johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,873
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli amesema uchaguzi mkuu wa 2025 utatoa fursa kwa vijana kwa sababu zaidi ya 65% ya wapiga kura ni vijana
Rais Magufuli ametoa mfano wa mh Lukuvi kwamba hawezi kuwa Rais wa JMT 2025 kwa sababu atakuwa na miaka zaidi ya 70.
Maendeleo hayana vyama!
=======
RAIS MAGUFULI: Hakuna mtu alitegemea Mwinyi atakuwa Rais wa Zanzibar lakini pia Mwinyi katika kipindi chake chote hakuutafuta Urais, vitu hivi vinapangwa. Hakuna mtu alijua profesa Ibrahim atakuwa Jaji mkuu wa Tanzania hata mimi sikujua kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kwa sababu katika miaka yote ishirini nikiwa waziri na nikiwa mbunge sikuwahi kuomba hata ujumbe wa NEC.
Sikuwahi, wajumbe wa NEC walikuwa wakina Lukuvi, tangu aingie mle ni mjumbe wa NEC lakini Urais hakuupata na sina uhakika kama ataupata Urais. Wewe sasa hivi ana miaka sitini na kitu, tukapendekeze kwenye central committee tukachague Rais anaenizidi umri mimi, ndio ukweli.
Maneno mengine yanaumiza lakini nataka niwaeleze muwe mnajitayarisha kisaikolojia kusudi msipoteze hata hela zenu, hata wewe profesa Kabudi huwezi ukawa Rais, najua haya mambo ni magumu lakini huo ndio ukweli.
Mzee Kikwete wakati anaondoka, alisema hataona Rais ambae anamzidi umri wake, sasa muangalie mimi nina umri gani nitakapokuwa namaliza, ujipimie kuanzia kwenye umri pale. Yaani Malecela tumpendekeze awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haiwezekani! Ameshakuwa mstaafu, tunamheshimu, tunampenda.
Najua mmenyamaza kwa hiyo inawezekana umekaa na jirani yako ambae ndie atakuwa Rais ambae labda ni kijana zaidi kwa sababu 65% ya watanzania ni vijana na hivi ndivyo vilivyomsaidia Mwinyi kushinda kule, wapiga kura ni vijana wether you like or not huo ndio ukweli, sasa huwezi ukawapelekea wapiga kura mtu ambae sio saizi yao.
Maneno yanauma lakini si mmeniomba niseme hapa, mimi nilikuwa nimekaa kimya tu leo nisiseme, nilikuwa nachomekea tu.