OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,072
- 114,561
Kama tuna nia ya dhati ya kumsaidia Rais Magufuli kutatua changamoto ya sukari nchini, hatuna budi kumshauri kitaalamu, na sio kishabiki. Majuzi niliweka andiko hapa juu ya crisis ya sukari nchini nikieleza mbinu za kiuchumi za kukabiliana na changamoto hii na sio kutumia ubabe.
Kama kweli unaipenda Tanzania na unamtakia heri Rais JPM afanikiwe ni vizuri kumshauri, kumpongeza na kumkosoa pale anapoteleza. Kuna watu wamenifuata inbox wanalalamika "Malisa hii serikali haina jema kwako, kila siku kuiponda?"
Kwanza nieleza wazi kuwa huwa sipondi serikali. Kuponda maana yake ni kupinga tu bila kuwa na hoja. Mimi huwa nafanya "intellectual critics" (kukosoa kwa hoja na kushauri kwa kupendekeza alternatives ili kuleta ustawi kwa wananchi). Na Hii ndio maana ya usomi.
Rafiki yangu mmoja yeye kila jambo analofanya Magufuli anashangilia na kusema "NINA IMANI NA MAGUFULI". Ni jambo jema kuwa na imani na mtu lakini kama humsaidii wala kumshauri pale anapoteleza imani yako haina maana. Lazima tujifunze kuwa critical na tuelewe kuwa kukosoa si dhambi, hasa kama ukosaji unafanywa kwa maslahi ya taifa.
Haiwezekani sukari imefika Sh.4000 katika baadhi ya maeneo ya nchi, halafu sisi tunashauri alternatives za Rais kufanya ili kutatua tatizo hili tunaonekana wabaya. Huku wengine wakishangilia kuwa WANA IMANI na Rais. Hiyo imani yako kwa Rais itakusaidia nini kama bibi yako atashindwa kunywa chai kutokana na mfumuko wa bei ya sukari? Hata mimi nina imani kubwa sn na mama yangu lakini anapoteleza huwa namwambia "my lovely mamito hapa umechemsha".Then namshauri njia bora ya kufanya asiteleze tena.
Kupiga tu makofi kwa Rais kuwa una imani nae ni uzwazwa. Hata waliomuangusha JK wengi ni wale waliokua wakimpigia makofi na kuimba kuwa wana IMANI nae. Tuliomkosoa tukaonekana wabaya, leo JPM anamkosoa JK kwa mambo yaleyale, lakini cha ajabu watu walewale walioimba kuwa wana imani na JK ndio haohao wanaomshangilia JPM. Uzwazwa.!
Sasa turejee kuhusu hili la sukari. Kwanza nipende kuweka wazi kuwa hakuna mtu mwenye lengo la kuona watanzania wanataabika. Hakuna mtu mwenye nia ya kuona watu wakishindwa kunywa chai kwa kukosa sukari. Hakuna mtu aliye tayari kuona sukari ikiuzwa Sh.5000/= kwa kilo.
Kwahiyo both "wakosoaji" na wale "washangiliaji" wa JPM wote tuna nia moja ya kuona bei ya sukari ikipungua. Tatizo ni kwamba tunatofautiana approach.
Washangiliaji wanaamini approach anazotumia JPM ni sahihi na hazitakiwi kukosolewa. Yani wanamuona JPM ni kama malaika hawezi kukosea, na kumkosoa ni dhambi. Kwahiyo akisema hakuna kuingiza sukari nje bila kibali maalumu wanashsngilia, bei ikipanda wanalia, lakini tukishauri wanakasirika. Kichekesho. Wanasahau kuwa JPM nae ni binadamu na ana madhaifu yake.
Binafsi naamini tangu mwanzo kabisa wa suala hili JPM alikosea approach. Na makosa ya Rais wetu huyu mpendwa ndiyo yanayotugharimu hadi hivi sasa. It was one mistake with several goals. Wenye "upeo" tuliona Rais kakosea, lakini tuliposema tukaonekana wabaya. Washangiliaji wakaendele kushangilia kuwa wana IMANI na Rais. Leo wameona matokeo wanaanza kulia.
