Rais Magufuli - Mema Yake Hayaonekani?

Nakubaliana nawe 100%.

Ukweli ni kuwa kama tutamsema vibaya Rais kwa kila jambo, jema na baya, hata yeye hawezi kujua abadilike wapi maana lolote alifanyalo ni baya. Ataamua kufanya chochote kwa sababu anajua atalaumiwa tu.

Mazuri tuyakiri. Mabaya aliyoyafanya kwa dhamira njema, tuyatambue. Na yale tunayoyaona ni mabaya tuyaseme, tulalamike na kuyakataa. Kuyakataa yote siyo sahihi, na itamwondolea Rais moyo wa usikivu.
Kwa siasa ya saizi ni vigumu haya unayosema yatokee. Team kusifia kila kitu wako busy kutafuta chochote cha kusifia na team kuponda kila kitu nao Hivyo Hivyo. So ukiona watu wanaponda au kusifia kila kitu, we Angalia kilicho sahihi na fanya kwa sehem yako.Kingine jua kuna watu wako kazini ktk kusifia au kuponda kila kitu na kuanzisha mada mbalimbali.
 
Wasiojulikani ni pamoja na unayemsifia, unapowalaani wasiojulikana unamlaani pia na unaemsifia,pamoja na kwamba kichwani kwako unafikri kuwa unamsifia na kuwalaani wasiojulikana,lakini ukaeukijua kuwa bila kuwepo unaemsifia wasiojulikana hawapo.
 
Wewe jiunge, lakini mawazo huru ya wananchi yaheshimiwe. Wasiojulikana hatuwahitaji. Police wafanye kazi zao kuwakamata wahalifu
Odhiambo cairo, yawezekana hukunielewa, mimi sijiungi nao juzi, leo wala kesho na sidhani kama naweza kujiunga na kundi linalotanguliza maendeleo mbele ya haki ya kuishi. Huu msimamo wangu hauyumbi wala hautayumba kama wasiojulikana wataendelea kudaiwa hawajulikani na watu wanaowatuma.

Siamini ili tupate maendeleo lazima Ben Saanane (RIP!) apotezwe, siamini ili tupate maendeleo Mh. Tundu Antiphas Lissu lazima amiminiwe risasi, siamini ili tupate maendeleo Wananchi waokotwe kwenye viroba, na siamini ili tupate maendeleo tuwe na watu katika ngazi yoyote ile walio juu ya Katiba.

Katika awamu hii wasiojulikana wanawezeshwa kufanya wanayofanya na ndio maana wa kwanza kabisa kuwataja walikuwa ni vyombo vyetu vya Usalama. Wasiojulikana wanatekeleza tu gizani visivyoweza kutekelezwa na vyombo rasmi vinavyojulikana hadharani. Wasiojulikana wana baraka zote za awamu hii, period.
 
Mabaya yakizidi mema hata kama yale mema machache ni mazuri kiasi gani maana yake huondoshwa na yale mabaya yaliyokithiri.

Halafu hakuna jambo linalonikera awamu hii kama kulazimishwa kuyaona mema ya Rais, yeye afanye wajibu wake sisi tunaona hata bila kuambiwa.

Nakupongeza sana...

Umeandika kwa aya moja na mistari michache ya sentensi, lakini ujumbe wake ni mkubwa na kujibu insha yote ya mleta mada!!

Congratulation once again.....
 
Nakupongeza sana...

Umeandika kwa aya moja na mistari michache ya sentensi, lakini ujumbe wake ni mkubwa na kujibu insha yote ya mleta mada!!

Congratulation once again.....

I’m humbled
 
Odhiambo cairo, yawezekana hukunielewa, mimi sijiungi nao juzi, leo wala kesho na sidhani kama naweza kujiunga na kundi linalotanguliza maendeleo mbele ya haki ya kuishi. Huu msimamo wangu hauyumbi wala hautayumba kama wasiojulikana wataendelea kudaiwa hawajulikani na watu wanaowatuma.

Siamini ili tupate maendeleo lazima Ben Saanane (RIP!) apotezwe, siamini ili tupate maendeleo Mh. Tundu Antiphas Lissu lazima amiminiwe risasi, siamini ili tupate maendeleo Wananchi waokotwe kwenye viroba, na siamini ili tupate maendeleo tuwe na watu katika ngazi yoyote ile walio juu ya Katiba.

Katika awamu hii wasiojulikana wanawezeshwa kufanya wanayofanya na ndio maana wa kwanza kabisa kuwataja walikuwa ni vyombo vyetu vya Usalama. Wasiojulikana wanatekeleza tu gizani visivyoweza kutekelezwa na vyombo rasmi vinavyojulikana hadharani. Wasiojulikana wana baraka zote za awamu hii, period.
Walianza na Alphonse Mawazo (RIP) na mazishi hawakutaka yafanyike
 
Hata Afrika Kusini enzi zile za makaburu ilijenga miundo mbinu mingi tu, kuizidi nchi yoyote barani Afrika, lakini nchi hiyo ilitengwa na dunia nzima kutokana na tabia zake za ubaguzi......

Hivi Afrika Kusini ya enzi ile ina tofaiti gani na TZ yetu ya sasa??

Hapa TZ ya sasa kuwa mpinzani inaonekana kama mhaini!

Kupotezwa na watu wasiojulikana, kubambikiwa kesi za kuhujumu uchumi na maisha waliyoyazoea hawa wapinzani wetu wa nchi hii

Kila mtanzania anapaswa kwa sasa kukemea kwa nguvu zake zote mtindo huu wa utawala wa serikali ya awamu ya tano, kwa kuwa watanzania kwa sasa tumetia doa kubwa sana huko duniani, kutokana na mtindo huu ulioanzishwa na viongozi wa awamu ya tano, ya kutotaka kufuata misingi ya haki za kibinadamu na kuisigina Katiba ya nchi
Nimekuelewa
 
Ni kama ulikuwa unasubiri taarifa ya deni iwekwe hewani ili uiunganishe na suala la wasiojulikana.
Suala hapa ni kwa nini watu wafurahie ndege yetu kukamatwa nje ya nchi? Sababu kubwa ni yale mabaya yanayotendekea nchini ndiyo yanayofanya watu wasione hata uzuri wa yale mazuri.

Sisi wengine tunaona kuwa si vema kuyaona yote mabaya kwa sababu tu kuna mabaya. Mabaya kama haya ya wasiojulikana, japo yanatia kinyaa, ysituzuie kuyaona yaliyo mema. Hiyo ndiyo hoja ya msingi.
 
Pole ndugu yangu, kila kitu kina mwanzo. Wako wengi kama wewe waliokutangulia, hawakuwahi kuwa wapambe wa Rais, CCM au serikali ila when things got tough, their toughness couldn't withstand the test na kwa sasa wao in wapambe wakubwa wa Rais, CCM an serikali. Walikuwepo kabla yako na watakuwepo baada yako...wapo waliozawadiwa na wapo wanaosubiria kuzawadiwa na orodha in ndefu. Karibu, join the team!
Hata huko kukerwa na yanayoendelea katika awamu hii kama ya Wasiojulikana yana mwanzo na mwisho. Wapo waliokerwa labda hata kukuzidi wewe ila when things got tough, their toughness couldn't withstand the test na sasa hawakerwi tena. Walikuwepo kabla yako na watakuwepo baada yako...wapo waliozawadiwa na wapo wanaosubiria kuzawadiwa na orodha in ndefu. Karibu, join the team!

Bams
labda na mimi niko njiani...siku yangu ya kuwasaliti raia wema wa taifa hili wanaodai utawala wa haki unaozingatia sheria na unaoheshimu Katiba haiko mbali! Labda when things get tough, my toughness won't withstand the test na bila shaka nitaunga mkono kuteswa kwa ndugu zangu, rafiki zangu, jirani zangu na Watanzania wenzangu, kwa kudai tu haki ya kuishi salama kama Katiba yetu inavyoelekeza. May be I too will join the team!

Who knows! Maybe my shadow knows best! But the truth still remains that when the going gets tough, only the tough keep going. Kwa nafsi yangu, utu, haki na uhuru ndizo zinatutofautisha na viumbe vingine duniani na kwa binadamu ndizo nguzo kuu za maisha kama ulivyo msingi wa nyumba. Bahati nzuri hizi zimeorodheshwa kwenye Katiba na hivyo Katiba ikishakiukwa, maendeleo yoyote yale hayana maana!
Nashukuru kwa maoni yako.

Siku nitakapounga mkono unyanyasaji, utekaji watu, upotezwaji watu, mauaji ya watu, watu kutengenezewa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, na mengine yanayofanana na hayo, NINA HAKIKA SITAKUWA MIMI, HAITAKUWA NAFSI YANGU BALI MWILI WANGU UTAKUWA UMEVAA ROHO YA SHETANI.
 
Hata mkoloni alijenga miundombinu ikiwemo reli na kadhlika na tulidai uhuru kwasababu uhuru na haki za binadamu ni muhimu kuliko hayo mareli na madege.
 
Suala hapa ni kwa nini watu wafurahie ndege yetu kukamatwa nje ya nchi? Sababu kubwa ni yale mabaya yanayotendekea nchini ndiyo yanayofanya watu wasione hata uzuri wa yale mazuri.

Sisi wengine tunaona kuwa si vema kuyaona yote mabaya kwa sababu tu kuna mabaya. Mabaya kama haya ya wasiojulikana, japo yanatia kinyaa, ysituzuie kuyaona yaliyo mema. Hiyo ndiyo hoja ya msingi.
Kabla ya haya ya wasiojulikana hayajaanza, hao wanaochukia serikali walikuwa na sababu nyingine nyingi tu za kuichukia.

Leo wanaitwa wasiojulikana lakini kumbuka haya mambo yamekuwa tangu enzi za awamu ya kwanza, sio mambo mazuri lakini yamekuwepo.

JPM anachukiwa kwa mengi, kaziba mirija myepesi ya upigaji iliyokuwa imezoeleka. Kero kubwa zaidi ni kulishambulia kabila lake hadharani tena moja kwa moja.

Makabila ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete yalikuwa hayashambuliwi, ni jambo fulani lenye uwezo wa kuleta mpasuko mkubwa huko tuendako, Mungu apishie mbali.
 
Mimi naanza kwa kukunukuu, "Siwasemei wengine, lakini mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la ndege lenye ndege na linalotoa usafiri wa anga wa uhakika, ulikuwa ni uamuzi mzuri."

Hata mimi nakubaliana na wewe kuhusu kuwa na shirika letu la ndege linafanya kazi lakini sikubaliani na namna uamuzi huu ulivogubikwa na mambo ya kisiasa na sio kwa manufaa ya walipa kodi na wananchi wote kwa ujumla. Kuna haja gani ya kudanganya kwamba shirika linaingiza faida?
 
Sijawahi kuwa mpambe wa Rais, CCM au Serikali. Kati ya mambo yaliyonikera na yanayoendelea kunikera katika awamu hii ni hawa Wasiojulikana. Hawa kazi yao ni kuteka, kutesa, kuua, kuwaonea na kuwatengenezea watu kesi bandia na kupoteza watu. Huu ni unyama wa hali ya juu usiostahili kuwepo katika jamii iliyostarabika na inayotambua maana ya utu wa mwanadamu. Hawa wanaturudisha kwenye primitivity. Hawa wameleta chuki kubwa miongoni mwa raia na raia dhidi ya Serikali.

Jana tumeambiwa ndege yetu imekamatwa kule South Afrika kwa amri ya mahakama. Mitandaoni kwa maoni ya wengi inaonesha kuna wengi waliofurahishwa na tukio hilo!

Mara kadhaa nimetumia ndege za ATCL ndani na nje ya nchi. Kuna mema mengi kuiona ndege ya Tanzania nje ya nchi, nawe unaenda kupanda ndege ya nchi yako, tena ndege iliyo nzuri. Unapanda na kwenda moja kwa moja nchini kwako, siyo safari yako ni kwenda Dar, lakini kwanza unazungushwa mpaka Addis Ababa au Nairobi. Unapopanda ndege ya nchi yako, na unaenda moja jwa mojga nchini kwako, unaokoa muda, unatengeneza soko la ajira na bidhaa kwa wananchi wenzako, unatangaza taifa lako na kuna ile proud ya nchi yako pia.

Siwasemei wengine, lakini mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la ndege lenye ndege na linalotoa usafiri wa anga wa uhakika, ulikuwa ni uamuzi mzuri. Mimi ni kati ya wanaoamini kuwa uamuzi wa kuwa na shirika la reli lenye train za kisasa ni uamuzi sahihi. Mimi naamini tunahitaji usafiri wa majini ulio salama na wa uhakika. Tunahitaji umeme wa kutosha na wa uhakika. Hivi vitu ni vyetu Watanzania wote, siyo vya serikali, Rais au CCM pekee yao. Vinatumia hela yetu sote lakini ili vitendeke ni lazima Wananchi wote tunatakiwa kuwa na ownership ili tuvipende, tuvitunze, tuviboreshe, na tuvihuzunikie vinapokubwa na mikasa.

Kwenye ndege, reli, meli, umeme, nidhamu serikalini, matumizi ya fedha za umma, maamuzi ya haraka, n.k; naipongeza Serikali, nampongeza Rais na nawapongeza Wananchi wote.

