Rais Magufuli & Makonda hongereni sana. Sasa tuing'arishe Dar es Salaam

m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
979
1,353
Nafarijika sana utendaji kazi wa ndugu yangu RAIS Magufuli kwa kushirikiana na RC Makonda katika jiji letu la Dar. Nichukue fursa hii kuwapongeza na kuwatia moyo nikiwa kama mwananchi wa kawaida kabisa ninaye furahishwa kwa uchapa kazi wao safi. Natambua ni binadamu wasio kasoro katika utendaji wao ila nawapa hongera sana na kuwatia moyo.

Leo napenda niwape changamoto za kusaidia kuliboresha jiji letu la Dar na mengineyo kama ifuatavyo: -

1. Kwanza: Tujitahidi sote kwa pamoja kuliboresha jiji liwe safi na bora kwa afya za wakazi wake kwa wakazi wake kufanya usafi kwa kuzoa takataka kwa wakati lakini pia kusimamia sheria za uchafu. Pia yafaa kutafuta mbinu mbadala kuboresha taratibu na uwekezaji wa uzoaji taka katika jiji hili. Si hivyo tu hata dampo za utupaji takataka zitazamwe upya. Moshi wameweza Dar hatushindwi. Hili linamhusu Makonda moja kwa moja.

2. Pili: Tujitahidi kuboresha miundo mbinu ya jiji hasa barabara za Kariakoo ziwe za lami zote na mifereji ya maji taka iwekwe. Kwa kutumia fursa ya bajeti ya mwaka huu wa fedha 2018/19, ni wakati sasa kuona ni namna gani barabara zote za jiji la Dar kuboreshwa kwa kiwango cha lami na kujengwa madara na mifereji hya maji taka imara. Naamini inawezekana kupitia bajeti za ndani/wafadhili na mikopo pia. Tujaribu hili kwa awamu kila mwaka tuone mafanikio yake. (Magufuli + Makonda).

3. Tatu: Umefika wakati kwa barababra za miji yote mikubwa haswa Dar na Makao makuu ya nchi yetu Dodoma pia Mwanza, Arusha, Tanga na Mbeya kusimamiwa na TANROADS ili kuboresha miji hii na kuwa ya kisasa kwa kuweka barabara za lami za kisasa. (Magufuli + Mbarawa).

Naleta kwenu wadau wa maendeleo chanya. Najua wapo wenzetu waleee wa maendeleo hasi nao nawakaribisha kuchangia wazo hili kwa manufaa ya taifa letu.
 
Back
Top Bottom