comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Wana JF
Salaam
Mara zote katika kutoa amri fulani hasa yenye uelekeo wa kuingilia vyanzo vya mapato ni lazima kwanza tathimini ifanyike kwanza ili kujua madhara yake, hivi juzi juzi Waziri ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira Mh January Makamba ametoa amri ya kuondoa pombe za viroba sokoni bila hata kufanya tathimini ya athari za kimapato kwa muda mrefu, aidha lilikua ni agizo zuri kwa lengo la mazingira lakini ni agizo baya sana kwenye suala la mapato, kama inavyojulikana moja ya chanzo kikubwa cha mapato ni vinywaji vikali, Vilevile alitakiwa kwanza kutoa zuio kuingiza nchini wala kutengeneza pombe zenye vifungio vya mifuko ya nailoni maarufu kama Viroba nchini, pia angetoa tangazo la ukomo wa muda wa kuuza viroba kwa wale waliokua na hifadhi kubwa ya shehena za vinywaji hivyo.
Agizo lake la haraka bila kupima athari za kiuchumi nchini linaanza kuleta athari katika familia nyingi mfano tumesikia mfanyabiashara maarufu kujiua kwa kujipiga risasi pale Dodoma, ikumbukwe kwamba katika tukio lile athari zake zitakwenda mpaka kwenye mabenki kushindwa kupata marejesho ya mikopo yaliowapa wafanyabiashara.