Rais Magufuli: Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako ndio mji wenye nyumba na Makazi bora Tanzania

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Leo tarehe 11 April 2019,Akiwa mji wa Makambako mheshimiwa Rais amekiri wazi kuwa hajawahi ona mji Tanzania uliopangwa na kuwa na nyumba bora za Makazi kama Mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Ameomba mawaziri wakawaelimisha maeneo wanayotoka sehemu ya kujifunza nyumba bora ni Njombe

Yeye binafsi amekiri mkoa wake na mikoa mingi Tanzania hawaufikii mji wa Makambako

Ameshauri watu wakajifunze mkoa wa Njombe hasa mji wa Makambako

Hongereni Makambako
 
Makambako pale kwenye vibanda vya ulanzi na madanguro?

Kwa hiyo Makambako pamejengeka vuzuri kuliko Dodoma na Mwanza?

Acheni utani!
Anaongelea nyumba bora, Dodoma kuna nyumba za nyasi na tembe,
Mkuu tukisema Dar kuna Makazi hovyo hatuongelei ofisi na magorofa ya Posta na kariakoo

Angalia Makazi ya sinza, buguruni, magomeni ni kama taka taka ambazo hazikupaswa watu kuishi,
 
Anaongelea nyumba bora, Dodoma kuna nyumba za nyasi na tembe,
Mkuu tukisema Dar kuna Makazi hovyo hatuongelei ofisi na magorofa ya Posta na kariakoo
Angalia Makazi ya sinza, buguruni, magomeni ni kama taka taka ambazo hazikupaswa watu kuishi,
Ninapafahamu Makambako vizuri. Kuna vibanda vya Mpesa, Mabanda ya mbao, gesti bubu, vibanda vya walevi, na maduka.
Nyumba za makazi zipo ila siyo bora kushinda za Buguruni wala Manzese, DSM.
Acheni kulinganisha Buguruni na mtaa wa Makambako
 
Ni ukweli usiopingika kwamba nyumba za mkoa wa Njombe hasa Wilaya za Njombe na Wanging'ombe ni bora kuliko maeneo mengine ya nchi. Tangu miaka ya 1980 vijijini vya Njombe nilikuwa havigawa ardhi ya kujenga kabla mwombaji hajaonyesha tanuri la matofali ya kuchoma. Ndiyo maana hakuna tembe huko. Shida yao ni sakafu na bati tu.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom