Rais Magufuli Kwanini Hujamkataza Mwakilishi Wa Sikonge Kufanya Siasa Nzega Wakati Umekataza?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,058
Siamini kwamba mtukufu Rais hukumsikia yule mheshimiwa sana aliyeanza kukinadi Chama Cha Mapinduzi wakati mkutano wako hapo Nzega ulikuwa ni wa kiserikali na siyo chama.

Pamoja ukweli kwamba dakika tano baada ya kuanza kuongea watu walianza kusambaratika, bila shaka wengi waliona unafanya marudio ya juzi na jana kuhubiri kuhusu watumishi hewa, mishahara hewa n.k

Lakini kubwa zaidi ni vitisho kwa wanasiasa wa upinzani unaodhani wanakukwamisha, ila ingekuwa vizuri ungemtisha mwakilishi wa Sikonge pamoja na kwamba alikuwa anakutukuza chama chako lakini pale hakustahili.

Hongera mapokezi mazuri ikiwemo ukarabati wa zimamoto wa Ikulu ndogo, hata halmashauri leo wamefanya usafi. Lakini komesha siasa kwenye mikutano yako au waruhusu na wengine wafanye siasa maana wana hamu nayo.
 
Tanzania bado haijapata raisi! Tukipata raisi tutawaambia kwa sasa tuna Waziri mkuu tu
 
Tanzania bado sana katika suala la haki, ili uwe na haki unapaswa kuwasifia watawala

KUMBE NDIO MAANA HATUNA AMANI AFRICA
 
Uongozi ni hekima amboyo imekuwa bidhaa adimu sana awamu hii.Hapa ni mwendo kasi tu
 
bado tuna safari ndefu. hasa ukijua kuwa chama ni kilekile hakiwezi kuwa na jipya. tunavyokwenda ni sawa na mtu ageukie kulia,kushoto, nyuma na mbele, lakini mtu ni yuleyule. ila sisi tunaona ndiyo mabadiliko
 
Kuwa kiongozi haihitaji kuwa na elimu kubwa. Hata alie maliza elimu ya msingi anaweza kuwa kiongozi mahiri.
 
Back
Top Bottom