Rais Magufuli: Mawakili wanaowatetea wahalifu waliokutwa na ushahidi nao wawekwe rumande ili wakome

Rais John Magufuli aliyaongea hayo jana alipokuwa akiongea kwenye sherehe za uzinduzi wa mwaka mpya wa sheria, alisema kuna watu wanakutwa na ushahidi wa wazi kabisa lakini kuna mawakili wanaoenda kuwatetea, mawakili hao wanatakiwa kuwekwa rumande waonje joto ili hata wakitoka wajifunze kutokutetea wahalifu...



kuwa msikilizaji zaidi ya kuwa msemaji ni hekima iliyotukuka.

"Knowledge speaks, but wisdom listens" - haya ni maneno ya Jimi Hendrix (ambaye hakuwa kiongozi wa siasa, serekali wala dini bali mwanamuziki tu!)
 
Kukutwa na kithibiti haina maana ya kuwa wewe ndo mhusika, ingekuwa iko hivyo basi isingekuwa na ulazima wa kuwa na mawakili, kauli kama hiyo kutolewa na mtu kama huyo sidhani kama itakuwa ni haki
 
Mh JPM, bora awe anasoma hotuba za kuandikiwa, kila siku anavyoongea vya kichwani mwake, anazidi kujishushia heshima.
 
Mkuu alishasema ye hajabobea kwenye sheria kwa hiyo hajui kama hata jambazi wa red-handed naye ana haki ya kuwa na mwanasheria
 
Kubambikiwa kesi ipo sana, wengi wamefungwa kwa kesi za kutengeneza za uonevu na sasa kwa maneno ya mkulu wabambikaji kesi wataongezeka kinachofuata ni kuomba Mungu anakuwpusha na wabambikaji kesi vinginevyo magereza yatajaa wafungwa wasio na hatia bali kwa uonevu tu.
Kuna shida kubwa sana endapo mtu unashindwa kuwa na hata uwezo wa kufikiri pande zote katika jambo lolote mtu unafikiri upande mmoja tu na kutoa maamuzi na mtu wa hivyo unamapungufu makubwa sana ya uelewa wa mambo, maana ni lazima jambo lolote kabla ya kuliamua angalia madhara na faida kwanza na hilo wenye kuliweza ni wenye akili kubwa pekee, kama una akili ndogo itakuwa ni mwendo wa kukosea na kufanya marekebisho kila siku. Shida ipo kubwa sana.
 
Kazi ya Rais sio kusoma Mawazo ya Wasaidizi wake, Kazi ya Wasaidizi ni kuandika Mawazo ya Rais na ikitokea Wanayabadili acha amwagike Mubashara!

Miaka 50 iliyopita Ma Rais wamesoma sana Hotuba walizoandikiwa tuakalalamika zimejaa Siasa na Uongo Uongo Mwingi acheni afunguke Kipenzi cha Wanyonge!
Jitahidi ipo siku utakumbukwa kama watoa ukungu wengine.
 
Unatamani Ujinga na umesahau kama sheria ni msumeno walakotekote?! Haya matamko ya majukwaani kugeuka kuwa sheria punde si punde mtasema
Tamko la jukwaani si sheria.
Ukijidai ndo sheria lazima ile kwako.
Ukitaka kujua waulize waathirika wa ajali za barabarani baada ya tamko la Lowassa kurusu njia tatu..
Kuna watu kibao walinyukana uso kwa uso huko njia ya tatu (ambayo kupita ni kosa kwani kwa sheria za Tanzania tunatembelea upande wa kushoto).
Kuna baadhi hadi walifungwa jela kwa ajalo hizi kisa tu walidhani tamko la jukwaani ni sheria.

Leo hii mtu akiwafungulia polisi kesibya uharibifu wa mali, hachomoki mtu na atalipwa tu. Hakuna namna.
 
Sio kila mhalifu anatetewa ili awachwe huru wengine ni ili wapunguziwe adhabu
 
Nimecheka Sana. Ni wazo zuri ila mahakama na sheria, sio kile unachokijua lakini kile unachoweza kukitolea ushahidi mahakamani.
I'ts not what you know, It's what you can prove in court. That's how Legal system works.
:D
 
Ni kweli Mheshimiwa Rais kuna mawakili wengine wanajua kuwa mteja anayemwakilisha ana makosa lakini bado atachukua pesa na kudai kumwakilisha matokeo yake ataomba kila siku kesi ihahirishwe ili aendelee kuchukua pesa za mteja wake.
Ni muda muhimu kwa chama mawakili Tanzania kuwatumbua mawakili wasiokuwa waaminifu Mheshimiwa Rais Magufuli anachosema 100% ni kweli kabisa.
 
Back
Top Bottom