RAIS MAGUFULI, MKUCHIKA IWAJIBISHE WIZARA TAMISEMI-UTUMISHI TAIFA na MIKOANI.

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,099
34,045
Habari,

Kwako Mheshimiwa Rais wa JMT na Waziri wa Utumishi. Ninaomba kueleza changamoto kubwa ambayo baadhi ya wilaya na mikoa inazembea sana katika kulishughulikia au kulimaliza kabisa.

Tatizo au Changamoto hii inawakumba watumishi wa serikali ambao kwa namna moja au nyingine waliondolewa katika Payroll aidha kimakosa au kwa kutokuwepo wakati wa uhakiki wa vyeti kwasababu za msingi.

Baadhi ya wilaya za mkoa wa KIKIMANJARO na baadhi ya wilaya zingine zina watumishi walioondolewa katika Payroll kwa muda mrefu sana na baadae wakawekwa chini ya uangalizi kuprove kama wanahudhuria katika vituo vyao vya kazi kila iitwapo leo.

Watumishi hawa wapo makazini na taarufa zao zimeenda wilayani na hata mkoani na zaidi tayari walishahakikiwa vyeti vyao na kuonekana kuwa havina shida kabisa lakini mpaka leo hii wameendelea kupata shida na taabu za kufanya kazi pasipo kupata mishahara kabisa.

Baada ya ufuatiliaji wa tangu Mwaka jana kinachoonekana ni UZEMBE uliopo kwa Maafisa Utumishi kwani kila wanapofuatwa na kuulizwa kuhusu suala hili aidha wanakuwa nje ya ofisi ama wakifuatwa ndio wanakuwa wanaanza tena mwanzo kukumbuka kushughulikia jambo hili kana kwamba hawakuwa makini kulifuatilia.

Mara nyingi wamekuwa wanatoa kauli za kukatisha tamaa na kutojali SHIDA, ADHA na MATESO tunayopata Watumishi na ni kama wametengeneza Network kwa makusudi haya.

Mh. Waziri George Mkuchika mimi ni muhanga katika hili na tayari tulishaandika barua kadhaa kwa Katibu Mkuu Utumishi na TAMISEMI ila jambo hili halijashughulikiwa tangu Mwaka jana.

Tunaomba sana Uongozi uangalie na ikiwezekana uchukue hatua juu ya Maafisa Utumishi wa Wilaya na Mikoa wanaozembea suala hili bila kujali adha wanayopata watumishi wenzao.

Maafisa Utumishi hawa wanafahamika kwa majina na yatakapohitajika majina yao tutakuwa radhi kuyataja popote endapo hatutaingizwa katika Payroll kwa mwezi huu kwani hakuna sababu ya msingi ya kutowekwa katika payroll ilihali tunaendelea na kazi.


Tunashukuru.
 
Ni kweli hii changamoto nimeisikia kwa walimu wawili wa shule x wakilalama juu ya kadhia hii. Niliwashauri waende mahakamani kuishtaki halmashauri iliyomuajiri pamoja na wizara mbili za utumishi na hazina ili watendewe haki! Na tayari wamefanya hivyo na kwa jinsi mwenendo ulivyo watalipwa pesa ndefu sana! Nawe nenda mahakamani ukadai riba na usumbufu!
 
Nashukuru sana kwa ushauri. Tulikuwa tunafikiria na wenzetu kufanya hivyo mkuu.
Ni kweli hii changamoto nimeisikia kwa walimu wawili wa shule x wakilalama juu ya kadhia hii. Niliwashauri waende mahakamani kuishtaki halmashauri iliyomuajiri pamoja na wizara mbili za utumishi na hazina ili watendewe haki! Na tayari wamefanya hivyo na kwa jinsi mwenendo ulivyo watalipwa pesa ndefu sana! Nawe nenda mahakamani ukadai riba na usumbufu!
 
Back
Top Bottom