Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Kama ni hivyo nami nashauri watanzania tujihami na hao watekaji kwa kupiga yowe la majambazi ili hata kama ni vyombo vya usalama basi wakaendeleze utekaji peponi. Zakaria was very right to shoot them. Wananchi walitakiwa wawaponde mawe
Angalau tukio hili la Zakaria kule Tarime, na pia la Nape Dar yanathibitisha Ni kina Nani watekaji na wauaji..

Ameongelea watekaji tuu, mbona hazungumzii wauaji Kama wale waliotaka kuua TL ??!
 
"Magufuli ni miongoni mwa watekaji! na sasa hataki kusikia kelele za anao waumiza". Anacho fanya ni intimidations ili watu tukae kimya huku tukiona wenzetu wakipotea! Kuna matukio mengine ya wazi kabisa yanayo wahusisha usalama wa taifa, kama lile la Zakaria....yapo mengine yasiyo kuwa na majibu na mengine yenye majibu ya kitoto masikioni mwa wenye timamu.
Hslafu mlivyo mazuzu uchaguzi mkuu mnamchagua,, jaman nyi watanzania lol
 
Hapo kwenye kuzuia watu wasijinyonge Kamanda amezurura aisee. Siriazi kabisa anasema hadharani watahakikisha wanawasaka na wanawakamata watu wanaotaka kujinyonga. Sasa utathibitisha vipi mtu ana mpango wa kujinyonga maana hata anaeenda kujinyonga akifika barabarani anavuka kwa uangalifu asije akagongwa.
Wenyewe mashhabiki wa utawala huu wanaelewa eti
 
Siku mtu Fulani akiondoka humu duniani tbl rekodini mauzo yenu hamtaamini.
Naunga mkono hoja. Sijui ikitokea (nahisi lipo njiani) halafu inikute sina fedha sijui nikamkope nani. Siku hiyo ugimbi hadi lukela
 
Watu hawasemi haya bure bure.

Tuanze na kesi ya Dr Ulimboka. Jamaa alitekwa na akateswa sana, na waliomtia kwenye mtego aliwataja kwa majina hadi namba zao za simu, wako state house. Nini kilifanyika kutatua huu uhalifu?

Vipi kuhusu Ben Saanane. Mara ya mwisho alisema amepigiwa simu ameitwa na mtu, hajaonekana mpaka leo! Uchunguzi umefika wapi? Kama mmekwama, wenzenu huwa wanaomba msaada kwa wananchi. Nyie kimya.

Vipi kuhusu Azory, mmefanya juhudi gani mpaka sasa? Mkewe amesema walikuja watu kumchukua wakiwa na gari. Mmefanya juhudi gani kuchunguza, waziri anakuja kuleta kejeri, mwingine anasema disappeared and died.

Lissu alilalamika mpaka akatoa aina na namba za gari zinazomfuatilia. Amepigwa risasi kwenye nyumba za serikali, uchunguzi umefika wapi? Taarifa za gari lilikuwa linamfuatilia zimefikia wapi?

Vipi kuhusu mwenyekiti wa halmashauri Kigoma, alipotelea kwenye ofisi ya halmashauri. Nini kimefanyika so far.

Vipi kuhusu Lwajabe, na kifo cha utata? Vipi kuhusu Zakaria wa Mara.

Serikali inapaswa kujua, nature abhors vacuum!

Kunapotokea mambo, halafu kukawa hakuna majibu, watu watajaza wenyewe. Na wasilaumiwe wakifanya hivyo. Haiwezekani visa vya ajabu ajabu vinawakuta watu wa kundi moja: wakosoaji wa serikali.
 
Mh anasahau watumishi wa TISS si maraika ni binadamu tunaishi nao wengine madem zetu wengine shemeji zetu kwaiyo hawa madem zetu tukiwakoleza wanaropoka pia wale shemeji zetu dada zetu wakiwapa vizuri wanalopoka

Mfano sasa hivi tupo kuwabembeleza kweli hawa nadem zetu wa TISS watuambie kwanini mh anapenda kuvaa koti moja tu why kwanini?
Sijaelewa juu ya koti moja
 
Mzee mmoja alimpandisha kijana wake juu fensi, akamwambia kijana wake 'ruka chin nitakudaka' kijana akaruka then Mzee akamkwepa, Kijana akadondoka chini, kijana alilia kwa uchungu akamuuliza Baba ake kwanini umeniacha nianguke?

Baba ake akamwambia nlitaka ujifunze kutoamin mtu/ watu.
Nime ipenda hii hadithi
 
Back
Top Bottom