bopwe
JF-Expert Member
- Oct 1, 2013
- 1,768
- 1,445
Moja ya malengo yako ni kuona Raia Masikini wakifaidi uhuru, fursa na nafasi za maisha zilizopo nchini.
Fursa hizi ni nyingi na zipo katika shughuli tofauti ikitegemea kiwango cha
elimu
mtaji
na maeneo
kuna fursa za kazi za serikali
kuna fursa za kazi kwenye secta binafsi kama kuajiriwa au kuanzisha biashara mbali
kuna fursa za kilimo , kama ni kilimo cha biashara au cha kujikimu mtu na familia yake
kuna fursa za wavuvi ..kupata fursa za kuvua na kuuza samaki kama pale Ferry
kuna fursa za vibarua mbali mbali wakiwamo
wajenzi na vibarua
wafagia barabara
boda boda
hawa wote wanatumia fursa zilizopo na kwa kiwango fulani wanalindwa lindwa na vijisheria ..angalau wanafanya kazi zao bila bughudha ..wanatambuliwa.
kuna kundi moja la wananchi wako hawana fursa za kuwa huru nchini mwao. Wao biashara zao kila siku haramu , kila siku wana chezea virungu vya mgambo , nakumbuka uliwahi kusema mgambo wa jiji kupiga masikini hawa itakua mwishio...hawa ni pamoja na
kama ni suala la usafi au utaratibi...basi jiji ...lije na ubunifu...waweke utaratibu wanaotaka . madafu yanatakiwa na yanapendwa waje na wazo la vipi wauza madafu wafanye biashara zao..waweke utaratibu..sio kuwapiga marufuku bila ya solution ya kuwasaidia
wauza matunda nao waagize jiji waje na solution ..lakini sio kukataza
na mama ntilie nao jiji waje na utaratibu...huduma yao inapendwa kuifuta kwa kumwaga chakula chao sio haki
Naamini utasikiliza kilio hichi na kupiga marufuku uonevu huu..kwa kuwataka Jiji waache maonevu haya na badala yake waje na utaratibu wanao utaka...lakini kabla ya kutoa muuongozo tunakuomba usimamishe uonevu huu kwa masikini hawa...ambao ndio nguzo yako
ahsante

- wauza Madafu na Baiskeli zao hawa mtaji wao ni elfu 40...hawa masikini wa mungu wana watoto , wanataka kuwapeleka watoto wao shule nao wanataka kula nao wanataka kufaidi fursa lakini Mgambo wanawanyima fursa hio, kila siku ya mungu wanafukuzana nao, wanawanyanganya baskeli zao na kuchukua madafu (mtaji) . wauza madafu sio wahalifu...wanafanya kazi halali...na madafu ni bidhaa muhimu ni kiburudisho na dawa kwa wagonjwa. .. hawa wanatembeza na baiskeli zao hawachafui mji ..sioni sababu ya kuwanyima fursa masikini hawa kutoa huduma hii...mgambo wanawapiga kila siku inakua kama wanauza unga...ni dhulma kwa masikini hawa...sioni sababu yao kwa nini wasiuze madafu ...sioni sababu yao kuwa wahalifu kuuza madafu ndani ya nchi yao...ni uonevu
- Pili kuna mama ntilie...hawa nao bado wanasumbuliwa hasa maeneo ya upanga , mjini , kariakoo, ilala nk. Mgambo bado wamekua wakipita kila siku kumwaga na kuwapiga na kuwadhalilisha kina mama hawa masikini wa mungu...sioni dhambi ya huduma hiii , kazi yao sio haramu nao pia wanatumia fursa ya kuwa huru na ukweli watanzania wengi wanatumia chakula cha kina mama hawa..chakula chao ni rahisi na kitamu pia..lakini inasikitisha kuona mgambo wanapita kila siku kuwapiga marungu na kumwaga chakula na mitaji yao..kuwarejesha katika ufukara...tunapiga vita ukahaba...lakini biashara hizi za kina mama wasio na mitaji mikubwa nayo tunaipiga vita ..hii sio haki hii ni dhulma
- tatu kuna wauza matunda..nimeona mara kadhaa Mawaziri wengi husima njiaani kununua matunda kutoka vijana hawa ambao wamebeba matunda yao kwenye Carts au Baiskeli , wakiwa wameketi pembeni ya baadhi ya mitaa ya mjini , upanga , masaki, nk nk....hawa nao wanatumia fursa za kuwa huru ndani ya nchii yao. Biashara ya matunda sio Haramu, ni halali na wanasaidia wana nchi wengi kuwasogezea huduma hii....wengi hawachafui mazingira wanajitahidi kufanya kwa usafi ...lakini hakki hio ina pondwa na mgambo na jiji ..kila siku wanapondwa pondwa na mgambo hakika inatia uchungu , sio haki ni dhulma kuwafanyia wananchi mambo haya.