Ngoja nieleze kwa kifupi ni kwanini apprpach aliyotumia JPM tangu mwanzo ilikua na makosa, na ni kwanini approach anazoendelea kutumia hadi sasa haziwezi kusaidia badala yake zitafanya hali kuwa mbaya zaidi.
#MOSI
Ikumbukwe kabla ya February 18 Rais JPM alipotoa katazo la kuzuia sukari ya nje "bila kibali maalumu" hakukua na tatizo la sukari nchini. Sukari ilikuwepo ya kutosha na iliuzwa kwa bei ya kawaida. Lakini baada ya tangazo la Rais tatizo likaanzia hapo. Sukari ikaanza kukosekana na ikaanza kupanda bei kiholela. Kwa hiyo tamko la Rais ndiyo chanzo cha leo kununua sukari Sh.4000/= kwa kilo.
Swali ni je Rais alizuia sukari ya nje kwa nia mbaya? Jibu ni hapana. Rais alikua ana nia njema ya kulinda viwanda vyetu vya ndani (infant industries) dhidi ya viwanda vikubwa vya nje. Viwanda vyetu bado ni vichanga (infant) kwahiyo tusipoweka njia nzuri za kuvilinda, vitakufa kutokana na ushindani wa nje. Hii ni mbinu ya kawaida kbs ktk uchumi iitwayo Protectionism.
Kwahiyo LENGO la JPM lilikua jema ila NJIA (approach) aliyotumia ni MBAYA. Na hili ndio tatizo kuwa la Rais wetu. Ana MALENGO MAZURI sana juu ya Taifa letu lakini anatumia NJIA ZISIZO SAHIHI kufikia hayo malengo. Matokeo yake anakwama njiani.
Ndio maana Mbowe aliposema JPM ana nia njema ya kulifikisha taifa hili mahali fulani lakini hata yeye mwenyewe hajui ni wapi, watu walimbeza. Lakini ndio ukweli. Serikali haikutakiwa kumbeza Mbowe bali kuchukua ushauri wake na kuufanyia kazi. Wakae na Rais wajue nia yake ya kule anakotaka kufika halafu wamshauri njia ya kufika. Tusipomshauri njia sahihi za kutumia atashindwa kufikia malengo yake.
Kwa mfano hili la sukari alisema "nasitisha uagizaji wa sukari ya nje kuanzia leo". Hii si sahihi. Na bahati mbaya washauri wake hawakumshauri vizuri. Bila shaka nao ni walewale wa kuimba mapambio ya kwamba wana imani na JPM.
Hakutskiwa kuzuia uingizwaji wa sukari kwa ghafla (kuanzia leo). Masuala ya kiuchumi huwezi kufanya drastic channge bila kuleta athari kwa wananchi. Kwahiyo Rais angeweza kutoa mwezi mmoja under ceteris peribus ili watu wajipange.
Kisha hakupaswa kuzuia sukari yote kutoka nje. Alitakiwa kuruhusu iingie kiasi fulani kucover deficit. Kumbuka demand ya sukari nchini ni tani 420,000 lakini uzalishaji wa sukari kwa viwanda vya ndani ni tani 300,000 tu. Kwahiyo tuna deficit ya tani 120,000. Hizi Rais Magufuli alitakiwa aruhusu ziendelee kuingizwa.
#PILI
Kwa kuzuia sukari kutoka nje, wafanyabiashara wakubwa (tycoons) wametumia mwanya huo KUMHUJUMU Rais. Wamenunua stock yote ya ndani na wanaitoa kwa kujisikia, wakijitetea kwamba uhaba wa sukari unatokana na kuzuiwa sukari kutoka nje. Nahati mbaya Rais JPM nae akaingia ktk mtego huu. Akaagiza serikali kununua sikari tani 100,000 (kwa mujibu wa Waziri mkuu) ili kucover hiyo deficit iliyosemwa kuwa ipo. Another WRONG APPROACH.
Kama ni kamari tunasema kete ya JPM imeliwa. Hawa "matycoon" walikua wanamtega JPM na bahati mbaya hakuelewa huo mtego. Akaagiza serikali inunue hiyo sikari iliyopelea. Hili ni kosa. Rais hakutakiwa kuiambia serikaki inunue sukari kucover deficit. Alitakuwa awape hao "matycoon" msalaba huo waubebe wenyewe ili aweze kuwawajibisha. Waswahili husema mchawi mpe mwanao akulelee.
Ikiwa hawa matycoon wanaojiita "wadai wa sukari" wangeruhusiwa kuagiza hiyo sukari iliyopelea lazima wangetoa na ile waliyoificha, ili wasionekane waongo. Lakini kwa kuwa serikali imejitwika msalaba huo, hawa jamaa watakaa kimya na hiyo sukari ya nje ikifika hawatatoa ya kwao waliyoficha.
Kwahiyo sukari ya nje itakuja lakini bado tatizo la sukari litaendelea kuwepo. Kama huamini subiri wiki ijao ifike then uone kama bei ya sukari itapungua madukani. Hii ni trick ambayo serikali wameshindwa kuishtukia.
#TATU
Serikali kutumia ubabe kutatua changamoto ya sukari, WRONG APPROACH. Uchumi ni sayansi, na changamoto zake hutatuliwa kwa mbinu za kisayansi si ubabe. Ukitaka kuamini ubabe hausaidii kwenye uchumi kamuilize mzee Mugabe.
Katika Ulimwengu wa ubepari ambapo njia kuu za uchumi zimeshikiliwa na watu binafsi ni ngumu serikali kutumia ubabe na kufanikiwa. Hawa matycoon wanachofanya sasa hivi ni kutunishiana misuli na serikali lakini anayeumia ni mwananchi.
Kwa mfano leon nilikua Nzega jamaa mmoja wa duka la jumla alikua akiuza sukari mfuko wa kilo 25 kwa Shilingi 54,000/=. Baada ya muda akafunga duka kwenda kula. Aliporudi akasema mfuko ni 60,000/=. Yani kajisikia tu kupandisha baada ya kuona wateja ni wengi.
MY TAKE.!
Hii ni vita kati ya mabepari against serikali. Vita hii inaweza kuchukua muda mrefu kuisha huku wananchi wakizidi kiteseka maana wao ndio wahanga wakuu. Na ubaya ni kwamba hawa mapepari wana mbunu nyingi "chafu" za kupambana na dola. Hata kama watashindwa ktk vita hii lakini watakua wameshaumiza sana wananchi.
Kwahiyo mwambieni Rais JPM asome kdg kuhusu CAPTAIN OF INDUSTRY ataelewa kuwa ubabe sio mbinu sahihi ya kukabiliana na changamoto za kiuchumu. Kuna mambo yanahitaji ubabe lakini si uchumi. Mimi binafsi naunga mkono ubabe kwenye baadhi ya mambo lakini sio masuala ya kiuchumi. Uchumi una formular zake, una principle zake. Letz abide the formulars.
Huko Amerika wakati wa Sugar Revulution "matycoon" wa huko walihujumu serikali zao hadi kuhakikisha viwanda vyote vya sukari vya serikali vimekufa ili waruhusiwe kuanzisha vyao maana vya serikali vilikua vinawawekea "kauzibe"
Sasa sitaki na sisi tufike huko. Japo tunaweza kufika huko tusipokua makini. Wale rafiki zangu wanaoimba WANA IMANI NA MAGUFULI kwenye kila afanyalo inabidi wakae kimya kidogo kipindi hiki wasije wakatuponza. Au wakizungumza wamshauri JPM kitaalamu na apime kabla ya kuchukua maamuzi.
Narudia kusema; Kumshangilia Rais na kuimba kuwa una imani nae hata anapoteleza humsaidii, unampoteza. Masuala ya kiuchumi hayatatuliwi kibabe. Lazima JPM akubali kuwa yeye ndiye aliyekosea (from the first attempt) hadi tulipofikia. Si lazima akiri hadharani kuwa alikosea. No. Anapaswa kujua Moyoni kuwa yeye ndiye kiini cha tatizo la sukari nchini.
LENGO lake lilikua JEMA lakini akatumia APPROACH isiyo SAHIHI. Akatuponza.
Kwahiyo atafute wadau wa sukari akae nao na kujadili suluhisho. Awaruhusu waingize sukari lakini ktk kiwango cha kucover deficit tu, na azuie serikali isiendelee kuigiza sukari nchini. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumesolve tatizo la sukari, wakati huo tukijipanga kutafuta long term plans ili tuzalishe sukari ya kujitosheleza na kuacha kuagiza kutoka nje.