VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Ndani ya CCM ni mchafukoge. Maumivu ya utumbuaji wa majipu yamefika. Waliotumbuliwa,kwa asilimia kubwa sana, ni makada wa chama. Michango yao ya hali na mali imeyeyuka.
Michango yao iliyokuwa ikitumika kama posho,pashu na pashi,sasa haipo tena. CCM inayumba. Hakuna mikutano ya kichama,semina za namna wala ziara za kiidara. Majipu yanaumiza chama.
Rais,makada wanapanga usiwe wewe. Usiwe Mwenyekiti. Kuna marupurupu ambayo ni kama marapurapu yamebakia. Ukiwa Mwenyekiti,utayatumbua. Ukiyatumbua,makada watakimbia. Chama kitafifia na hata kujifia. Makada wapo tayari kuzuia Uenyekiti wako.
Kuna mambo mawili. Kwanza,CCM imekuwa ikijengeka na kukua kutegemea watumbuliwaje. Yaani,hayo mambo yao batili. Pili,makada wengi wa sasa wa CCM ni makadamaslahi. Itakuwaje ukiwa Chairman na kutumbua maslahi? Majipu yanahitaji dripu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam