Rais Magufuli: Mbunge wa Vunjo mh Mbatia ndio mpinzani mwenye uzalendo

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,820
141,722
Rais Magufuli amempongeza mbunge wa Vunjo mh Mbatia ambaye ni mwenyekiti wa NCCR Mageuzi kwa namna anavyofuatilia suala la Corona na kuishauri serikali.

Rais Magufuli amesema mara kadhaa mh Mbatia amekuwa akimpigia simu na kumtumia Meseji za kumtia moyo katika haya mapambano.

Chanzo: Channel ten!
 
Mara corona haipo mara mnapigiana simu mnatiana amani,which is which kwanza hapa mtaani watu wamechanganyikiwa je corona ipo au haipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ya kuambiwa changanya na yako ila CORONA ipo na inaua chukua tahadhali

Ila kwenye hili kamati kuu itutake radh kwa mambo waliyofanya 2015 this is too much

Its not over until its over...
 
Mbatia hana haja ya kuhofia uchaguzi ujao, ashinde asishinde bungeni ataingia, ikiwezekana na uwaziri juu.

Gharama yake kujitoa ufaham tu.
 
Nguvu moja itikadi tuweke pembeni tujielekeze kupambana na adui COVID-19!!
 
Kuna wabunge wengine wamejifungia Ndani wanaogopa corona

Sisi wapiga kura wao tunakata mitaa kutafuta riziki
Kuna Rais tokea Corona imeingia ameenda kujificha Chato kijijini kwao alikozaliwa huku akiendelea kulamba posho za safari kama kawaida!
 
Wewe jifungie km wabunge wako walivyo jifungie

Sisi Watanzania tuliowengi tunamsikiliza Rais wetu
Za kuambiwa changanya na zako,mambieni arudi ikulu maisha yaendelee kama kawaida!Sio nyie pigeni kazi huku yeye kajificha!
 
Kwa vyovyote vile ule mwaliko wa kwenda Ikulu utakuwa umezaa matunda. Tayari Mh. Mbatia na wachumia tumbo wenzake, tutegemee kuwaona kwenye Bunge lijalo.

Kwa hali hii ya ubinafsi uliokithiri na uchumia tumbo unaowakabili wanasiasa nchini mwetu, tutasubiri sana kuiona Ccm ikitoka madarakani kupitia sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom