Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,803
2,000
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli amesema uchaguzi mkuu wa 2025 utatoa fursa kwa vijana kwa sababu zaidi ya 65% ya wapiga kura ni vijana

Rais Magufuli ametoa mfano wa mh Lukuvi kwamba hawezi kuwa Rais wa JMT 2025 kwa sababu atakuwa na miaka zaidi ya 70.

Maendeleo hayana vyama!

=======

RAIS MAGUFULI: Hakuna mtu alitegemea Mwinyi atakuwa Rais wa Zanzibar lakini pia Mwinyi katika kipindi chake chote hakuutafuta Urais, vitu hivi vinapangwa. Hakuna mtu alijua profesa Ibrahim atakuwa Jaji mkuu wa Tanzania hata mimi sikujua kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa sababu katika miaka yote ishirini nikiwa waziri na nikiwa mbunge sikuwahi kuomba hata ujumbe wa NEC.

Sikuwahi, wajumbe wa NEC walikuwa wakina Lukuvi, tangu aingie mle ni mjumbe wa NEC lakini Urais hakuupata na sina uhakika kama ataupata Urais. Wewe sasa hivi ana miaka sitini na kitu, tukapendekeze kwenye central committee tukachague Rais anaenizidi umri mimi, ndio ukweli.

Maneno mengine yanaumiza lakini nataka niwaeleze muwe mnajitayarisha kisaikolojia kusudi msipoteze hata hela zenu, hata wewe profesa Kabudi huwezi ukawa Rais, najua haya mambo ni magumu lakini huo ndio ukweli.

Mzee Kikwete wakati anaondoka, alisema hataona Rais ambae anamzidi umri wake, sasa muangalie mimi nina umri gani nitakapokuwa namaliza, ujipimie kuanzia kwenye umri pale. Yaani Malecela tumpendekeze awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haiwezekani! Ameshakuwa mstaafu, tunamheshimu, tunampenda.

Najua mmenyamaza kwa hiyo inawezekana umekaa na jirani yako ambae ndie atakuwa Rais ambae labda ni kijana zaidi kwa sababu 65% ya watanzania ni vijana na hivi ndivyo vilivyomsaidia Mwinyi kushinda kule, wapiga kura ni vijana wether you like or not huo ndio ukweli, sasa huwezi ukawapelekea wapiga kura mtu ambae sio saizi yao.

Maneno yanauma lakini si mmeniomba niseme hapa, mimi nilikuwa nimekaa kimya tu leo nisiseme, nilikuwa nachomekea tu.
 

mzushi

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
2,935
2,000
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,071
2,000
Mara hii wameanza kuongelea urais 2025! CCM kweli wameamua kuitafuna nchi milele liwe jua iwe mvua; hii nchi hawaiachii kwa "vikaratasi". Badala ya kuongelea vitu vya muhimu hususan tume huru ya uchaguzi, Katiba Mpya, etc. wanaanza kutajataja nani anafaa na nani hafai mapema hivi? Kwa mtindo huu, tundelee kuzoea "bao la mkono" miaka mingi ijayo!
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,071
2,000
Mara hii wameanza kuongelea urais 2025! CCM kweli wameamua kuitafuna nchi milele liwe jua iwe mvua; hii nchi hawaiachii kwa "vikaratasi". Badala ya kuongelea vitu vya muhimu hususan tume huru ya uchaguzi, Katiba Mpya, etc. wanaanza kutajataja nani anafaa na nani hafai mapema hivi? Kwa mtindo huu, tundelee kuzoea "bao la mkono" miaka mingi ijayo!
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
13,071
2,000
Kigezo alichotumia ni 60% ya watanzania ni vijana hivyo Rais ajaye lazima atokane na kundi hilo. Kisichofafanuliwa ni ujana unaanzia miaka mingapi hadi mingapi! Otherwise it seems yeyote mwenye age sawa na or less than his ni kijana! Hayo ya Katiba unayajua wewe Chief.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
38,395
2,000
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli amesema uchaguzi mkuu wa 2025 utatoa fursa kwa vijana kwa sababu zaidi ya 65% ya wapiga kura ni vijana.

Rais Magufuli ametoa mfano wa mh Lukuvi kwamba hawezi kuwa Rais wa JMT 2025 kwa sababu atakuwa na miaka zaidi ya 70...
Itatusaidia nini sisi
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
3,934
2,000
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi...
Kwani yeye hajui hiyo mistari ya KATIBA?!!

Ndio ameshasema hivyo Kama MWENYEKITI WA CCM....

Sasa tuone KIPI "kitasimama" kati ya hivyo vifungu usemavyo na KAULI YAKE....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom