Rais Magufuli: Majungu hayajengi na wala hayaleti maendeleo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewaasa Viongozi wa Mkoa wa Tabora kuacha majungu kutokana na eneo hilo kutawaliwa na majungu baina ya viongozi na viongozi pamoja na wananchi.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo Januari 30, wakati akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi ambapo amewataka viongozi mkoani humo kuzungumza huku akiwaeleza wazi viongozi pamoja na wananchi kuwa kuwa majungu hayajengi na wala hayaleti maendeleo.

“Tuijenge Tabora kwa kuwa na umoja, tatizo moja ninaloliona hapa Tabora ni majungu, ukigeuka huku kuna jungu, huku unakutana na jungu, majungu hayajengi Mkoa, Viongozi wa Chama na Viongozi wa Serikali mliopepwa mamlaka Tabora jengeni umoja sio majungu” amesema Rais Magufuli.

“Mbunge wa hapa Tabora anapigwa vita wakati katika Wabunge wote Mwenyekiti wa Maadili ni huyu lakini anapigwa vita, hatuwezi kuwa wote Wabunge, mumtake au hamumtaki ataendelea kuwa Mbunge, Viongozi wa Dini iombeeni Tabora majungu yapungue” ameongeza Rais Magufuli.

“Kila mmoja hapa Tabora anapigwa majungu, RC unapigwa majungu, DC unapigwa majungu, Mkuu Wa Mkoa naamini utaitisha kikao mumalize majungu yenu hapa, nimechoka kusikia majungu, tunataka maendeleo ya Tabora sio majungu, sehemu yenye majungu huwa haiendelei”

Aidha Rais Magufuli ameeleza jinsi ambavyo majungu miongoni mwa wanachi mkoani humo yaliathiri idadi ya wananchi walioshiriki zoezi la kupika kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

“Baba wa Taifa amesomea hapa Tabora, Ukombozi wa Taifa umeanzia hapa, iweje hapa pawe kitovu cha kupika majungu, hata Wabunge na Madiwani mnapigana majungu chinichini, haya majungu Tabora yamefanya hata waliopiga kura wawe wachache, wamepiga 37% tu” amesema Rais Magufuli
 
Majungu kila mahali yapo, dawa yake ni kuwasema hadharani nani anamsema nani, hawatarudia
 
Majungu yana asili yake.

Tabora asili ya majungu. Kumbe mzee wa sukuma ndani alikuwa anavumilia mengi.

Majungu siyo mtaji ukufanye utajirike. Majungu siyo biashara ukanunuliwe.

Chanzo Cha majungu ni ujinga.
 
Majungu yana asili yake.

Tabora asili ya majungu. Kumbe mzee wa sukuma ndani alikuwa anavumilia mengi.

Majungu siyo mtaji ukufanye utajirike. Majungu siyo biashara ukanunuliwe.

Chanzo Cha majungu ni ujinga.
Well spoken. Tabora imekaa kiuswazi. Nature ya uswahilini ni majungu. Haina dawa hiyo. Labda ufanyike campaign kabambe ya population replacement. Half of the TB population peleka Mara, and the vice versa. Hapo utakomesha. Vikao tu havisaidii hata chembe.

Na Jiwe anatakiwa aambiwe kwamba chanzo cha majungu ya Tabora ni uvivu. Tabora kuna watu lazy aisee! Ukikuta kijana Ni mchonga vigoda na stul , huyo ndiyo anaogopwa kwa uchapa kazi!

Kingine, huo Mji umekaliwa na Waarabu wengi. Waarabu ni sumu kwenye miji ya Kiafrica. Sijui huwa Wana laana gani? Perhaps ni ile status yao wakati wa ukoloni - second citizens. Baada ya ukoloni wamebaki na mentality hiyo, pengine wakadhani wao ni first citizens. Na mbaya zaidi pure Arabs wameshakwisha, yamebaki mazalia na mulatoz ambao Ni machokalaa tu....
 
Well spoken. Tabora imekaa kiuswazi. Nature ya uswahilini ni majungu. Haina dawa hiyo. Labda ufanyike campaign kabambe ya population replacement. Half of the TB population peleka Mara, and the vice versa. Hapo utakomesha. Vikao tu havisaidii hata chembe...

Mtu wa Tabora hata akiwa Dar, majungu haachi. Yaani ni asili.
 
Huyu mzee kama kimeumana hivi yani. mbona haongei sera na mikakati ya kuinasua nchi na matatizo yanayoikabili?
 
Bwashee Mwenyekiti wako ndiye Kinara wa Majungu. Yaani anasimama jukwaani kukemea majungu wakati anachowaambia Wananchi pale ni majungu. Hosp za Serikalu na Binafsi zinawahudumia kina nani?? Mwambieni aache majungu.
Wapika majungu wanajua mlaji. Na huko hupakua majungu yao. Hakuna mlaji mzuri wa majungu kuzidi mdukuzi. Insatiable appetite. Ukiona unaletewa majungu elewa wanakujua! Yako hayo.
 
Wapika majungu wanajua mlaji. Na huko hupakua majungu yao. Hakuna mlaji mzuri wa majungu kuzidi mdukuzi. Insatiable appetite. Ukiona unaletewa majungu elewa wanakujua! Yako hayo.
Dah siredi ifungwe tu ushamaliza. Ukiona rafiki anakuagizia bia ujue anakufahamu kuwa ni mnywaji
 
Tabora ndo asili yao hiyo. Si unamuona hata msomi wao namba moja (Dr. Hamis Kigwangallah) aina ya uandishi anaofanya Fesibuku. Yaani anajitahidi sana kuminya, ila bado asili ya majungu inaonekana. Sasa piga picha mwananchi wa kawaida huko Tabora yuko fiti namna gani katika sekta ya majungu.

Kuhusu suala la uhuru kuanzia Tabora ni sawa kabisa. Maana harakati za uhuru zilikuwa ni majungu dhidi ya mkoloni.
 
watanzania wote wanao fanya kazi maofisini sio tu tabora bali nchi nzima acheni tabia ya majungu kazini kwani tabia ya kupigana majungu inapunguza ufanisi wa kazi.
 
Dah siredi ifungwe tu ushamaliza. Ukiona rafiki anakuagizia bia ujue anakufahamu kuwa ni mnywaji
Yawezekana nchi ikapona. Majungu hayajengi. Kumbuka Nchemba alivyotumbuliwa kwa sababu 13. Akarudi tena? Ndungulile kwenye kampeni mwenyewe hakuamini akiitwa msemakweli.

Na ndiye alipigania Kigamboni kuwa wilaya! Gambo alitumbuliwa kwa majungu. Si unajua tena Tabora huchuana na Pwani kwa mapishi. Lakini leo Gambo ni mbunge kwa sababu ya majungu. Alipeleka kunako kuwa Arusha Mjini hakuna mwakilishi wa wananchi!

Mchawi na mnafiki ni watu wa kuchoma kwa moto wa jehanamu. Uongo na majungu ni alama za mnafiki. Majungu ya mtaani madhara yake mtaani tu. Majungu yakiingia ikulu kiyama. Jamaa jf kasema: daktari kaumia!
 
Ni kweli kabisa.

Chadema wamekalia majungu tu kuhusu Corona!
Bora majungu ya Chadema hayaathili uhai wa mtu

Kuna majungu kwenye Baadhi ya miji na ndiyo Maana inakuwa ni shida kuendelea hiyo miji

Miji ni ya muda mreeefu tokea mjerumani Hadi hivi leo haijaendelea, wengi wa watu wa miji hiyo ni wenyeji tupu, hawataki wageni, na hata wageni wakija inakuwa kelo kwao, wakionyesha juhudi ya maendeleo wanapigwa majungu balaaa

Wenyeji hawafanyi kazi, mgeni akijituma, wako radhi hata kumwendea Kwa wapiga lamli, husema, yaani mgeni atoke huko alikotoka aje atajirike kuliko Sisi wenye mji, kuliko Sisi wenyeji?
Atatujua Sisi ni kina Nani

Hayo majungu, bado yapo Sana kwenye miji iliyokuwa ikikaliwa na waarabu

Angalia hata sasa, miji yoote iliyokuwa ikikaliwa na waarabu jinsi ilivyo, linganganisha na miji ambayo mwalabu hakukaa inakimbia tu kimaendeleo

Utakuta mji mzima hauna hata mtu mmoja aliye na degree!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom