Rais Magufuli: Mawakili wanaowatetea wahalifu waliokutwa na ushahidi nao wawekwe rumande ili wakome

Jozi 1 hujanielewa bodaboda nilimaanisha pikipiki si dereva wa hiyo bodaboda. Sasa na uliza tena mbona hamkutetea bodaboda zilipohukumiwa kung'olewa matairi polisi? Hapa hukumu ya bodaboda ni nyingine na ya dereva wake ni nyingine.

Na washawasha!
Hujaona magari yaliyotolewa matairi.Yote Hapana haki.Mahakama ndiyo ingetoa hukumu na si polisi.Sababu polisi wanashindwa kutumia weledi wa taaluma yao wanajikuta kwenye kesi zinazokuja kuwabadilikia baadaye.

Imenikuta week jana nashushwa na gari ndogo polisi akaja mbio, bahati nzuri dereva akawa amekimbia na ni eneo ambao si rasmi kwa ajili ya Mwendokasi lakini polisi alitaka kutubambikia kesi.

Shida ya Haki za msingi za RAIA Polisi wana zinaenda kwa ajili ya kufurahisha watawala. Na Watanzania tusipokuwa na umoja tunafurahia sababu tu ya uwezo mdogo alionao Mtanzania mwenzetu.Ni shida sana .
 
Ni kweli Mheshimiwa Rais kuna mawakili wengine wanajua kuwa mteja anayemwakilisha ana makosa lakini bado atachukua pesa na kudai kumwakilisha matokeo yake ataomba kila siku kesi ihahirishwe ili aendelee kuchukua pesa za mteja wake.
Ni muda muhimu kwa chama mawakili Tanzania kuwatumbua mawakili wasiokuwa waaminifu Mheshimiwa Rais Magufuli anachosema 100% ni kweli kabisa.
Ninachofahamu mnapokubaluana na wakili Lazima mkubaliane na kiasi cha kulipa mpaka kesi iishe.
 
Na mfano ile mahakama ya mafisadi walijenga ya nini? Si wangeongeza magereza ili mtu akikamatwa apelekwe moja kwa moja gerezani?
 
Huyu mzee sina hakika kama anajua sheria na utaratibu wa utetezi
Mtu mwenye PHD ya kweli, Ungelitegemea awe na General knowledge ya Maswala Muhimu ya Kijamii. This Guy Ni Msomi feki. Wa Kukremu na Kununua Vyeti. Kwanza Kwa anavyojifanya anajua Kila Kitu ni Vigumu kuniambia alikuwa na uwezo wa akujifunza (He is an Autistic, and Sadist) Next time iwe mandatory kwa Mgombea Urais apimwe akili.
 
Rais John Magufuli aliyaongea hayo jana alipokuwa akiongea kwenye sherehe za uzinduzi wa mwaka mpya wa sheria, alisema kuna watu wanakutwa na ushahidi wa wazi kabisa lakini kuna mawakili wanaoenda kuwatetea, mawakili hao wanatakiwa kuwekwa rumande waonje joto ili hata wakitoka wajifunze kutokutetea wahalifu...



wala simlaumu, ulitegemea kusikia nini toka kwa mtu aliyesoma chemistry aongelee kitu kinachohusu mahakama? hapo ndio uelewa wake wote wa sheria anaamini hivyo, na ni fedheha kwa taifa kwamba mkuu wetu hajui misingi ya sheria nchini na inawezekana haheshimu misingi ya sheria. dunia nzima mtu huwa hahukumiwi adhabu bila kusikilizwa hata kama amefanya kosa. Hata Yesu walimpeleka mbele ya pilato kwanza kabla ya kumuua, haki ya kuwakilishwa na mwanasheria hata kama wewe ni muuaji ni ya kikatiba. amesahau kuwa serikali yake huwa inatoa hela kuwapa mawakili wa kujitegemea wawawakilishe watu wenye kesi za mauaji mahakama kuu, kwasababu ni lazima walipiwe wakili na serikali inafanya hivyo, hata kwa wale wauaji ambao ushahidi upo wazi kabisa, wanakuwa na wakili na wakili huyo analipwa na serikali. nashindwa kumuelewa mkuu.
 
wala simlaumu, ulitegemea kusikia nini toka kwa mtu aliyesoma chemistry aongelee kitu kinachohusu mahakama? hapo ndio uelewa wake wote wa sheria anaamini hivyo, na ni fedheha kwa taifa kwamba mkuu wetu hajui misingi ya sheria nchini na inawezekana haheshimu misingi ya sheria. dunia nzima mtu huwa hahukumiwi adhabu bila kusikilizwa hata kama amefanya kosa. Hata Yesu walimpeleka mbele ya pilato kwanza kabla ya kumuua, haki ya kuwakilishwa na mwanasheria hata kama wewe ni muuaji ni ya kikatiba. amesahau kuwa serikali yake huwa inatoa hela kuwapa mawakili wa kujitegemea wawawakilishe watu wenye kesi za mauaji mahakama kuu, kwasababu ni lazima walipiwe wakili na serikali inafanya hivyo, hata kwa wale wauaji ambao ushahidi upo wazi kabisa, wanakuwa na wakili na wakili huyo analipwa na serikali. nashindwa kumuelewa mkuu.

Chemistry my Foot, hata Furnace anaiita Finance!
 
Kama nyie mnaona ni mharifu mnampeleka mahakamani kufanya nini si mpeleke gerezani moja kwa moja
awalaumu polisi wake wanaokamata wahalifu na kuwapeleka mahakamani. kama hataki mawakili wawawakilishe, awape polisi wake amri ya kufanya mara tu wakiwakamata kama anafikiri hizo zitakuwa haki za binadamu. kuna watu wengi sana wanabambikwa kesi na kama ushahidi hautalewa mahakamani na kuwa challenged, wengi wanaweza kufungwa wakati hawakufanya kosa.
 
Wakati mwingine tumkubali Mh
Rais. MTU kafanya hatia hadharani halafu anatokea msomi anamtetea kwamba ana haki ya uovu alioufanya wewe unaona sawa kweli? Eti ndo utawala bora na sheria? Rudi kwa lowassa kachukue akili zako uwe RAIA mwema.
Kaka acha ushabiki kada mwenzangu..ili unayoyasema yalingane na Yale ya Mkuu ni vyema wapeleke bungeni wakabadili Katiba kwanza kisha sheria then yatekelezwe. Sheria yatamka everyone is innocent until proven guilty by court of law. Najua unachangamsha genge tu hauko serious katika hilo...na sio Nyumbu wewe maana hufuati mkumbo tuu.
 
ni kweli anayetetea mhalifu naye ni mhalif
wote wakae ndani
haujawahi kukamatwa na kupelekwa mahakamani wewe. kuna siku utakamatwa na kupelekwa mahakamani hayo unayoyaongea yatakutokea puani. nikupe mfano tu, kuna watu wanashikiliwa kwa miaka kadhaa hadi leo hii mahabusu kwa kesi za mauaji, lakini hawakuua, na kesi ya mauaji wakati wa usikilizwaji ni lazima mshitakiwa awakilishwe na wakili, mara nyingi serikali inatoa fungu kuwalipa mawakili wa kujitegemea wawawakilishe wahalifu ili hukumu itakapotolewa iwe ya haki. kuna watu wamekutwa tu na simu ya marehemu pengine waliinunua in good faith, marehemu yule amekufa kifo kisicho cha kawaida, mwenye simu anashikiliwa hadi leo hii, kuna watu wamebadilishiwa begi wakati wa kusafiri na begi lenye madawa ya kulevya, hadi uje ujulikane hayakuwa ya kwako, umeshasota sana gerezani, kuna watu walikuwa wameondoka na wapenzi wao kwenda kwenye sherehe, wameachana huko na hakuna anayejua waliachana kila mtu akaenda kwake, mmoja wao akauawa na majambazi huko lakini anayejulikana aliondoka naye ni huyo rafiki, rafiki anashikiliwa hadi leo gerezani kusubiri upelelezi. kuna kipindi kulikuwa na watu special kutunga ushahidi hasa kwenye kesi za armed robbery kuwakomesha baadhi ya watu(kuwa fix) wapo hata raia tu,....kuna watu wengine raia wa kawaida ukiwa na ugomvi naye wanakutungia zengwe la ajabu, nilishawahi kuwakilisha mtu kesi ya kubaka kumbe hajabaka kabisa wanagombania shamba, mwingine anaambiwa ameua kumbe hajaua kabisa wana ugomvi wa kiukoo wanakomeshana na wanaleta ushahidi wa uongo kabisa, bila wakili kuja kujua ni wa uongo umeshasota sana na unaweza kufungwa. sisi ni wanasheria, hatuna shida, ninyi raia mnaoshabikia hicho alichokisema rais wenu ndio mtaumia....yeye hataumia wala ukoo wake wote, wala hakuna mwanasheria atakayeumia isipokuwa amefanya kweli.....ila ninyi raia ndio tunawapigania na bahati mbaya hamjui hata mnachoongea. siku yako yaja utajuta.
 
Mtu mwenye PHD ya kweli, Ungelitegemea awe na General knowledge ya Maswala Muhimu ya Kijamii. This Guy Ni Msomi feki. Wa Kukremu na Kununua Vyeti. Kwanza Kwa anavyojifanya anajua Kila Kitu ni Vigumu kuniambia alikuwa na uwezo wa akujifunza (He is an Autistic, and Sadist) Next time iwe mandatory kwa Mgombea Urais apimwe akili.
Kudos bro
Hili la kupimwa akili ni muhimu maana tutajaongozwa na chizi fulani hivi
 
Nahisi hili linahitaji debate ya kina ili kujua kama mtu aliyekamatwa na ushahidi atetewe kisheria au la. Hata hivyo, haitoshi kutoa hitimisho kuwa mtu fulani ni mhalifu unless korti imethibitisha kwa kiwango cha kutokuwa na mashaka yoyote. Bila hivyo kuna watu wengi watafungwa bila hatia. Lakini pia mahakimu wanapaswa kuwa waadilifu kwa kiwango cha hali ya juu sana ili watoe haki. Mtu akiwa na kosa na ushahidi ukatolewa lazima atatiwa hatiani tu. Mimi nakumbuka nilikuwa naangaliaga movie za Ki Nigeria. Unakuta mtu kawekewa maiti ya mtu kwenye buti la gari yake ili ionekane yeye ndo kaua. Katika mazingira hayo polisi wakimkamata mtu huyo atakuwa na ushahidi, lakini huyo mtu hajaua. Na hayo mqmbo yapo sana. Mtu huyu akifungwa kwa sababu ya huo ushahidi anakuwa hajatendewa haki maana kabambikiziwa
 
WALIOKO MAGEREZA WENGI HAWANA HATIA .JE IKIWA WAKILI KATETEA NA AKASHINDWA MTEJA WAKE AKAENDA GEREZANI.HAPA NAPO TUSEMEJE ?
 
Wapingaji wengi humu ni mawakili na lawyers...... chief ndo ashatamka..... we jichanganye na school of law yako uone... km ibara zitakusaidia au lah...


Acha upumbavu we mpingaji....
Fuata maelekezo ulee familia ako....
We nani katika hii Nchi.
 
Back
Top Bottom