevaa kijani.
Ina maana wengine wote wasiovaa kijani wakishambuliwa... ni sawa?
Na hapo hapo inatoa maana kwamba "MwanaCCM yeyote aliyevaa kijani" akimshambulia asiyevaa 'kijani,' mwanaCCM huyo afanyweje...atuzwe, asifiwe?

Sijui kama anayeyasema haya maneno anaelewa 'implications' zake kwa taifa hili.
Huu ni uongozi wa kutugawa waTanzania.

Wazee wenye busara wasiruhusu hali hii kwa kukaa kimya.

Mzee Mwinyi anaogopa kuwekwa kizuizini? Mbona hiyo ingekuwa ni heshima kwake kwa umri alio nao kwa kuonyesha analijali taifa alilowahi kuliongoza!
 
Haya unaweza kuyaona ni madogo lakini madhara yake ni makubwa due tutafika stage tuanze ulizana makabila kama ilivyo kwa kenya ko umoja wetu hautakuwepo kwa ss hivi ni uhasama unajengwe tu miongoni mwa watu kwa kuona kuwa kundi moja linabebwa zaid kwao wataona kila wanachofanya ni sahihi hata kama ni kinyume na utaratibu
Ukabila uingieje wakati yeye kazungumzia CCM. Nyie ndo kila jambo mnalichukulia kikanda something very wrong. Kama hukubaliani na maneno yake usihusishe kablia lake kila mtu na zake mkichwa
 
Magufuli ni rais mzuri sana ila vitu vinavyomshushia hadhi ni vidogo vidogo sana

Anakosa utashi sio kama tu kiongozi bali kama gentleman

lakini namkubali kwa kuwa ana uthubutu kwa mambo makubwa mapungufu yake ni hayo ya kugawa watu
Huko kugawa watu ndio failure kwa kiongozi. Sifa kuu ya kiongozi ni uwezo wake wa kushawishi na kuwaweka pamoja watu wenye mitazamo inayotofautiana.

Vv
 
Back
Top Bottom