Rais Magufuli, Mkiti CCM Taifa, Waziri wa Elimu na Tamisem Saba Saba Secondary, Mtwara kuna Tatizo

Kambamiti

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
291
165
Shule ya Sekondary Saba Saba ni shule ya kutwa iliyopo Mtwara Mjini. Shule hii ni moja ya kati shule Kongwe, Tanzania. Yafuatayo ni matatizo yaliyopo
1. Nyumba za walimu zinakaliwa na makada wa CCM. Wakati serikali inasisitiza kujenga nyumba za walimu, CCM wao wanang'ang'ania kuweka watendaji wa chama katika nyumba za shule.

2. Shule haina hati miliki ya ardhi. CCM wanadai ardhi ya shule ni mali ya chama. Hivyo, katika kufuatilia upatikanaji wa hati ya ardhi ya shule, shule imekwama kwakuwa CCM wanadai wao ndio wamiliki wa ardhi. Hapa wanapingana na agizo la serikali kuwa kila taasis ya serikali iwe na hati miliki ya ardhi.
3. Karibu na eneo la shule zimejaa garage nyingi ambazo zinasababisha usumbufu kwa wanafunzi.

Mwisho naomba mawaziri husika wafuatilie suala hili linaathiri utendaji wa shule.
 
Uko mbali mi nipo vigwaza hapa lakini shule yetu ina matatizo mpaka naona aibu kuyasema wao wamekazana na chunusi huko mjini
 
Uko mbali mi nipo vigwaza hapa lakini shule yetu ina matatizo mpaka naona aibu kuyasema wao wamekazana na chunusi huko mjini
Mkuu kama nimeona ukiyasema kwenye uzi mmojawapo hapa au siyo wewe. Kwamba kuna darasa moja na mwalimu mmoja akitumia usafiri wa pikipiki!
 
Mkuu kama nimeona ukiyasema kwenye uzi mmojawapo hapa au siyo wewe. Kwamba kuna darasa moja na mwalimu mmoja akitumia usafiri wa pikipiki!
sio mimi maana kwa ari ilivyo sina uhakika kama uyu ticha anauwezo wa kununua hata hiyo pikipiki
 
daah ! kweli bwana sabasaba mtwara imezidi kuna magereji kibao ,ya Akina MTAWA, LOLAND, Na nyingine nyingi watu wanakatiza katikat ya njia , kuna viwanja vya michezo ,havihudumiwi,walimu wanapanga mbali ili hali kuna nyumba nyingi,
 
Kuna kitu kinaitwa saba saba alumnae kazi yake ilikua kufatalia na kutoa suluhisho la matatizo ya hio shule huko Mtwara!! So far nini kinaendelea hadi shule igeuzwe garage? Shame on it though nimepitia hiyo shule pia
 
Back
Top Bottom