Rais Magufuli mikopo elimu ya juu bado giza nene

Smkwawa

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
651
964
Anaandika.

Abdul Nondo.

Magazeti mengi,vyombo vya habari vimeandika,na watu wengi wamekuwa wakiandika baada ya kauli ya Mh.Rais juu ya kuidhinisha sh.bil 147 kwa mikopo elimu ya juu.

Ila watu wengu walikuwa wakishangilia bila jua kuwa hali ipo namna gani ,twende wote:

Bajeti iliopitishwa na bunge wizara ya elimu ikiwa na bajeti ya wanafunzi elimu ya juu mwaka huu ni sh.bil.427 (2017-2018).kwa wanafunzi mwaka wa kwanza ,wa pili ,watatu na wanne.kati ya hizo bil.427 bodi ili Fanya portion (fungu) la bil 108.8 kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambapo idadi iliyotengwa kutokana na kiasi cha fedha kuwa kidogo ni wanafunzi elf.30 tuu wa mwaka wa kwanza .ndio maana unaweza pata jibu kuwa idadi ya wanafunzi elf 30 kupata mkopo ilitangazwa hata kabla ya wanafunzi kuomba mkopo.

Na bodi wana kiri kuwa kati ya wanafunzi elf 61 sio elf 30 tuu ,ndio wanasifa LA hasha ,bali uhaba wa bajeti yao.

Sasa tuje katika kauli ya Raisi ya Jana kusema ameidhinisha sh.bil.147 mikopo ya juu, ni kweli Mh.Rais ameidhinisha hiyo bil.147 tangu tarehe 29 sep.2017 kwa taarifa nilizozipata ,ila sio ongezeko ni idhinisho la fedha ndani ya bajeti ile ya Bil.427 ,hivyo kiasi hiki sh.bil 147 ndio kimetoka serikali kuu ila kipo ndani ya bajeti ya bil.427,ya mikopo elimu ya juu.

Kiasi bil 427- bil 147 =280 bil.hiki kiasi cha Bil.280 ndicho bodi wameachiwa walipe ,kwa taarifa za ndani fedha za bodi makusanyo haziendi hazina ,zinabaki katika Akaunt ya bodi (EXIM BANK) Bodi wanajumuisha bil.147 iliyoidhinishwa na Rais na ile ya makusanyo ya bodi ambayo wanayo katika akaunt yao watachukua bil .280 kuongezea ,hivyo bil.147+bil.280 ya fedha kutoka mfuko wa bodi inakuwa bil.427 ya bajeti iliotengwa.

Hoja yetu nini?

Hoja yetu ni kuwa tulitegemea ufanisi,fedha kutoka serikali kuu kwenda bodi ,imepungua kwa kiasi kikubwa ,yaani mzigo wrote wameachiwa bodi ya mikopo ,serikali kuu imepunguza kiwango cha kuchangia Mikopo elimu ya juu,sababu tuu ya kuona makusanyo ya bodi .makusanyo ya bodi bado hayakidhi kuhudumia mikopo ya wanafunzi elimu ya juu,serikali kuu imeanza kujitoa kuidhinisha fedha kwenda bodi ,matokeo yake serikali inaidhinisha fedha kidogo saana ,alafu ujazo wote wa bajeti ya mikopo elimu ya juu inaachiwa bodi ya mikopo.

Miaka yote serikali kuu ndio imekuwa ikitoa fedha nyingi zaidi kwa ajili ya mikopo elimu ya juu,Takribani bil 300 hadi 400 zimekuwa zikitolewa na serikali kuu ,ambapo kama serikali kuu ingeendelea kutoa kama ambavyo imekuwa ikitoa miaka yote ,alafu tukajumuisha na makusanyo ya bodi tungekuwa na bajeti kubwa takriban bil.580 ,ingetosha kabisa kutatua tatizo la mikopo elimu ya juu.hii inafanyika Kenya Higher education loans board ,inapewa fedha yote kama ilivyotengwa na bunge ,na hutumia tena mapato yao ya makusanyo hujumuisha na kuwapa wanafunzi.

Sisi Tanzania, tunafanya Compensation (fidia) bajeti ya mikopo inatengwa kidogo,serikali inatoa kiasi kidogo ,bajeti yote inamaliziwa na bodi .

kitendo cha serikali kuu kuachia mzigo wote bodi ya mikopo na yenyewe kulipa kidogo,haileti ufanisi ,kwani itapelekea wanafunzi wengi kukosa mkopo na hivyo wengi kuhairisha masomo.

Sera ya elimu ,ya 2014 ,sehemu ya 3.3.2 ya tamko ,"serikali itaondoa vikwazo vinavyozuia fursa ya wanafunzi kuendelea na kukamilisha mzunguko wa elimu katika ngazi husika" kwa namna tuendavyo vikwazo kwa wanafunzi havitaondoka wanafunzi wengi watarudi nyumbani.

Mwalimu Kambarage J Nyerere "in education we don't have retrenchment but we have investment" we sow what we shall reap tomorrow.we shall have doctors,teachers,presidents,MPs and economists.

Katika elimu hakuna ubana matumizi ila uwekezaji ,tunapanda tutakachovuna kesho,madaktari,walimu,maraisi,wabunge na wanauchumi.

Ombi ,tunamuomba Mh.Rais ,kwa jitihada zake,tunaomba asaidie wanafunzi wafikie ndoto zao,bajeti iliotengwa ni ndogo SAA hivyo sh.bil.427 na hiki kiasi Mh.Rais ulichoidhinisha tunakuomba uongeze kidogo ,kwani kiasi kutoka serikali kuu kwenda bodi kiasi ,kimepungua saana sh.bil 147 ,tunakuomba Mh.Rais ,uwaone wanafunzi hawa ambapo wengi walioomba wanasifa waliomba elf 61 wametengwa elf 30 ,tuuu .Mh.Rais we we ni mzazi pia ,waongezee bajeti kidogo kuziba gap ili wanafunzi wengi wenyesifa wapate ila sasa hata yatima wameachwa.

Sababu bajeti haiotoshi Mh.Rais,liangalie hili.,uwasaidie hawa wanafunzi ambapo ndio viongozi wetu,umewasomesha bure sekondari ila chuo umekumbana kikwazo kitakachoziba ndoto zao.

Shukran.

Abdul Nondo.
0659366125
Abdulnondo10@gmail.com



FB_IMG_15090867462570682.jpg
 
Tusipowekeza vya kutosha kwenye elimu tusitegemee tija huko mbeleni-tutakua na upungufu wa wataalamu. Issue ya access to higher education nchini Tanzania inaelekea serikali haija ivalia njuga. Kutoka udahili hadi utoaji wa mikopo-serikali inatafuta sababu ya kupunguza access to higher education. Role ya vyuo binafsi secondary na universities nayo ni matatizo. Kama alivyosema mleta mada nimemsikia waziri wa kenya akisema mwaka wa jana kila aliyefaulu wamehakikisha anapata chuo. Tujitafakari na kujisahihisha. We have to invest today for tomorrow. Tony Blair alisema yeye:Elimu, Elimu, na Elimu kuwa ndo vipau vyake vitatu vikubwa. Tuamke zaidi.
 
Alishasema 40% ya budget yake ni mambo ya maendeleo ( miradi kama ujenzi wa barabara) ingine mishahara na upuuzi flani
 
Bado jamaa anasema ana hela nyingi. Inchi ni tajiri lazima inunue ndege kwa cash.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom