Rais Magufuli, mpime Makonda kwa kipimo cha utu wa mtu!

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,239
9,527
Utu wa mtu ni jambo la msingi ambalo kwa ubinadamu wetu, bila kujali itikadi ya vyama vyetu au jinsi tunavyoonekana, wote tumezaliwa sawa na hakuna kigezo kwa yeyote kati yetu kuishi kwa manyanyaso.

Samahani ila, Kwa pamoja kama watanzania tumefanikisha mambo mengi kwa umoja ulioshikiliwa na heshima yetu kwa utu wa mtu. Tumeyafanikisha hayo kabla, ya uhuru, wakati wa uhuru na baada ya uhuru kwa lengo la kuhakikisha utu wa mtu unalindwa.

Tumepambana na magonjwa wakati wote huu bila kujali itikadi zetu kisiasa, tumechangia nchi nyingi kupata uhuru, na leo pamoja na mapungufu, bado tunapiga hatua kwenye elimu, tuna piga hatua watu watoke kwenye umasikini. Ila kazi yetu bado haijakamilika, na haitakamilika Kama tutarudi nyuma sana kwenye jambo lililompa Nyerere jina kimataifa. Jambo linayoyapa maisha ya binadamu wote maana, UTU WA MTU.

Leo watumishi wa umma wanaonekana hawana umuhimu, Mungu anipunguzie hasira maana baba na mama yangu ni watumishi na ningekuwa kinondoni wakati ule Makonda anawadhalilisha watumishi wa ardhi ningemkata mabanzi straight away!

Kuna mambo mengi ambayo bila umoja wetu kama watanzania hatuwezi kufanikisha kama tutaona hakuna uzito kwa mmoja kati yetu kudharauliwa na kudhalilishwa. Yupo kijana mmoja -Bouzine, ambaye alijiwasha kwenye historia ya majuzi kwaajili ya manyanyaso tu ya mgambo na nchi ikawaka, rais akaondoka madarakani.

Kitendo cha Makonda kuwadhalilisha watumishi wa ardhi kinondoni ni kitendo kinachoumiza dhamira za wengi, ni haki na usawa na utu wa mtu vilivyokanyagwa bila kipimo.

Magufuli turudishe pamoja kama taifa ili kutambua mabadiliko tunayoyataka. Sio kila mabadiliko ni maendeleo.
Leo tukitaka viwango vikubwa vya utendaji kwa kila mtu katika taifa tuanze na viongozi, tuanze na midomo yao. Mheshimiwa rais, tuanze na Makonda.

Ili mabadiliko yatokee, kila mtu afanye nafasi yake. Kwa hili mimi nimefanya yakwangu. Bado wewe!
 
Mkuu mnapoteza muda wenu bure , kumbuka huyu kijana alipewa nafasi na Magufuli kumdhalilisha kiongozi mwandamizi Wilson Kabwe mbele ya hadhara na kuna waliodai kitendo hicho kilisababisha kifo cha yule mzee .
 
Mkuu tujaribu tu kuliimbia hili sikio lililokufa, labda siku moja litafufuka litusikia.
Kuyanyamzia haya kwa miaka minne iliyobakia, four painful years, yataka moyo
 
MAKONDA mm nakwambia kwa uzuri tu,Amani na utulivu,Kumbuka hata Amri kumi xa mungu zinasema waheshimu babayako na mamayako,kitendo cha kumpiga yule mzee rika ya babayako lazima ikufikishe pabaya wewe na uzaowako wote,mm nashangaa watu wanakushangaa lakini hawajui laana ndi imeanza kukufuata.Yule mzee ni baba yako kabisa ulivo mnasa vibao adharani ulitegemea watumishi wenzio utawaacha? na ukumbuke hata huyo anaekupa kiburi kuna siku utamuwakia tu.
 
Kama ni laana basi iwe yake, isiwaumize watanzania wote!
 
Magufuli asipojibu kwenye hili la Makonda ategemee majibu kutoka kwa raia wema wa nchi hii.
Paul Alex umeangalia angle moja tu ya wafanyakazi wa ardhi, umeshawahi angalau kuumiza kichwa chako ni kujiweka kwenye angle ya wale wanaodhulumiwa haki zao na hao hao wanaoonekana kudhalilishwa na mheshimiwa mkuu wa mkoa?.

Umeshawahi kuongea na wazee wanaonyanganywa kilicho chao na hao hao ambao walizoea kujiona miungu watu?.

Mkuu kuna mwenyekiti mmoja wa serikali ya mtaa hapa jijini, ukiingia ofisini kwake kwanza lazima uwe na tshs 20000 ndipo muongee nae, jaribu kujiweka kwenye mazingira ya wale ambao hawana hiyo fedha na shida zao zinahitaji utatuzi wa haraka.

Mnapoanzisha uzi msiwe mnafuata mkumbo jaribuni kuangalia reality ipo vipi ili msije kuonekana hamjui mnachokiandika.
 
Alichofanya Makonda ni sahihi?
 
Alichofanya Makonda ni sahihi?
Mkuu ni sahihi sana tu. Ulitaka tuendelee na utaratibu ule ule wa kuishi kirasimu?.

Mkuu kuna watu wananyanyasika sana, kama wewe sio mmojawao tambua kuwa wapo wengi.

Dhuluma mbaya sana imefanyika nchini mwetu kwenye masuala haswa ya ardhi. Ilikuwa ni lazima maamuzi ya kijasiri yafanyike.
 
Achilia mbali kwamba wale watumishi wa ardhi wa Kinondoni walijitahidi kujibu kadiri ya uwezo wao ila Makonda amekosea.

Kulikuwa na tatizo na alikuwa na nia ya kulitatua ila frustration sio jibu.
Hakuonyesha sifa yoyote ya uongozi kwenye approach yake.
Hakufanikisha chochote kwa kutukana zaidi ya kudhalilisha taasisi iliyomteua, kujidhalilisha yeye mwenyewe, kuidhalilisha sheria na kudhalilisha watu wanaoamini katika sheria.

Ameweka doa jeusi kwenye imani ya watanzania kwa uongozi wao na amewaangusha vijana kwenye harakati zao za kuongoza na kuingia kwenye nafasi za uongozi.

Makonda ni moja kati ya viongozi wabovu kwenye utawala huu.
 
Mkuu ni sahihi sana tu. Ulitaka tuendelee na utaratibu ule ule wa kuishi kirasimu?.

Mkuu kuna watu wananyanyasika sana, kama wewe sio mmojawao tambua kuwa wapo wengi.

Dhuluma mbaya sana imefanyika nchini mwetu kwenye masuala haswa ya ardhi. Ilikuwa ni lazima maamuzi ya kijasiri yafanyike.
Uwhiiu.
 
Sohwa ndio Tanzania ilipofika.
Unaweza kunya mavi mengi halafu ukasema ni pilau na utapata watu wa kukuunga mkono.
Jamani,hivi huyu makondra amewapa nini wakuu wake mpaka waweze kumvumilia hivi??hii siyo kawaida jamani,!
 
Jamani,hivi huyu makondra amewapa nini wakuu wake mpaka waweze kumvumilia hivi??hii siyo kawaida jamani,!
Nadhani kuna haja ya kufanya uchunguzi kwenye hili jambo. Nakuahidi kuweka uzi hapa ndani ya masaa 24 kuchunguza kamba aliyoshikilia huyu bwana.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom