Rais Magufuli leo anamuapisha Kamishna wa Maadili Jaji Mwangesi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,883
141,815
Hafla hiyo itafanyika Ikulu , Chamwino jijini Dodoma saa 4 kamili asubuhi.

Tukio litarushwa mubashara TBC, Channel ten na ITV.

Updates;

======

Rais Magufuli ameingia ukumbini na zoezi la kiapo limeanza.

Kiapo kimekamilipa na sasa Naibu waziri wa Utumishi mh Ndejembi anatoa salamu za wizara.

Rais Magufuli ameanza kuhutubia kwa kuwataka viongozi wote kujaza fomu za maadili kwani zimebaki siku saba tu muda wa kisheria kujaza fomu hizo kukamilika.

===
RAIS MAGUFULI: ASHUKU USIRI WA KURUDISHA FOMU KWA NJIA YA MTANDAO

Katika kumuapisha Kamishna wa Maadili, Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi, Rais John Magufuli amesema fomu za maadili zisirudishwe kwa njia ya mtandao

Amesema mtu akirudisha fomu kwa njia ya mtandao na akawepo mtu anayejua ‘passwords’ anaweza kuangalia fomu hizo na kujua siri za mtu husika na kuharibu kwa kuwa wadukuzi wako wengi

Amesema ni muhimu watu kudownload mtandaoni lakini warudishe fomu hizo kwa kuzipeleka tume ya maadili na sio kutumia njia ya mtandao

Amesema njia ya mtandao ni hatari kwa sababu wadukuzi wanaweza kubadili hata viwango vya fedha ambavyo vimeandikwa
 
Anamtafutia sababu MKM ije kuwa Yale Yale ENL....tusubiri matamu yaja !!! Anaona anajijenga na soon atakuwa nguvu ndani nje chama na serikali ......DEDz etc ....muda mwalimu mzuri
 
Hali sector ardhi ni tete atoe maelekezo BOT na wadau wabuni njia mbadala, familia zinapoteza makazi na mabenk yanakwama rejesha fedha hakuna wanunuzi.
 
Mimi nasubiri dongo la kufungia mwaka. Ukute atafanya teuzi nyingine on the spot.
 
Back
Top Bottom