Rais Magufuli: Marufuku vikundi vya watu kugawa barakoa. Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,492
2,000
Hayo ni maagizo aliyoyatoa leo huko Dodoma ndani ya uwanja wa Jamuhuri Dodoma kwenye mkutano wa CWT.

Asema marufuku kwa vikundi vya watu kugawa barakao na ukikutwa ukamatwe ujibu ulikozitoa pamoja na hayo kama vipi shona ya kwako na unaweza chukua sidiria ya upande mmoja na kuifanya barakoa


Nukuu

Ukitaka kuvaa barakoa kashone yako, mbona ni rahisi tu, barakoa mbona imekaa kama titi moja la Mtu mmoja hivi limekatwa upande mmoja, weka huku kama... aaah samahani Mh.Waziri nimesema hapa, nilikuwa nachomekea tu kidogo”

Juzi nilikuwa nasikiliza taarifa ya habari kuna group linaitwa Magufuli Forum wala silijui, ila sishangai Mtu kujiita Magufuli hata akijiita fisi ni hiyari yake, lakini walikuwa wanagawa barakoa wala hazijulikani zinatoka wapi, tutaumia kwa kukosa maarifa


Njia nyingine ambayo inaweza kutumika ni kuletewa vifaa vya corona vyenye corona, anapokuletea Mtu barakoa hujui ameitoa wapi kataa, mwambie kavae wewe na Mke wako na Watoto wako nyumbani, tutaumizwa
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,471
2,000
Alichokuwa anaongea lazima usalaama wakipitie sasa wanamuachaje Rais anazungumza hovyo narudia tena wafukuzwe wanamdharirisha Rais kiukweli
Kama ni kujidhalilisha basi ni yeye mwenyewe... si kila asemacho kinaweza haririwa ... only kinachoandikwa tu.. PRESIDENTIAL LANGUAGE NI SHIDA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom