Rais Magufuli, mbona bia ya Balimi haina nembo ya TBS?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,099
8,727
Shikamoo popote uliko Mh. rais, mimi nakusalimia nikitokea Kinore hapa mkoani Morogoro!

Baada ya salamu ninakuuliza wewe rais na waziri mliofungia viroba na baada ya viroba watu wakaamia kwa haraka kwenye bia hiitwayo Balimi. Mbona haina nembo ya TBS na inauzwa bei ileile? Kwanini ulifungia viroba vyenye nembo ya TBS na sasa unaiacha hiii bia isiyo na nembo?

balimi.jpg


Au TBS nao wamekuwa kama wale wa madini tena? Wewe bia mpaka inafika hapa kinore bila nembo hii najua wewe ndo utakuwa umeamrisha maana tofauti na hapo inaonesha watendaji wako wanapokea mlungula.

Naomba jibu haraka Mh rais.!

Mimi bosi wako mkulima kutoka Kinore Moro sasa shambani kuvuna mpunga
 
Picha mkuu ili tukusaidie kupaza sauiti maana hiyo Balimi Busungu wengine hata hatujui ipoje!!

Au nayo ipo packed kwenye viroba!
 
Mdau tafuta kivuli ulale hapo hadi hangover ikuishe, pia uwe unakunywa jioni tu usiwe unakunywa kila wakati kwani sasa balimu zinakupa uwehu.
 
Kwa sasa huyu Magufuli alivyojificha u Mungumtu naona muda mfupi tu mtu atauliza "Rais Magufuli mbona mke wangu hanifulii chupi?"
 
Huko kwenu Kenya kwanza hauna uzalendo Sababu sisi wazalendo tunaitambua kinywaji bora kabisa cha watu wakaida BALIMI
Dah!!! mkuu ananinyang'anya uraia wangu kisa kutoijua BALIMI tu?

Tatizo sijui ladha vileo ndio maana inakuwa ngumu kwangu kujua majina yake. Ila hapo juu nimeona picha tu so huu uzi watu kama mimi ulikuwa hautifai kuchangia.
 
Back
Top Bottom