RAIS MAGUFULI, MAJALIWA WATUMIKA VIBAYA -Mfanyabiashara SCUBA atamba kuwaweka Mfukoni

mwobho

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
808
352
Mfanyabiashara SCUBA atamba kuwaweka Mfukoni
JM1-4.jpg

L Awanyang’anya Ardhi watu akisingizia kutumwa nao

L Atisha watu kwa kuonyesha Picha alizopiga na viongozi hao

L Atamba Polisi, Mahakama vipo upande wao kwa sasa

Na. JAMVI LA HABARI.

Jina la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na lile la waziri mkuu wake Majaliwa Kassim Majaliwa, yameanza kutumika vibaya na na watu mbali mbali ikiwemo wafanyabiashara ili kujipatia mahitaji yao kirahisi JAMVI LA HABARI linathibitisha.

Taarifa za uchunguzi ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha namna watu hao wanaotumia majina ya viongozi wakubwa wakiwemo Rais na waziri mkuu wanavyosababisha usumbufu kwa watu wengine, taasisi za serikali na taasisi binafsi huku kipaumbele chao kikiwa ni kutimiza malengo yao binafsi ama ya kibiashara bila kujali wenzao watajisikiaje.

Katika tukio lililojichukulia umaarufu hivi karibuni ni lile lililofanywa na mfanyabiashara (sharrif) Abdulkadir Scaba Scuba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya amani mkoa wa Dar es salaam kuvamia na kupora ardhi zaidi ya heka 5000 zilizopo kigamboni na yeye mwenyewe kujikabidhi heka elf tatu na heka elfu mbili kuzigawa kwa watu mbalimbali wakiwemo vigogo wa taasisi mbalimbali za serikali.

Taarifa hizo zinaonyesha kuwa SCUBA amekuwa akipita akitamba maeneo mbalimbali ya jiji kuwa kwa sasa hakuna mtu yeyote katika Tanzania hii atakayeweza kumfanya chochote kwa kuwa yeye anamiliki ufunguo wa moja kwa moja kuingia ikulu saa na wakati wowote anapojisikia kufanya hivyo.

Sambamba na kujitapa huko SCUBA anadaiwa kuwatisha watu wote anaoingia nao kwenye mgogoro hasa wa kudaiana mali au anapokuwa kwenye mjadala wowote, huwatisha kwa kuwaonyesha picha zake mbali mbali alizopiga na viongozi hao wa kitaifa.

Miongoni mwa picha anazotambia SCUBA na kuwatishia watanzania wenzake ambao kwa namna moja ama nyingine hawana uwezo wa kufanya kama yeye, ni ile inayomuonyesha SCUBA akiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli picha ambayo ameisambaza pia kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.

Picha nyingine anayoitumia kuwatisha watu inamuonyesha SCUBA akiwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa wakiwa wamesimama ofisini na kuitambia kuwa yeye ni mtu wa kuingia ofisi zote kwa sasa.

SCUBA, kwa kujiamini kabisa, anawatisha watu kwa kuwaonyesha pia picha ya yeye akiwa na waziri mkuu tena, safari hii wakiwa wamevaa kanzu na kofia ikiwa ni ishara kuwa walikuwa kwenye shuhuli ya kidini.

Gazeti hili linafahamu kwamba, ni jambo la kawaida sana kwa viongozi wa kitaifa kupiga picha na watu mbali mbali hapa nchini pindi yanapotokea matukio mbalimbali ya kijamii yanayowakutanisha watu wengi na viongozi wao ambao sio mara kwa mara hukutana.

Rais Magufuli ni miongoni mwa viongozi wengi barani afrika ambao wanapoombwa kupiga picha na mtu hukubali bila kinyongo na mara nyingine yeye mwenyewe huwaambia watu aliokutana nao haya njooni tupige picha (mfano alipotembelea ghafla wizara ya fedha na kuwakuta wafanyakazi wameondoka. Akawaambia waliopo wapige naye picha).

Kitu kinachoshangaza na kuonyesha kutaka kumtumia vibaya Rais na waziri mkuu wake, ni kitendo cha mfanyabiashara huyu kuzitumia picha hizo kama kinga yake ya kibiashara na kuendelea kuwatisha watu kwa simu.

Mzee mwakabenga ni mmoja wa wahanga wa mikwara ya mfanyabiashara huyo amenukuliwa akisema kwao sasa imekuwa ni kero na mateso kiasi cha kutokuamini kama Rais Magufuli analijua hili na kama analiunga mkono.

‘’kwa kweli sielewi kama Rais analifahamu hili, maana yeye mwenyewe anasema ametumwa na Rais na Waziri mkuu. Hivyo hana wasiwasi, lakini siamini kama waziri mkuu au Rais anaweza Kumtuma Kufanya vitu vya namna hii’’. Alisema

Akiongea kwa masikitiko ameendelea ‘’huyu bwana huku kigamboni sasa hivi amefikia hatua mpaka ya kujiita Rais wa huku, ukimuuliza kwa nini anakwambia yeye na Magufuli ni damudamu’’.

‘’Mara anatuonyesha Missed Call ya Rais, Mara ya waziri Mkuu, mara atuulize sisi kama tulishawahi kukutana na Rais ama hata kupiga naye picha?. Kama ni kweli Rais na waziri mkuu wanampigiaga simu huyu bwana basi anafaidi huu sana huu utawala na ndio maana anatutesa’’. aliongeza

Vithibitisho ambavyo gazeti hili linavyo vinaonyesha kwamba SCUBA amekuwa na tabia hiyo na zaidi amekuwa akiwatisha hata polisi kutomchukulia hatua yoyote yanapopelekwa malalamiko dhidi yake na mara nyingi malalamiko hayo hugeuzwa na kuwa mashitaka dhidi ya aliyelalamika.

Katika tukio la kupora ardhi hiyo ya heka 5000, SCUBA anadaiwa kuigawa heka 2000 kwa watu kadhaa mashuhuri hapa nchini ambao gazeti hili lina orodha yao, miongoni mwa watu hao wamo askari polisi, wanajeshi, wafanyakazi wa serikali na viongozi kadhaa wa umma.

Gazeti hili linaendelea na uchunguzi juu ya SCUBA na watanzania wengine wote wenye tabia na mienendo kama yake.

Katika hali ya kawaida ni hatari kwa ustawi wa nchi kwa watu wa tasnia mbalimbali kutumia majina ya viongozi kujinufaisha
 
Hii nchi ina mambo, kila mtu ana sharubu!
‘’kwa kweli sielewi kama Rais analifahamu hili, maana yeye mwenyewe anasema ametumwa na Rais na Waziri mkuu. Hivyo hana wasiwasi, lakini siamini kama waziri mkuu au Rais anaweza Kumtuma Kufanya vitu vya namna hii’’....taarifa inasema
 
Hii inasound kama gesture nani rubbish haiweze kanikupiga pic na rais iwe kigezo cha kua ana free pass ikulu
 
‘’kwa kweli sielewi kama Rais analifahamu hili, maana yeye mwenyewe anasema ametumwa na Rais na Waziri mkuu. Hivyo hana wasiwasi, lakini siamini kama waziri mkuu au Rais anaweza Kumtuma Kufanya vitu vya namna hii’’
 
Rais amesikia na waziri mkuu pia, tunangoja majibu tuone kama ni kweli wamemtuma.

Lakini najiuliza maswali kadhaa sipati majibu, kama ni kweli wanamtuma..

wanamtuma yeye kama nani?
Nini ujira wake ktk kutumwa huko?
Je viongozi wa serikali hawajui wajibu wao mpaka atumwe yeye?
Nini kazi ya waziri wa ardhi na maafisa ardhi wa eneo husika? Wawakirishi wa rais kisheria yaani mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wako wapi? Kama rais kweli ana mwamini yeye na kumtuma kwanin asingemteua kuwa mkuu wa mkoa au wilaya?
Hayo ni baadhi ya maswali ninayojiuliza pasipo majibu.
Nadhan zama za vitisho hivyo vimepita kitambo wote wanaotishwa hawajitambui.
Haya Mheshimiwa rais tujibu kama umemtuma.
 
waandishi wa tanzania hata sijui kama walienda shule..
.kwani inashindikana nini hao watu kumtuma scuba?anajiamin vip mpka kuchukua eka 5000 za wanavijiji...inawezekana picha anazitumia ipasavyo kama alivyoelekezwa..badala ya kumtuhumu wangejilizisha kwanza.
 
Rais amesikia na waziri mkuu pia, tunangoja majibu tuone kama ni kweli wamemtuma.

Lakini najiuliza maswali kadhaa sipati majibu, kama ni kweli wanamtuma..

wanamtuma yeye kama nani?
Nini ujira wake ktk kutumwa huko?
Je viongozi wa serikali hawajui wajibu wao mpaka atumwe yeye?
Nini kazi ya waziri wa ardhi na maafisa ardhi wa eneo husika? Wawakirishi wa rais kisheria yaani mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wako wapi? Kama rais kweli ana mwamini yeye na kumtuma kwanin asingemteua kuwa mkuu wa mkoa au wilaya?
Hayo ni baadhi ya maswali ninayojiuliza pasipo majibu.
Nadhan zama za vitisho hivyo vimepita kitambo wote wanaotishwa hawajitambui.
Haya Mheshimiwa rais tujibu kama umemtuma.

umejenga hoja nzuri sana
 
Kumbe wote ni majipu du sasa awa watatumbuliwa na nani?
‘’kwa kweli sielewi kama Rais analifahamu hili, maana yeye mwenyewe anasema ametumwa na Rais na Waziri mkuu. Hivyo hana wasiwasi, lakini siamini kama waziri mkuu au Rais anaweza Kumtuma Kufanya vitu vya namna hii’’
 
Mfanyabiashara SCUBA atamba kuwaweka Mfukoni
View attachment 339789
L Awanyang’anya Ardhi watu akisingizia kutumwa nao

L Atisha watu kwa kuonyesha Picha alizopiga na viongozi hao

L Atamba Polisi, Mahakama vipo upande wao kwa sasa

Na. JAMVI LA HABARI.

Jina la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na lile la waziri mkuu wake Majaliwa Kassim Majaliwa, yameanza kutumika vibaya na na watu mbali mbali ikiwemo wafanyabiashara ili kujipatia mahitaji yao kirahisi JAMVI LA HABARI linathibitisha.

Taarifa za uchunguzi ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha namna watu hao wanaotumia majina ya viongozi wakubwa wakiwemo Rais na waziri mkuu wanavyosababisha usumbufu kwa watu wengine, taasisi za serikali na taasisi binafsi huku kipaumbele chao kikiwa ni kutimiza malengo yao binafsi ama ya kibiashara bila kujali wenzao watajisikiaje.

Katika tukio lililojichukulia umaarufu hivi karibuni ni lile lililofanywa na mfanyabiashara (sharrif) Abdulkadir Scaba Scuba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya amani mkoa wa Dar es salaam kuvamia na kupora ardhi zaidi ya heka 5000 zilizopo kigamboni na yeye mwenyewe kujikabidhi heka elf tatu na heka elfu mbili kuzigawa kwa watu mbalimbali wakiwemo vigogo wa taasisi mbalimbali za serikali.

Taarifa hizo zinaonyesha kuwa SCUBA amekuwa akipita akitamba maeneo mbalimbali ya jiji kuwa kwa sasa hakuna mtu yeyote katika Tanzania hii atakayeweza kumfanya chochote kwa kuwa yeye anamiliki ufunguo wa moja kwa moja kuingia ikulu saa na wakati wowote anapojisikia kufanya hivyo.

Sambamba na kujitapa huko SCUBA anadaiwa kuwatisha watu wote anaoingia nao kwenye mgogoro hasa wa kudaiana mali au anapokuwa kwenye mjadala wowote, huwatisha kwa kuwaonyesha picha zake mbali mbali alizopiga na viongozi hao wa kitaifa.

Miongoni mwa picha anazotambia SCUBA na kuwatishia watanzania wenzake ambao kwa namna moja ama nyingine hawana uwezo wa kufanya kama yeye, ni ile inayomuonyesha SCUBA akiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli picha ambayo ameisambaza pia kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.

Picha nyingine anayoitumia kuwatisha watu inamuonyesha SCUBA akiwa na waziri mkuu Kassim Majaliwa wakiwa wamesimama ofisini na kuitambia kuwa yeye ni mtu wa kuingia ofisi zote kwa sasa.

SCUBA, kwa kujiamini kabisa, anawatisha watu kwa kuwaonyesha pia picha ya yeye akiwa na waziri mkuu tena, safari hii wakiwa wamevaa kanzu na kofia ikiwa ni ishara kuwa walikuwa kwenye shuhuli ya kidini.

Gazeti hili linafahamu kwamba, ni jambo la kawaida sana kwa viongozi wa kitaifa kupiga picha na watu mbali mbali hapa nchini pindi yanapotokea matukio mbalimbali ya kijamii yanayowakutanisha watu wengi na viongozi wao ambao sio mara kwa mara hukutana.

Rais Magufuli ni miongoni mwa viongozi wengi barani afrika ambao wanapoombwa kupiga picha na mtu hukubali bila kinyongo na mara nyingine yeye mwenyewe huwaambia watu aliokutana nao haya njooni tupige picha (mfano alipotembelea ghafla wizara ya fedha na kuwakuta wafanyakazi wameondoka. Akawaambia waliopo wapige naye picha).

Kitu kinachoshangaza na kuonyesha kutaka kumtumia vibaya Rais na waziri mkuu wake, ni kitendo cha mfanyabiashara huyu kuzitumia picha hizo kama kinga yake ya kibiashara na kuendelea kuwatisha watu kwa simu.

Mzee mwakabenga ni mmoja wa wahanga wa mikwara ya mfanyabiashara huyo amenukuliwa akisema kwao sasa imekuwa ni kero na mateso kiasi cha kutokuamini kama Rais Magufuli analijua hili na kama analiunga mkono.

‘’kwa kweli sielewi kama Rais analifahamu hili, maana yeye mwenyewe anasema ametumwa na Rais na Waziri mkuu. Hivyo hana wasiwasi, lakini siamini kama waziri mkuu au Rais anaweza Kumtuma Kufanya vitu vya namna hii’’. Alisema

Akiongea kwa masikitiko ameendelea ‘’huyu bwana huku kigamboni sasa hivi amefikia hatua mpaka ya kujiita Rais wa huku, ukimuuliza kwa nini anakwambia yeye na Magufuli ni damudamu’’.

‘’Mara anatuonyesha Missed Call ya Rais, Mara ya waziri Mkuu, mara atuulize sisi kama tulishawahi kukutana na Rais ama hata kupiga naye picha?. Kama ni kweli Rais na waziri mkuu wanampigiaga simu huyu bwana basi anafaidi huu sana huu utawala na ndio maana anatutesa’’. aliongeza

Vithibitisho ambavyo gazeti hili linavyo vinaonyesha kwamba SCUBA amekuwa na tabia hiyo na zaidi amekuwa akiwatisha hata polisi kutomchukulia hatua yoyote yanapopelekwa malalamiko dhidi yake na mara nyingi malalamiko hayo hugeuzwa na kuwa mashitaka dhidi ya aliyelalamika.

Katika tukio la kupora ardhi hiyo ya heka 5000, SCUBA anadaiwa kuigawa heka 2000 kwa watu kadhaa mashuhuri hapa nchini ambao gazeti hili lina orodha yao, miongoni mwa watu hao wamo askari polisi, wanajeshi, wafanyakazi wa serikali na viongozi kadhaa wa umma.

Gazeti hili linaendelea na uchunguzi juu ya SCUBA na watanzania wengine wote wenye tabia na mienendo kama yake.

Katika hali ya kawaida ni hatari kwa ustawi wa nchi kwa watu wa tasnia mbalimbali kutumia majina ya viongozi kujinufaisha

kweli kabisa.
 
Sijawahi kuliona au kulisoma hili gazeti la Jamvi la Habari. Lakini kwa kuangalia tu jina lake "Jamvi la Habari" ambalo binafsi naona halina mvuto sana na pia kwa kuona hiyo front page yake iliyopo hapo juu kwa haraka haraka napata mashaka na umakini wa gazeti hili.

Kwanza, pale juu kwenye gazeti kuna hii ya kuomba radhi kwa PPF kutokana na kuihusisha kimakosa katika habari iliyotoka katika matoleo yaliyopita (kukosa umakini).

Pili, chini ya picha ya huyo Scuba na rais Magufuli (ambayo ni photoshop) kushoto mwa gazeti kuna maelezo ya picha ambayo ukisoma sentensi yake ya mwisho utagundua kuwa wamerudia baadhi maneno (kukosa umakini).

Tatu, picha ya kulia, maelezo yaliyo chini yake yanazungumzia picha ya Scuba na Magufuli wakati picha hiyo ambayo nayo inaonekana ni photoshop ni ya Scuba na waziri mkuu Majaliwa (kukosa umakini).

Sasa kwangu mimi msomaji mpya na kwa gazeti jipya kama hilo ambalo bado linaangaika kwenye market penetration ninapojumlisha makosa hayo matatu YALIYOTOKEA KWENYE TOLEO MOJA kwa haraka haraka napoteza kabisa imani na gazeti husika na hivyo kuwashauri wawe makini au tuseme waongeze umakini kwenye kazi yao.
 
Watanzania mmezidi uzezeta yaani uninyang'anye ardhi yangu kwa kunionesha picha ya raisi naondoka na shingo yako.
 
Back
Top Bottom