beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwa miongoni mwa walio katika Serikali inayoongozwa na Rais Hussein Mwinyi, akisema uzoefu wake kama Kiongozi ni mkubwa na unahitajika kwenye Uongozi wa sasa.
Akizungumza kutokea Chato Mkoani Geita, Rais Magufuli amesema, katika Umoja wao (Dkt. Mwinyi na Makamu wa Kwanza na wa Pili wa Rais) mwanga wa Maendeleo ya Zanzibar umeanza kuonekana, akisisitiza pia ni Maendeleo ya Tanzania
Amewataka waendelee kufanya kazi akiwahakikishia ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema hatowaacha kamwe kwasababu wote wanahubiri Amani.
Rais Mwinyi na Maalim Seif wamewasili Wilayani Chato leo kwa ziara ya siku mbili.