Huyu Rais ni binadamu, aweza kufanya makosa, na wakati mwingine ni wakati anapodhamiria kufanya mema. Hilo linapotokea, tusitazame tu yale makosa bali tuitazame ile dhamira yake njema.

Yawezekana kutokana na mambo ya hovyo yanayofanywa na wasiojulikana, yakatufanya kuichukia awamu hii kwa kila jambo hata tukashindwa kuyaona yaliyo mema.

Lakini kwa hakika, kuna mambo ambayo Rais anayasimamia na yanafanyika, ni mambo sahihi. Tunaweza kumlaumu kwa baadhi ya mambo lakini kuna mambo ya msingi kwa Taifa letu anayoyasimamia, tunaweza kuyapuuza leo lakini kuna siku, huenda akiondoka madarakani au atakapoondoka Duniani, tutamkumbuka. Katika yale mema ambayo Rais anayafanya, Mungubayape baraka ili yakapate kuleta faida kwa Taifa letu. Na yale ya wasiojulikana na wasiojulikana, wakapate laana kuu wote wenye kuyatenda na kuyapanga.

Maadui wakubwa wa Taifa letu, kwa serikali, kwa CCM na kwetu wananchi wote, ni hawa Wanaojiita wasiojulikana. Hawa ndio wanaoondoa upendo miongoni mwa wananchi na wananchi walio wengi dhidi ya serikali na watawala.

Hawa wanajua Mbowe, Msigwa, Heche, Mdee, kila siku wanajua wamekula nini, wamelala na kuamka saa ngapi, wameongea na nani na muda gani, wamevaa nini, n.k. lakini hawana uwezo wa kujua ATCL imeshtakiwa, hawana uwezo wa kujua ndege itashikiliwa, hawana uwezo wa kujua korosho hazitauzika, hawana uwezo wa kujua mahindi yakizuiwa kuuzwa nje yatakosa soko, n.k. Hii inatupa ujumbe kuwa, hawa Wasiojulikana wanachokijua ni uovu na siyo kulisaidia Taifa kwa mambo ya msingi kama usalama wa kiuchumi.

Hivi kweli ATCL imeshindwa kuwa na makubaliano ya ulipaji wa madeni yake mpaka kufikia hatua ya kuchukuliwa ndege yetu? Pamoja na yote, ndege yetu kushikiliwa ndani ya nchi rafiki inasikitisha sana! Hawa akina Kabudi hawana diplomasia ya biashara na uchumi? Au wanachojua ni zile diplomasia za miaka ya 60 tu za hata mtu akijikwaa kwenye gogo aliloliwekwa mwenyewe anasema, 'unaona njama za mabeberu na wakoloni!'.

Hii inadhihirisha wazi ukweli ambao wengi wamekuwa wanausema, Rais hana watu sahihi kwa majukumu ya kitaifa. Mara nyingi watu wanaofanya kazi kubwa ya kumsifu boss wao ni wale wenye mapungifu makubwa kiuwezo na ni watu wasiojiamini.

Poleni Watanzania kwa hii aibu ya kidogo chetu kutaka kunyang'anywa.
Watu wasiojulikana wanatumwa na kulindwa na Nani ?
 
Nashukuru kwa maoni yako.

Siku nitakapounga mkono unyanyasaji, utekaji watu, upotezwaji watu, mauaji ya watu, watu kutengenezewa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha, na mengine yanayofanana na hayo, NINA HAKIKA SITAKUWA MIMI, HAITAKUWA NAFSI YANGU BALI MWILI WANGU UTAKUWA UMEVAA ROHO YA SHETANI.
Eenh, Bams Bhwanah, sasa linganisha hayo na ndege zetu... haiwezekani kwa njia yoyote ile!

Bams, achilia mbali kuweka mlinganisho wa mambo ya mavitu na uhuru/haki za watu.

Ngoja nikustue kidogo kwa mfano huu unaosikitisha, lakini ni mfano stahili. Hakuna Mzalendo wa kweli anayeweza kuvumilia kuona nchi yake ikinyanyasika, kwa mfano kuvamiwa na taifa lingine. Lakini si ajabu kuona watu wa taifa fulani wakishangilia nchi yao kuvamiwa kama utawala uliopo unafanya mambo ya kuwakandamiza wao.
Hakuna jambo baya na la kustua na kusikitisha kama hilo, lakini hutokea; na hapa sijasema nasi tumefika hatua hiyo. Kwa hiyo kushikiliwa kwa ndege kama wapo wanaoshangilia hilo, wachukulie katika mfano huo.
 
Back
Top Bottom