Rais Magufuli: Mawakili wanaowatetea wahalifu waliokutwa na ushahidi nao wawekwe rumande ili wakome

Umeshawahi kusingiziwa kesi hata ya KUBAKA tu ndugu yangu??Kama bado basi acha mara moja kushabikia upuuzi uliozungumzwa.

Kamuulize yule MFUNGWA aliyeswekwa ndani,kwa tuhuma za KUBAKA ambapo hadi leo hakuna anayeujua ukweli
kwahyo nayeye alinyimwa wakili au umesahau mada
 
Ifikie mahali kabla hujasema lolote kutoka kwa mtu, ni vyema ukamsikiliza na kumuelewa vyema
 
Mimi mtetezi na shabiki wake mkubwa ktk mambo mengi. Lakini kwa hili kakosea sana. Kila mtu anahaki ya kujitetea au kuweka mtetezi kwa niaba yake hadi pale mahakama inapothibitisha ni kweli ana hatia. Kuna watu wanakuwa wametengenezewa mazingira ya kuwa na hatia ya kutenda kosa lakini kiuhalisia hawakutenda kosa hilo. Au bahati mbaya mazingira yanamsababisha aonekane ametenda kosa kumbe sivyo. Tukianza kuwanyima watetezi watuhumiwa tutajikuta tunawafunga au kuwanyonga watu wema wengi tu.
mkuu inamaana hata yeye nyumba za serikali alizouza na kumhonga Sundi Malomo itabidi apelekwe mahakamani maana ndio uthibitisho ule haswaaa
 
Wakili hajakuonea maana wakili anatekeleza kazi yake kwa mujibu wa sheria na kumbuka mahakama siku zote inatoa uamuzi wake kulingana na ushahidi uliyotolewa,kinachofuatwa mahakamani ni sheria sio haki,haki itapatikana kwa muumba
kwahyo tunakubaliana kua hao mawakili hawana maana kuwepo mungu ndo muhimu
 
mkuu hayo yotee unayoyasema shida ni moja tu serikali haina mawakili nguli kupangua hoja hivyo raisi ameamua kuwasaidia kuingia kingi aibu ya aina yake ni mahakama tu ndio itamtia mtu hatiani na si matamko ya mtu kulazimisha.
Hajui kama kuna nchi nyingine hao wahalifu wanapewa mawakili na serikali na gharama inalipwa na serikali.
 
akili nyingine! hajui hata ukutwe unachinja mtu ni haki yako kuwa na wakili!
Bora amekuja kuongelea huku nyumbani huko ugenini angetutia aibu
Au nyie mnatumia jicho moja kuona, kila siku mnalaumu jeshi la polisi kuachia waalifu ss siku hizi mmeamua kuwauwa baada ya kusikia neno mwizi, huwa mnauhakika gani kuwa ni mwizi na kwann mchukue sheria mkononi?
 
Kwa njaa kali ya mawakili na vitendo vya rushwa vilivyotawala Afrika naunga mkono tamko la mkuu kwa asilimia kubwa...

'It's really frustrating when criminals are walking freely because they have ability to buy some people and continue with evils in the same communities" ......If you are defending them then it's you are duty to reform them and not allowing them to go to the streets with the same behaviors again...... Blot out the unneccessary vicious cycle
 
akili nyingine! hajui hata ukutwe unachinja mtu ni haki yako kuwa na wakili!
Bora amekuja kuongelea huku nyumbani huko ugenini angetutia aibu
Kwan ukikutwa unachinja mtu hata polisi utafika? Anyway, ukibahatisha kufika polisi ukiwa hai una haki ya kutetewa mahakamani na kama huna uwezo serikali itakupatia wakilo.

Kila mwenye akili anapaswa kupinga matamko hatarishi na yanayoashiria uvunjwaji wa katiba.
 
Back
Top Bottom