Rais Magufuli: Mimi sijaribiwi, wasije kunijaribu. Atakayeleta vurugu atashughulikiwa bila huruma!

Siasa ni ngumu kwelilweli

Gamba la nyoka,
Siasa wala siyo ngumu ila wanasiasa na mabolisi hasa walioko madarakani ndo wanaifanya siasa ionekana ngumu!
Katika hili la KUZUIA MAANDAMANO au KILA MBUNGE AFANYE MIKUTANO KWENYE JIMBO LAKE TU kulingana na maelekezo ya JPM mwenyewe limefanya siasa za Tanzania kuwa ngumu sana!
Hakuna kifungu/kipengele katika KATIBA kinachoelekeza kama Rais anavyotaka!!!
Kama Rais haongozi kwa kufuata Katiba na Sheria hakuna jina jingine litakalo mfaa zaidi ya kumwita "DIKTETA".
 
Hivi Rais ataitumbua lini hii Mimba ya Nape? Kijana mdogo alikuwa na mwili mdogo kama wa kike leo hii mtumbo huo kushinda hata wa marehemu Komba. Rais hii kitu itazame vizuri.
 
Wanao mpinga jpm na kuganya juhudi za kuvuruga mipanho kazi yale kwa yaiga hili ,hao hawapishani na sama na elshababu.kila siku kazi yao kuipinga serikali tuuuu,Jamani jpm naye alichaguliwa na watu wa taifa hili pia,sasa mbona hamuwatendri haki watz waliomchagua ,kwani hao wanao teyea haki ,je wanaishia wapi !?!mbona hawapiganii haki ya wale ambao walimchagua kiongozi wao,na sasa kiongozi wao hapewi nafasi ya kuwatumikia .ninyi mnaotetea haki mbona mko kimya hapo?'
 
Unataka kumlinganisha na mbowe au lowasa? Huyu ni mkuu wa nchi hapa yuko kazini hata akifanya siasa anatekeleza ilani ya chama chake, sasa mbowe akiitisha mkutano wa hadhara anatekeleza ilani gani wakat ikulu anapaskia kwenye radio na magazetini
Umeandika upuuzi,nani amekwambia ilani inatekelezwa kwenye majukwaa ya siasa?Shame
 
Yeye ni mbunge wa taifa zima,mfio sababu anaenda kote.na bado amesema hazuii mbunge kwenda kufanya kazi keenye jimbo lake la Hai.nenda kafanye huko .
 
1469824287961.jpg
 
Magufuli huyu hata walinzi wake muda si mrefu watamchoka...ni suala la muda tu!
 
Anajidanganya... Yatamtokea puani asubiri mziki wake... Magufuli sio mungu, huwezi kuwafunga midomo watu... Mikutano ya hadhara ni sehemu ya kazi za kila siku za siasa
Uko sahihi kabisa mkuu ukiwazuia kufanya siasa wakati ndo kazi zao unataka wafanye nini? Juzi mbunge wa Karatu ameitwa polisi kuhojiwa kwa sababu amefanya mkutano wa hadhara jimboni kwake kusikiliza kero za wananchi wake bado kuna nyumbu wanasifia huu upuuzi
 
Iliyokatazwa ni mikutano ya adhara, tena ya uchochezi, hata ccm chama dola hawafanyi mikutano. Mikutano ya ndani haijakatazwa, hata chadema walifanya mikutano minne mfululizo na kutoa matamko yao,
Bungeni walifunga pempers mdomoni, wakamkimbia NS,
Iyo anayoenda kufanya kahama ni ya ndan mkuu
 
Katika kujibu mapigo ya wenzetu wanaokuja na operation sijui ya nini, Rais kasema yeye hajaribiwi. Na kamwe mtu yoyote asithubutu kumjaribu. Huu ni muda wa kazi, hivyo tuwaache wananchi wachape kazi..

Mytake: Hii safi sana. Kama wapinzani na makundi ya kijamii yalizoea kuifanyia dola majaribio this time hakuna kitu kama hicho.

Ushauri wangu:
Jamani tusomeni alama za nyakati. Uongozi huu hauhitaji siasa zisizo na tija. Huu ni muda wa kazi..


.....Happening Now... Manyoni....

View attachment 372953
MSITUTISHE NA MSIFIKILIE TUNATISHIKA NA MAIGIZO YA CCM,,,,,WATUUE TUFE MAANA HATA YY ATATOKA TU KWENY URAIS NA ATAKUFA,,,,,MNATAKA TUMWONE BINADAMU KAMA MUNGU TUUUUUU KILA WAKATI,,,,Kumbukeni kabla ya yy kuwa rais tulikwepo na ataondoka na kutiuacha.....01/09 kama kawaida ni UKUTA
 
Magufuli ni Mwokozi asema mwanasiasa Dovutwa kwa mujibu wa gazeti la uhuru.Haya maneno yana ujumbe MZITO SANA hasa unapolitafakari kwa KINA neno la Mungu na lapendeza sana kutamkwa na mkongwe kama Dovutwa,Haleluya.

amekatiwa kitu kadogo , ( kama kipo tena) ???
 
hii ni kadri ya katiba au kadri ya Magufuli?

Inabidi ifike wakati tumwogope Mungu

huyu bwana aliapa kuilinda katiba

Nirejee maneno ya Rais mstahafu Njomba Ben Nkapa kwamba Watanzania wengi ni wavivu wa kufikiri! Mtu ambaye hana uvivu wa kufikiri anayechemsha Bongo kufikiri,kuwaza,kutafakari na hatimaye kutoa ufumbuzi wa tatizo HAWEZI KUKUBALIANA NA KAULI AU SEMI ZA JPM zenye kuleta ukakasi na kuhatarisha Amani ya nchi hii!!!
Hivi kati ya Rais Magufuli na UKAWA nani anayechochea vurugu???
Rais aliapa kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT lakini ajabu yeye amekuwa wa kwanza kuivunja!
Anacholazimisha Magufuli ni kuwagawa Watanzania KIMAJIMBO, KIVYAMA na KIITIKADI!
Unapolazimisha mbunge wa CCM afanye siasa jimboni kwake tu na wa CHADEMA, wa CUF,wa ACT Wazalendo,NCCR Mageuzi maana yake Wananchi wa maeneo hayo hutaki wasikie sera za vyama vingine kitu ambacho si sahihi! Magufuli anataka mpaka kufikia 2020 Tanzania itakuwa vipandevipande!!!!
Wako wapi watu wa kupiga kelele kupinga upuuzi huu? Watu wa media mko wapi kukemea uovu huu?????
 
Ifike mahali kila mwananchi wamgawie passport yake ili mda wowote ahame hii nchi.
Baada ya miaka mitano turudi.!
 
Kwa kauli hii ni dhahiri mikutano wala maandamano hayajakatazwa ila tu ifanywe na Mbunge au diwani wa eneo husika, siyo mbunge wa eneo X kufanya mambo hayo katika eneo Y.
Japo nimeelewa hivyo bado sijafahamu mustakbali wa vyama visivyo na mbunge au diwani je wao mikutano yao ya hadhara wataifanyaje?
Ikawaje sasa wale wabunge wa Karatu wakakamatwa ?! na kushtakiwa Arusha ?!
 
Back
Top Bottom